Gharama za kumuuguza Mzee zinaongezeka. Sisi tumeshachoka kwa kweli. Bora tu achukuliwe

Na yeye amezaa vitamrudi mara 100 yake.
 
Shukuru sana mzee yupo hai wenzio wanatamani wawaone wazazi wao hata sekunde moja haiwezekani
 
Hiyo ni laana ukichunguza iko ndani ya familia pengine hata huyo Baba yenu alishawahi mfanyia Mzee wake haya na nyie bila kujielewa mnaendeleza kizazi cha laana badala ya kuikata minyororo ya laana hakika hiyo laana itakutafuna subiri bakora zako kutoka Kwa hao unaowaita watoto wako.
 
Kama unemchoka mnyonge mpaka afe uje uone matokeo yake
 
Nawe utafanyiwa mabaya zaidi. Laana hiyo haikuchi kamwe.
 
Sasa this time anaumwa tena. mwezi wa 3 huu amelala tumehamisha hosp zote. Tunagharamia ukimwangalia age yake nayo imeenda sana. 90 plus. Anataka aendelee kuishi kufanya nini hapa duniani?
Kufeni nyie na ibilisi wenu mwachieni Mungu kazi yake msimuingilie
 
Badala ya kumshambulia mtoa mada, ni vyema mkamchangia fedha kwenye account yake ya Benki ili akamuuguze baba yake.

Na wengine nimewaona mnajiita maparoko humu na mmetoa risala ndefu za masikitiko. TOENI PESA.

Ni kweli mtoa mada ametoa maneno makali. Amekosea, lakini kasema ukweli mchungu.

Sasa toeni hizo hela. Nashauri aweke account number yake hapa, si ajabu wote mtakimbia na kutimka wakati mnajifanya mnazijua biblia.

Shenzi sana. Vinginevyo muacheni asikitike. Anapitia magumu.
 
Nahitaji ushauri wenu kwa kweli hili jambo limenifika hatua nimechoka sana. Sipendi unafiki...
Kiongozi mimi nimekuelewa japo najua wabongo walivyo wanafiki watakulaumu sana. Sasa wewe fanya hivi rudi kwa wazee waelewa wa kijijini kwenu hlf uwape haya maelezo itakuwa imeisha hiyo. trust me.
 
Hahahahaha we endelea kuchakata mbususu tu....kwenye maadili zero kabisa
 
Hahahahaha we endelea kuchakata mbususu tu....kwenye maadili zero kabisa
Sio kwamba maadili zero. Tatizo binadamu mnakuwa na unrealistic expectations. Sasa mtu umeshagonga 75 lakini unataka kiweka kifo mbali huo ni upuuzi.

Haya mambo ya kwenda india watu wauze nyumba alafu mtu anarudi anakaa miezi mitano anayeya ni upuuzi. Madaktari wenyewe wameshakuwa mawakala wa mahospital hawa.

Maisha matamu una afya njema lakini hii trip home trip nyumbani hapana kwa kweli
 
Wabongo wanakusaidia kwa maneno tu 😆🤣🤣,hao maparoko na masheikh ndio majanga watajifanya kukupa mistari ila pesa ni hapana.

Wanajidai wana ogopa laana,mbona Magufuli walikua wanamuombea kifo hawakudai ni laana,watu ni wanafiki walio kubuhu.
 
Ahaaa eti ni mbishi abataka kuisha dah. Wacha babu aishi. Kuna siku uta miss hata sauti yake, vituko vyake etc, huyo hafi leo mpaka afikishe 110yrs
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…