Gharama za kumuuguza Mzee zinaongezeka. Sisi tumeshachoka kwa kweli. Bora tu achukuliwe

Hakuna cha "mercy killing" uuwaji ni uuwaji tu kuondoa uhai wa mtu unasema ni mercy?
 
Neno la Muumba wetu ni amri hivyo ni amri kuwalea wazazi wawili kwa heshima na kuwajali.
 
Niliwahi sikia baadhi ya makabila kuna dawa huwa wanameza..sasa wakifikia hatua ya uzee hawafi haraka..yaani mpaka kuna dua maalumu wanasomewa ndio wanakufa..inaweza kufikia mtu ni mzee mpaka baadhi ya sehemu za mwili kama zinaoza ila bado hakati moto..

Binafsi naamini kila mtu anakufa kwa siku zake..kama siku zake bado msitake kumuwahisha..unless mfanye kama baadhi ya nchi za ulaya kumchoma sindano..kitu ambacho sio sawa.
 
Wewe yasikie tu hawa wanaosem vumilia hawajui eti wanakupa mistari ya Qoran hyo ni theory ukija kweny uhalisia utajua hujui. Sisi kwetu wazee walifikia hatua wakataka wamuwekee baba yao sumu afe lkn ikashindn coz kila mtu alipata ugumu wa kummywesha hyo sumu, mzee akafa kwa wakati wake na watu wakapata ahueni
 
Juz. Nilikuwa Happ seliani hospital kumuona mam ake na jamaa angu ambaye aamelzwa hapo aisee had nikawaonea huruma mnk walimtoa pale na kumpeleka ktk kipimo Cha CT scan ya hospital ya nsk huku nikiona kbsa kuwa mgonjwa huyu awezi kukatisha usiku hajaondoka nilitaka niwaambie kuwa watulie tu mnk sioni dalili ya mam huyu kusurvive kwa jins alivyo kuwa mnk alishindwa had kula kwa takribani week nzima.

Ajabu ilipoa fika saa nane usku yule mgonjwa akafariki nikakumbua ule usumbufu wa kumuamisha amisha na kuanagika nae aisee kuuguza sikia kwa mwinginee tu bi pesa zinatoka jamani.
 
Hoja hupingwa na hoja lete aya inayopinga aliyoyatoa huyo member ikiwa wewe unaijua dini kuliko yeye.

Mtu yeyote anweza kuwa alhaji akishaenda ku hiji makka ,mtu yeyote anaweza pia kuwa mufti maana ni nafasi ya uteuzi wa kiserikali na haizingatii elimu ya dini .

So usitumie hayo kama chaka la kujifichia pinga hoja kwa hoja
 
Kuna tofauti kubwa ya kuzungumza na kufikiria mambo kichwani. Haya mambo ungeyetafakari kichwani tu kwa kuwa ndio ulivyo ila kwa kudiriki kuyatamka umeyapa uhai. Yatakusumbua maisha yako yatakuwa na mwisho mbaya tema mate chini piga magoti omba msamaha. .

Nakuombea Mungu akutie nguvu kipindi hiki kigumu unachopitia ili huu mtihani uweze kuuvuka salama. Pole sana ndugu. .
 
Unataka tukushauri umuwekee sumu Mzee ili afe? Aisee hapana.Kumbuka kuwa Mzee hakuomba mwisho wake uwe wa kuanikwa kama mjusi(kama unavyosema).

Hakuna ayuaje mwisho wake. Siku ya mauti yake itakapifika,atakufa.Kikubwa ni kumtanguliza Mungu Kwa kila jambo na kuwa na subra.Pesa inatafutwa.
 
Kiukweli vizazi vya sasa hivi ni kama watoto wamepoteza kabisa mapenzi kwa wazazi wao.. yani kupoteza gari inakuuma kuliko afya ya mzee wako??

Ukute yeye alijima sana kukusomesha akitegemea siku moja na wewe utajitoa vile alijitoa kwako.. kimsingi punguza upendo kwenye material things kuliko utu

Hiyo itakusaidia kuishi maisha yenye furaha zaidi.. hata mzee akiondoka nafsi haito kusuta isipokuwa itakuwa baraka kwako mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…