Gharama ya kutuma fedha kupitia mitandao kwa sasa ni ghali

Na wanang'ang'ania zile sehemu nyeti kama simba. Simba wakati wa kuwinda akishika winda, anakaba koo kwani anajua windo haliwezi kujitetea kirahisi. Serikali nayo inajua ''wadanganyika'' ni mafukara wa kutupwa, hivyo suala la kuhemea kwa kutumiana visenti haliepukiki. Wanang'ang'ania hapo hapo. Mpaka siku ''mdanganyika'' atakapoamka na kujikomboa tusitegemee mambo kujibadilisha yenyewe.
Hahahahah kujikomboa kwenu si kulia lia na kutafta huruma😅😅😅!!! Dawa nia kuanzisha mgomo baridi mnasusia kutuma hela mitandaoni nchi nzima na kukimbilia miamala ya benki!

Hata watumiaji wakipungua by 40% tu kwa mwezi mmoja ni pigo tosha kwa hao dhalimu na watunga sera za kipuuzi!
 
Gharama ya kutuma fedha kupitia mitandao kwa sasa ni ghali mno na inatukatisha tamaa. Kutuma mathalani Tshs.1m/= kwa anayetuma anakatwa Tshs.16,000 na anayepokea anakatwa Tshs.14,000.

Hivi kweli ni haki?. Kwa Mtanzania wa kawaida kiasi hicho anaweza kununua madebe matatu ya mahindi kwa ajili ya familia au kilo 4 za nyama kwa ajili ya familia. Nina imani watu wengi watahamia Benki na kuanzia sasa mimi binafsi nimeacha kutumia mitandao kwa ajili ya kutuma fedha.

Uamuzi uliofanywa na Serikali ulikuwa uamuzi ambao hauna manufaa kwa wananchi.
Wapinzani ndio Wamesababisha KUPITISHA HII SHERIA BUNGENI SAFI SANA
 
Na wanang'ang'ania zile sehemu nyeti kama simba. Simba wakati wa kuwinda akishika winda, anakaba koo kwani anajua windo haliwezi kujitetea kirahisi. Serikali nayo inajua ''wadanganyika'' ni mafukara wa kutupwa, hivyo suala la kuhemea kwa kutumiana visenti haliepukiki. Wanang'ang'ania hapo hapo. Mpaka siku ''mdanganyika'' atakapoamka na kujikomboa tusitegemee mambo kujibadilisha yenyewe.
🤣🤣🤣
 
Gharama ya kutuma fedha kupitia mitandao kwa sasa ni ghali mno na inatukatisha tamaa. Kutuma mathalani Tshs.1m/= kwa anayetuma anakatwa Tshs.16,000 na anayepokea anakatwa Tshs.14,000.

Hivi kweli ni haki?. Kwa Mtanzania wa kawaida kiasi hicho anaweza kununua madebe matatu ya mahindi kwa ajili ya familia au kilo 4 za nyama kwa ajili ya familia. Nina imani watu wengi watahamia Benki na kuanzia sasa mimi binafsi nimeacha kutumia mitandao kwa ajili ya kutuma fedha.

Uamuzi uliofanywa na Serikali ulikuwa uamuzi ambao hauna manufaa kwa wananchi.
Wewe una pesa unatuma pesa zote hizo?

Mbona hata ATM ukitoa hizo pesa au ukitolea ndani gharama ni kubwa kama kawaida..Acha ulalamishi lipa kodi upate maendeleo.
 
Kuna kipindi nilienda Mtwara nikashangaa sana yaan bodaboda anatoka Newala anapeleka Masasi 10m sasa naona walikua sahihi,
Makato ya sasa ni makubwa mno
Utajua sasa kuwa yanawezekana kabisa
 
Gharama ya kutuma fedha kupitia mitandao kwa sasa ni ghali mno na inatukatisha tamaa. Kutuma mathalani Tshs.1m/= kwa anayetuma anakatwa Tshs.16,000 na anayepokea anakatwa Tshs.14,000.

Hivi kweli ni haki?. Kwa Mtanzania wa kawaida kiasi hicho anaweza kununua madebe matatu ya mahindi kwa ajili ya familia au kilo 4 za nyama kwa ajili ya familia. Nina imani watu wengi watahamia Benki na kuanzia sasa mimi binafsi nimeacha kutumia mitandao kwa ajili ya kutuma fedha.

Uamuzi uliofanywa na Serikali ulikuwa uamuzi ambao hauna manufaa kwa wananchi.
Tutarudi tu kujipanga kwenye mabenk mkuu hamna namna
 
Naona kila mtu anatoa mfano wa M. 1 . Lakini ingependeza zaidi zifafanuliwe gharama za kutuma na kutoa elfu 5 , elfu 10 pia.
Maana hizi ndizi zinatumiwa sana na walio wengi.

Tukumbushane tu awali gharama za kutuma elfu 10 ilikuwa 350 ambayo ni karibia asilimia 5 ya muamala husika na gharama ya kutoa elfu kumi ilikuwa 1450 ambayo ni zaidi 14% ya muamala.

Lakini kutuma 1M gharama ilikuwa 3500 ambayo haifiki hata 1% ya muamala na kutoa 1M ilikuwa elfu 8,000 ambayo pia haifiki hata 1% ya muamala.

Elfu 5 , elfu 10 ndizo zinazotumwa sana na wanyonge . Hivyo sisi wanyonge makato makubwa tumelogwa nayo sana na tushakuwa sugu.

Tuwekeeni makato ya sasa ya kutuma na kutoa elfu 5 elfu 10. Tuone sisi wanyonge tupo ktk hali gan.
 
Kwa hiyo nikitaka kumtumia mtu Million1 ili apate kama ilivyo niweke Millon1 na elfu30...

Nyingi sana...

Kutoka elfu7.5 mpaka elfu30...
 
Back
Top Bottom