Usalama uko wa kutosha, naona wapo wenzio wanaofanyia kazi Kitangali (Newala DC).
Mtaa mzuri kwako ni PCCB au maeneo yaliyo karibu na barabara ili iwe rahisi kwako kusafiri asubuhi kuelekea kibaruani.
Bei za vyumba ni rafiki, unachagua standard yako, mfano vipo vya 10k, 20k, n.k.
Lakini sehemu rafiki ya wewe kuishi kiusalama na isiyo na uswahili mwingi lazima upate sehemu ambayo kodi haipungui 30k hadi 100k.
Vyumba unalipia kwa mwezi au miezi 2, 3, 6 na kuendelea. Kwa mara ya kwanza unaweza lipia kwa miezi mitatu au zaidi, baada ya hapo unalipia kwa muundo uuwezao.
Nyumba za kupanga ni nyingi sana kipindi kama hiki kisicho cha msimu wa Korosho, hivyo unajichagulia upendavyo.
Utapata chumba kupitia kwa mwenyeji wako au dalali.
Huko hakuna ule utaratibu eti bila dalali haupati chumba cha kupanga.