Gharama ya kuweka mfumo wa umeme

Sijakosea hesabu bali type error.hapo kwenye pair namanisha roll.

*2.5 mm roll 3
*1.5mm roll 6
 
mkuu, ukipata bei hiyo naomba u-share na mimi
 
Habari wakuu,

Naomba msaada wa kujuzwa makadirio ya gharama ya kufanya wiring kwa nyumba ya vyumba 4 (vyumba 4, sebure, dining, stoo na jiko), pamoja na vifaa vinavyohitajika.

Natanguliza shukran zangu za dhati.
Milioni moja inatosha kila kitu, kuanzia Vifaa mpaka gharaama za ufundi na kulipia kabisa TANESCO kama nyumba yako haiitaji nguzo
 
Wastani chumba nne unatakiwa kuandaa pesa isiopungua lakinane na nusu hapo nyumba itakua imetimia , angalizo hela hiyo haitahusika na mfumo wa Ac, laki tatu na nusu au tatu ni ya fundi , laki tano ni ya vifaa wasiliana nami 0652670595/0773120431
Main switch 6 way
Rcd
Earth rod
1.5mm²
2.5mm²
Bado switches
Lamp holder
Laki tano ndogo kwavifaa
 
Duh,
Embu changanua bas mkuu tuone
Katika wiring, vifaa ambavyo huwa vina bei kubwa ni Main switch, Chuma cha Earth, na waya wa kupokelea umeme pekee.
Ila vifaa vingine kama nyaya, bomba na switch huwa vina bei ya kawaida sana kati ya 500 mpaka 2500.
Kwahiyo gharama ya waya huwa inatajwa kwa mita moja hivyo gharama halisi itakuwa kulingana na urefu wa waya utakaotajiwa na fundi wako.
Gharama za kuunganisha umeme TANESCO kama huitajiki kuwa na nguzo Hazizidi Laki nne, ambapo gharama halisi ni Tshs. 320,960 baada ya kupewa Control number pia utapaswa kumlipa mkandarasi gharama za mchoro ambapo utalipia mchoro ambapo ni kati ya 20,000/= mpaka 50,000/= kutegemea na wepesi wa mdomo wako kuongea na mchoraji.

NB:
Hakikisha fundi akutajie idadi ya vifaa vinavyohitajika na ukanunue Mwenyewe usimpe pesa fundi akanunue hata kama unamwamini kiasi gani.
Pia wakati wa zoezi zima la wiring unapaswa uwepo site maana wana tabia ya kuagiza vifaa vingi ambavyo hawavitumii vyote ili wakauze.
Nakushaauri tumia bidhaa za Tronic maana ndiyo wanafanya vizuri kwenye upande wa ubora
 
Ahsante Mkuu,
Sijafikia hiyo hatua nadhani kwenye mwezi wa kumi panapo majaaliwa nitafikia. Hizi gharama zinahusisha na kutindua pia?
 
Ahsante Mkuu,
Sijafikia hiyo hatua nadhani kwenye mwezi wa kumi panapo majaaliwa nitafikia. Hizi gharama zinahusisha na kutindua pia?
Hakuna haja ya kutindus Mkuu kama mwenye nyumba utakuwa umejipanga vyema kwenye ujenzi wa nyumba yako.
Hakikisha kabla fundi hajaweka Plaster umeshalaza bomba na kufunga box kabisa kulingana na matakwa ya wiring ya nyumba yako.
Hii itakupunguzia gharama na usumbufu katika wiring maana kazi itakayokuwa imebaki ni kutandaza nyaya tu kulingana na njia ambazo tayari umekwishaziweka hapo awali
 
Sijapiga plasta bado Mkuu lakin hata hizo bomba na switches (sockets) si ni lazima tofali? zitinduliwe kwanza
 
Wastani chumba nne unatakiwa kuandaa pesa isiopungua lakinane na nusu hapo nyumba itakua imetimia , angalizo hela hiyo haitahusika na mfumo wa Ac, laki tatu na nusu au tatu ni ya fundi , laki tano ni ya vifaa wasiliana nami 0652670595/0773120431
Nina mashaka na hiyo bei ya vifaa labda visiwe tronic
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] yani wiring ya nyumba unakununue waya za kupima.upo serious kweli wewe.taa za nnje tu zinamaliza pair moja ya waya.alafu wewe unaongelea habari ya kupima waya.
 
Ahsante Mkuu,
Sijafikia hiyo hatua nadhani kwenye mwezi wa kumi panapo majaaliwa nitafikia. Hizi gharama zinahusisha na kutindua pia?
Utapigwa mchana kweupe kaka.hakuna wiring ya ivyo.

*main switch dogo(6 way-ya kujibana)
Tsh 80,000.

*2.5 mm wire(1pair) - Tsh 240, 000.
*1.5 mm wire(1pair)-Tsh 135, 000.
*Circuit breaker- Tsh 45, 000.
*Earth load - Tsh 50, 000.
* Bomba -70 = Tsh 105, 000.
*10 mm(tuweke tu mita 5-Tsh 50, 000.

Hapa tu ishafika laki 7.

Bado swich socket,light switch, holder, squal box.

Hii ni nyumba ya wiring ya kimaskini sana ndo inakuja ela iyo maana hakuna wiring ya nyumba kwa sasa utumie pair moja ya 1.5mm.

Acheni kuwadanganya watu kuhusu wiring[emoji23][emoji23][emoji23]
 
Mie sio mtaalam,
Ngoja ministrant aje aangalie hizi hesabu.
 
Circuit breaker unanunua ya kazi gani wakati inakuwa ipo combined kwenye main switch za siku hizi kama zile za Tronic?
Hizo bomba 70 zote za nini ikiwa kila bomba moja inakuwa na Futi 10 na kila moja inauzwa 1,500 au unafanya wiring kwenye godown?
Kwa kifupi kama fundi wako alikutajia idadi hiyo ya vifaa amekupiga pakubwa sana, au kama wewe ni fundi basi nawaonea huruma sana wanaofanya kazi na wewe.
Nimefanya wiring recently nanimejifunza mengi kupitia tabia za mafundi kuongeza masifuri. Vifaa vingi vilibaki ina maana nisingekuwa site ningepigwa na kitu kizito kichwani tena chenye ncha kali
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…