Kuwa tu humble na upokee nasaha ulizopewa na Akhi kule. Hata kama ni kweli umetoka katika familia ya Masheikh, unaweza kuwa mjinga vile vile. Unaweza kuwa ulisoma sana mpaka huko Lamu alipotoka Sheikh al-Habib Swaleh bin 'Alawy Jamalul-Layl lakini ukarudi mjinga au ukawa hukupata baraka ya Ilmu uliyoipata au ikawa sehemu kubwa mno ya Ilmu hukuipata pia. Unaweza kweli ukawa umesoma (tena kwa usahihi kabisa) lakini ukapinda hivyo kusoma kwako ikawa hakujakusaidia chochote, na watu wakaipuuza Ilmu yako. Unamjua Wasil ibn 'Ataa? Alikuwa Mwanafunzi wa Imaam Hassan al-Basry (Rahimahullah). Wasil aliachana na Imaam Hassan al-Basry akaenda kwa wanafalsafa huko wakamvuruga mwisho akajitenga na Imaam al-Basry, na ndio akaanzisha Madh-hab ya Mu'utazilah. Alijitenga na Imaam al-Basry licha ya kuwa Imaam Hassan al-Basry alikuwa ni katika Taabi'i wakubwa sana. Kinachoangaliwa ni umesimama sawa? Sasa unafanya au unasema jambo ambalo halipo katika dini, kisha ukiambiwa kwa kurekebishwa, unajitetea kwa kusema wewe ni mjukuu wa Mufti na umesoma mpaka Mombasa na Lamu. Haqq haipimwi kwa hivyo Chizi Maarifa.
Mtabiri wa Nyota Mzee Yahya Hassan Juma kwenda kwa Baba yako kuzungumza "habari za dini ya kiislamu" sio hoja pia.
Hata mimi pia akina Mtabiri Mzee Yahya Hassan ni katika wazee wangu, na baadhi ya Wazee wangu walikuwa ni Masheikh Maarufu tu wa Kisufi (Allah awasamehe makosa yao na Awarehemu). Ila bado kuna wengi katika familia zetu hawafahamu dini. Mimi mwenyewe ni miongoni mwa wasiojua dini hasa ndio naanza kusoma. Mwanzo nami nilijiona najua dini ila nimekuja kugundua sijui kitu, ndio kwanza naanza.
Be humble. Allah atuongoze sisi na wewe pia katika njia iliyonyooka.
Yangu ni hayo tu.