Gharama za kumuuguza Mzee zinaongezeka. Sisi tumeshachoka kwa kweli. Bora tu achukuliwe

Gharama za kumuuguza Mzee zinaongezeka. Sisi tumeshachoka kwa kweli. Bora tu achukuliwe

Na Mola wako Mlezi ameamrisha kuwa msimuabudu yeyote ila Yeye tu na wazazi wawili muwatendee wema. Mmoja wao akifikia uzee, naye yuko kwako, au wote wawili, basi usimwambie hata: Ah! Wala usiwakemee. Na sema nao kwa msemo wa heshima

Hii ni Qur'an inatuamrisha haya
Kumbuka wewe ulivokuwa mtoto huenda ulikuwa msumbufu sana ila wazazi wako walikuvumilia iweje leo wewe huwezi kumvumilia mzazi wako?

Yawezekana angekuwa tajiri mkubwa tu lakini alisacrifice akakulea wewe kwa pesa zake leo hii iweje yeye ndio sababu ya wewe kupatikana lakini unamdhalilisha kiasi hiki.

Najivunia kuwa Muislamu kwani Uislamu umetufunza yote haya.
Na yeye amezaa vitamrudi mara 100 yake.
 
Shukuru sana mzee yupo hai wenzio wanatamani wawaone wazazi wao hata sekunde moja haiwezekani
 
Hiyo ni laana ukichunguza iko ndani ya familia pengine hata huyo Baba yenu alishawahi mfanyia Mzee wake haya na nyie bila kujielewa mnaendeleza kizazi cha laana badala ya kuikata minyororo ya laana hakika hiyo laana itakutafuna subiri bakora zako kutoka Kwa hao unaowaita watoto wako.
 
Kuna kipindi pia aliumwaaa.... tukafikia hatua tukasema bora tu arudishe number maana sasa inakuwa changamoto kwetu. Akaja akapona. Shida ikawa pale pale. Hakuna afadhali akiwa mzima shida akiugua shida. Ni msumbufu sana.

Sasa this time anaumwa tena. mwezi wa 3 huu amelala tumehamisha hosp zote. Tunagharamia ukimwangalia age yake nayo imeenda sana. 90 plus. Anataka aendelee kuishi kufanya nini hapa duniani? Sasa tunatumia pesa ambazo zingesaidia wajukuu wake kumtibu mgonjwa mbaye kwa kweli ameshakula chumvi ya kutosha hapa duniani. Mwisho wa siku tunamuona tu kama chuma ulete. Maana kila pesa zetu zinaenda kwenye matibabu yake. Meno yake yameshatoka, anaishi kwa shida. Anaanikwa tu juani kama mjusi ila bado anataka aendelee kuishi. Unajiuliza aishi kufanya nini hapa duniani? Mbona alishamaliza kila kitu?

Sasa inafikia kipindi tunasema bora tu akapumzike nasi tupumzike kidogo maana atatufilisi kwa kweli. Mimi nimeshauza gari moja, nimechukua mkopo, nimekuwa sasa nina madeni ile mbaya. Kwa mabro wengine nao.. ishakuwa shida. Maana tulishampeleka mpaka India kipindi fulani. Wakatwambia kwa huu umri asifanyiwe hayo matibabu maana kinga zake nazo zimekosa nguvu. So alilazwa tu akipewa madawa miezi mitatu. Gharama kubwa ilikuja kwetu. Akarudi amekuwa tia maji tia maji kama gari la mkaa trip moja shamba nyingine gereji.

Ila bado mbishi sana, bado anataka atibiwe na kupelekwa hosp za gharama, sasa mzee si atatuacha watoto wake tumefilisika halafu ndo afe? Hapo tutakuwa tumefanya nini? Nahitaji ushauri wenu kwa kweli hili jambo limenifika hatua nimechoka sana. Sipendi unafiki... hii hali ni ngumu sana maana sasa hata ukiona simu toka kwa ndugu unashindwa kupokea maana huchelewi kuambiwa sasa tuchangie kila mtu atoe 700,000 kuna vipimo na matibabu flani tena yanatakiwa.
Kama unemchoka mnyonge mpaka afe uje uone matokeo yake
 
Mkuu.. wewe huujui uislamu kuliko mimi. Ungenyamaza tu ili usije leta mjadala wa kidini hapa. Mimi toka babu yangu alikuwa sheikh, mufti na alhaj.

Wewe maamuma tu unataka jifanya unaifahamu dini na mistari ya kukariri kuliko watu wenye uelewa wa dini? Acha huo upuuzi hapa tunaongea kisomi siyo kimaamuma.
Nawe utafanyiwa mabaya zaidi. Laana hiyo haikuchi kamwe.
 
Sasa this time anaumwa tena. mwezi wa 3 huu amelala tumehamisha hosp zote. Tunagharamia ukimwangalia age yake nayo imeenda sana. 90 plus. Anataka aendelee kuishi kufanya nini hapa duniani?
Kufeni nyie na ibilisi wenu mwachieni Mungu kazi yake msimuingilie
 
Badala ya kumshambulia mtoa mada, ni vyema mkamchangia fedha kwenye account yake ya Benki ili akamuuguze baba yake.

Na wengine nimewaona mnajiita maparoko humu na mmetoa risala ndefu za masikitiko. TOENI PESA.

Ni kweli mtoa mada ametoa maneno makali. Amekosea, lakini kasema ukweli mchungu.

Sasa toeni hizo hela. Nashauri aweke account number yake hapa, si ajabu wote mtakimbia na kutimka wakati mnajifanya mnazijua biblia.

Shenzi sana. Vinginevyo muacheni asikitike. Anapitia magumu.
 
Nahitaji ushauri wenu kwa kweli hili jambo limenifika hatua nimechoka sana. Sipendi unafiki...
Kiongozi mimi nimekuelewa japo najua wabongo walivyo wanafiki watakulaumu sana. Sasa wewe fanya hivi rudi kwa wazee waelewa wa kijijini kwenu hlf uwape haya maelezo itakuwa imeisha hiyo. trust me.
 
ndio. ntulikaa chini na kuelezana ukweli wa mambo. kwanza niliwaambia hapao story za kukaa kama lump of pudding sitaki. 4 days out of 7 lazima wafanya mazoezi ya angalau 60 minutes ya kutembea. nashukuru waliona umuhimu wa hilo na wanafanya na wameona matunda ya hayo mazoezi. wamepunguza uzito mwigi na kufurah kuwa hai.

pili tumeelezana kuwa u are above 70 now, ukweli ni kwamba huko mnapo kwenda ni kufupi kuliko mlipo toka. hivyo basi tusiwe na unrealistic expectations pamoja na jitihada za makusudi za kulinda uhai lazima tukukubali kutokuweka kifo mbali sana.

tatu ni kwamba if so ikitokea case ya cancer there are no negotiations hapo tunajiandaa kissaikolojia kuwa mnayeya. tutakachofanya ni kuongea na doctor njia za kupunguza maumivu but that business of sijui enda india south africa halipo.

nne, if it so happens kwamba upo kwenye life support, ikipita one week na bado ngoma ngumu tunavuta plug. haman point yakukuweka hai kwa mashine wakatu u r already dead wood.

tano, utakapo kufa ndipo tutakapo zika. kama wataka kuzikwa kwenu vijijini waambie ndugu zako watagharamikia au kama vipi acha fungu la hela kabisa. no expensive coffin will be bought for u nor will we spend money kujenga kaburi. ur dead there is no need to speed money recklesly. kama upendo tutakuonyesha mkiwa hai not when u dead.

nashukuru wazee ni waelewa na all that is known hadi kwa ndugu so maisha ni mwake kabisa no presha kila kitu kinajulikana if they so pass away.
Hahahahaha we endelea kuchakata mbususu tu....kwenye maadili zero kabisa
 
Hahahahaha we endelea kuchakata mbususu tu....kwenye maadili zero kabisa
Sio kwamba maadili zero. Tatizo binadamu mnakuwa na unrealistic expectations. Sasa mtu umeshagonga 75 lakini unataka kiweka kifo mbali huo ni upuuzi.

Haya mambo ya kwenda india watu wauze nyumba alafu mtu anarudi anakaa miezi mitano anayeya ni upuuzi. Madaktari wenyewe wameshakuwa mawakala wa mahospital hawa.

Maisha matamu una afya njema lakini hii trip home trip nyumbani hapana kwa kweli
 
Badala ya kumshambulia mtoa mada, ni vyema mkamchangia fedha kwenye account yake ya Benki ili akamuuguze baba yake.

Na wengine nimewaona mnajiita maparoko humu na mmetoa risala ndefu za masikitiko. TOENI PESA.

Ni kweli mtoa mada ametoa maneno makali. Amekosea, lakini kasema ukweli mchungu.

Sasa toeni hizo hela. Nashauri aweke account number yake hapa, si ajabu wote mtakimbia na kutimka wakati mnajifanya mnazijua biblia.

Shenzi sana. Vinginevyo muacheni asikitike. Anapitia magumu.
Wabongo wanakusaidia kwa maneno tu 😆🤣🤣,hao maparoko na masheikh ndio majanga watajifanya kukupa mistari ila pesa ni hapana.

Wanajidai wana ogopa laana,mbona Magufuli walikua wanamuombea kifo hawakudai ni laana,watu ni wanafiki walio kubuhu.
 
Ahaaa eti ni mbishi abataka kuisha dah. Wacha babu aishi. Kuna siku uta miss hata sauti yake, vituko vyake etc, huyo hafi leo mpaka afikishe 110yrs
 
Back
Top Bottom