Gharama za kumuuguza Mzee zinaongezeka. Sisi tumeshachoka kwa kweli. Bora tu achukuliwe

Mtoto kama wew ndo Bora ubadilishane na kreti la bia

Mtoto hasara kabisa pambaneni na mzee wenu mpaka mwisho
 
chaajabu babu wa watu bado anataka kuishi ndo mana anawaambia nipelekeni hospital mercy killing mpaka mgonjwa atake mwenyewe.
Mercy killing au euthanasia haipo kwa nchi nyingi ikiwemo ya kwetu. Huko Uswisi, Udachi, Ubeligiji nk ndio unaweza kwenda na kuomba kusitishiwa uhai wako.
 
Tukiwaambia tuishinikize serikali Ili kila kichwa kuanzia miaka 18 kitoe 5,000 kwa mwaka Ili tupate Bima hamtaki sasa kila mtu apambane kivyake..

Nilichojifunza Bora kujiandaa kuweka hela ukiwa mzima unless yakukute ukiwa bado hujajipanga maana watoto wenyewe na ndugu ndio hao.
 
Huo ni mtihani wako ukitenda vinginevyo utajizolea laana kama zote..

Kama ni pesa unaweza pata overnight na pesa ni kudra sio juhudi na zinaweza potea sekunde tuu..

Mungu ndio ataamua hatima yake na si vinginevyo.
 
sijajua wewe nimwenyeji wa wapi ,ila hii ni tabia ya sukumaland.
Acha laana wewe unamchokaje mzee wako. kama umechoka waachie ndugu zako wamuuguza
 
Wakati unatapika kamasi ulipokuwa mchanga angelikuwa na akili butu kama hizi wala usingeweza kusurvive mpaka leo maana akili zako zinakuwezesha kuvuka barabara ya kijiji....
Mzee anahitaji matunzo na lazima mumhangaikie
 
chaajabu babu wa watu bado anataka kuishi ndo mana anawaambia nipelekeni hospital mercy killing mpaka mgonjwa atake mwenyewe.
Kikubwa wamlee mzee wao na wawe nae karibu sana dunia isitufanye tuwatenge wazee wetu kiasi hichi , huu ndiyo ule muda wa kuvuna baraka tele maana inakuwa unayapitia yale aliyoyapitia yeye na mke wake wakiwa wanakulea unaumwa kila muda yani hawapumziki wanahangaika kama wehu .

Halafu leo kuna jitu linakuja kuona pesa ina thamani sanaaa kuliko uhai na furaha ya mzazi wake hii ishu inakera sana aisee sanaaa.

Sasa kama ugonjwa tu analalamika je angekuwa amepooza ndo angeweza hata kumsafisha haja zake?
 
Pambavu kabisa , kwahiyo unataka ajiue au!?

Yaani wewe amekulea tangy mimba mpaka ulipojitegemea lkn saiz unavimbisha mbupu kitaa
 
Kuja kwa sheikh yahya hadi kwa mzee wako kusoma kwako lamu na mombasa habadilishi upumbavu wako mkuu.

Nimekuambia hoja inapingwa na hoja weka aya yoyote ya quran inayopinga maelezo ya yule aliyeku quote , haunaweka unabaki kujificha kwenye kivuli cha umetokea kwenye ukoo sijui wa mufti sijui nini.

Ingekuwa umesoma quran ungeelewa kuwa ni dhambi kubwa sana mzazi/wazazi wako waliye wazee wakikuambia jambo ukasema ile "Ah" ya kichini sana inayoonesha kukasirishwa nao na ambayo haijasikika ni dhambi mbaya sana.

Sasa leo hii wewe ambaye alikulea na kuhangaika na wewe usiku kucha na mchana kutwa yeye na mke wake hawatulii kama wehu unaumwa daily wanakutibu unaamka usiku hawalali hawa enjoy penzi lako kisa makelele na magonjwa ya utoto leo unakuja kuwaanika hapa??

Hivi ikitokea amepooza (Allah amuepishie) utaweza hata kumsafisha uchafu wake? Unaona visenti na gari na nyumba vina thamani sanaa kuliko mzazi?
 
Ulichokiongea kina maana kubwa ila wachangiaji wengi hapa watakukosoa sababu hawajastaarabika bado. Nchi Zilizoendelea Kimaarifa Mzee akifikisha umri wa kuanza kutegemea watu pale pale anapelekwa kwenye kituo cha kulea wazee, sababu ni asiwe mzigo kwa wanawe wanaohangaikia kazi masaa 12 kwa siku na kirudi kuanza kulea watoto zao.
 
Tunza sana hili andiko. Kama umejaliwa watoto basi watakuwa mashahidi wako wa kwanza.
Ni Mzazi wako kweli?
Tunamuombea uponyaji..
Mkuu kuwa na kiasi hajapenda kuugua
Mzazi wako ataumia sana akisikia haya..
 
Mkuu subiri ubaki naye hapo peke yako hapo hospital kumkaba na mashuka afe labda roho yako itatulia!!
 

Alhamdulillah ala kul hal..uislamu una raha Sana nami najivunia kuwa muislamu
 
Kauli huumba, huyu mwamba lazima kwenye uzee wake yaje yamrudi haya! Unamsemanmzazi wako kama kiufupi mtu fulani? Kwa nini msiuze mali yake mkaenda kumtibishia?
 
Huyo mzee ndio Israel mtoa roho au?
 
Hii dunia ina watu wabaya sana... Laiti wazaz wangekua wanatuambia jinsi walivyo hangaika kwa hali na mali tulivyo kuwa watoto hatujielewi, hakika tusingefikia hatua ya kuchoka kumtibia mzaz kias cha kutamani afe...
Ok usihofu soon atakufa ili pesa zako tamu zisitumike tena ktk matibabu, ila nina uhakika Mungu atakufanyia jambo na utaona ni heri hili ulilonalo
 
Vitu vingine hupaswi kuvitoa mdomoni si vizuri, muombee kwa Mungu ni baraka moja wapo, yeye aliwalea mpaka hapo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…