Gharama za kumuuguza Mzee zinaongezeka. Sisi tumeshachoka kwa kweli. Bora tu achukuliwe

pole kwanza , ila ayo ni maneno makali sana , ndo mana unaeza kuta Mungu anakuadhibu.. cha kufanya. msikilize , na umtibie kwa moyo wote uyo ni mzazi wako, ukiwa huna kinyongo , na unamuhudumia kwa moyo wote ,pesa zitakuja tu kaka, pesa zinatafutwa ila mzazi akikutoka kakutoka...
 
Mijitu minafiki hii.

Si ajabu unakuta ndio vinara wa kulawiti watoto wa sekondari.
 
Vizuri bunge lipeleke mswada bungeni wakuwarestisha watu aina kama yeye au hatayule anaamua kwa hiyari yake
 
Una maana wale wote unaowaona na kuwafahamu wanauguza na kiulea wazee wao na kuwajengea mpaka sehemu nzuri za kwenda uani ili wasipate shida na kuwatunza kwa kila kitu ni WAISLAM TUU???

Hata huyo Alha wako sijui nani sidhani kama anakuelewa.
 
[emoji125][emoji125][emoji125][emoji125]nitarudi baadae.....!!!
Fikiria hapo ndo bangi haijaruhusiwa kuuzwa madukani. Je ikiruhusiwa taifa na wazazi wataingia hasara kiasi gani kwa watu wa aina hii ya mleta mada!!
 
Nashindwa kukupa ushauri sababu naona maneno makali sana kwenye maelezo yako kama vile tumamuanika juani kama mjusi, tunamuona kama chuma ulete,ksms gari la mkaa
 
Una maana wale wote unaowaona na kuwafahamu wanauguza na kiulea wazee wao na kuwajengea mpaka sehemu nzuri za kwenda uani ili wasipate shida na kuwatunza kwa kila kitu ni WAISLAM TUU???

Hata huyo Alha wako sijui nani sidhani kama anakuelewa.


Hata wasio waislamu wapo wanaokuwanao bega kwa bega na kuwatunza wazee wao mpaka wanafariki, so, watalipwa hapa hapa duniani, akhera hawana kitu.
 
Unaringia Imani ya babu sijui baba yako kwani uliambiwa watakusaidia kuingia peponi? Ungekuwa imani yako unaifahamu vizuri na unawapenda na kuwaheshimu wazazi wako kama Quran Tukufu inavyosema ungeshakuwa na aibu ukafuta huo uzi kuliko ujinga uliofanya wa kulinganisha uhai wa binadamu (tena baba yako) na pesa ambazo unahonga hata bila kuombwa.
 
Huwa namwangaliaga my son bado ni mchanga wife anavyohangaika nae then nikipitia huu najisemea kesho na keshokutwa anakuja kukuanzishia uzi huku wa kipumbavu
 
Daaa poleni kama walikataaaa... ila wale bima hawaktaagi hela
Hawakataagi hela ila wanaangalia na umri,wakiona unachezea umri wa huyo mzee hawakubali,si unajua wapo kibiashara zaid
 
Hata wasio waislamu wapo wanaokuwanao bega kwa bega na kuwatunza wazee wao mpaka wanafariki, so, watalipwa hapa hapa duniani, akhera hawana kitu.
Ila nyie ndio mtakaolipwa mbinguni?,aisee hii dini ngumu sana
 
Pole sna mkuu..binafsi niliyapitia haya pale muhimbil mzee figo zilifeli..akawa anaenda chuja..hakuna rangi nilio acha iyona....kwa wiki tu ilikuwa inaenda 1 M plus...nilivurugwa haswa...ilibaki kidogo tu nianze kuchangisha lakin sikutaka...yan hapo nina kimeo cha dogo anasoma bila mkopo mliman pale...dah hapo hapo nina mavikoba plus pango la biashara kwa mwezi tu ni laki nane...nilijifunza pombe kali angalau niwe napata usingizi..nikiangali umri wa kuoa umefika 30 plus kidogo..mara nikapata kabinti nikakaweka mimba..afu nikamwambia ucjal..imefika muda wa kujifungua mwanaume nipo home peke angu...nikaplan nikaomba namba ya bimkubwa wake nikampigia nikaongea nae nikamuomba anitunzie mwanae mpaka atakapo jifungua na akimaliza tu ile miez mitatu nitamfata chapu bimkubwa akanielewa nikashukuru sana..basi nikamkimbiza mbeya nikamwachia mpunga bimkubwa wake nae kwenye akaunt yake nilimuekea 1.4M ...dadeki mahar cjatoa na baba mkwe akawa hajui nin kinachoendelea...dah maisha haya...yaan ilikuwa afe mzee au nifee mimi...nilimpqmbania pale muhimbil tokea 2019 na akaja kata moto 2021 december ..ila ndio alinipukutisha haswa...
 
Nilimuuguza mzee wangu kwa uri na thim kwa miaka miwili. Nililazimika kuahirisha mambo yangu yote ili kuhangaikia afya yake na akiwa na kesi nzito na ngumu za kansa na failure ya Figo zote mbili. Katu asilani sikukata tamaa.

Huu ndiyo wakati pekee niliokuwa nikimnyoa ndevu; kumfikisha toilet, kumfunga nepi, kumuogesha kwa kitambaa cha vuguvugu akiwa kitandani mwake, kumgeuza na kuongea nae hata kwa ishara pale kauli yake ilipokata.

Nilifarijika sana kuwa na ukaribu na mzee wangu kwa kiwango kile, nafasi ambayo sikuwahi kuwa nayo, wakati wa ugonjwa wake mapenzi yangu kwake yaliongezeka mara dufu.

Akafariki nikishuhudia kwenye visaidizi vya kupumua Hospitali ya Taifa Muhimbili. Nikapambana na kuupa mwili wake heshima stahiki na kumzika pale alipopenda azikwe.

Nikiona uzi kama huu, natambua kwamba KWELI BINADAMU tumetofautiana sana.

Nilichelea mzee angekuwa hata 100 lakini hakufika umri huo...

umekuwaje mleta sledi. Mwogope Mola wako...omba hiyo roho ya kikatili ikuondoke...
 
Kweli mzazi mmoja anaweza Lea watoto kumi lakini watoto kumi hawawezi.kumlea mzazi mmoja, NI kweli unakuja lalamika hili huku JF
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…