Gharama za matibabu ya wafanyakazi wa ndani wauguapo ni jukumu la nani?

Gharama za matibabu ya wafanyakazi wa ndani wauguapo ni jukumu la nani?

Sky Eclat

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2012
Posts
57,761
Reaction score
216,011
Huduma za afya zina gharama na hii ndiyo sababu watu wengi wanaishi kwa kudra za Mwenyezi Mungu. Wengine wanakwenda kupiga ramli kwa kuanguka na kuzimia bila kujua kuwa hii ni dalili ya hatari na inahitaji uchunguzi wa kitaalamu. Wengi huponea hutoa sadaka kanisani ili waombewe. Kuna wanaokwenda kwa Mwamposa kisa wanaharisha. Hili si kusudio la mada.

Nia yangu ni kuongelea matibabu ya hawa wanaotusaidia kazi za ndani. Kuna wanao ambiwa wajinunulie Bima ya Afya kutoka kwenye mishahara wao. Wengine wanaunganishwa kwenye bima ya familia (Hawa ni wachache sana).

Kuna mama mmoja alimtoa binti wa kazi Dodoma, binti alikua mdogo kama miaka 16. Wazazi wake walimtoa kutokana na ugumu wa maisha wakitegema kurushiwa hata 20,000 kutoka katika mshahara wake kila mwezi.

Yule mtoto alikuwa mgonjwa, alianguka mara nyingi baada ya kuamka asubuhi. Yule mama alimpeleka hospitali. Vipimo vya siku ile vilimgharimu laki tatu na mtoto aligundulika na matatizo ya moyo.

Yule mama alilaani sana kutumia laki tatu hospitali. Alimsimanga binti kuwa kama ulijua ni mgonjwa kwanini ulikubali kuja kwangu. Baada ya pale alimrudisha kwao. Ukizingatia hali za maisha ya wazazi wa binti Yule ni wazi kuwa hawataweza kumtibu mtoto wao.

Tunapotoa ajira kwa hawa ndugu zetu wanaotusaidia majukumu ya kulea watoto na wazazi wetu, tukumbuke pia kuwa wao ni binadamu na kuwe na utaratibu wa kuwasaidia katika matibabu. Mnaweza kushauriana nae apate Bima yake ya Afya.
 
Mshahara unaomlipa mtumishi kwa mwezi hutegemea sana allowance unazompatia.

Kama umekubaliana kumpatia 50,000 Ina maana malazi, chakula, hospital, mafuta ya kujipaka, sabuni na vitu vidogo vingine utampatia ikiwemo nauli ya kwenda na kurudi kanisani au msikitini (if anaenda na ni mbali? Pamoja na nauli siku ya off.

Akiumwa utampeleka hospital, utamtibu na hautamkata mshahara unless ugonjwa wake uwe no endelevu na unaona inakucost na unahisi amekuwa burden kwako basi utampatia nauli ya kurudi pamoja na madai yake if any.

Kama ni wa kuja na kuondoka ina maana ana kwake Mara nyingi mshahara ni laki na nusu plus nauli ya kwenda na kurudi kila siku kwa mwezi akiumwa atajijua sanasana unawajibika chakula Cha mchana anapokuwa kazini.

Tatizo la hawa watu huwa wanajisahau, unamtumia nauli anakuja mjini halafu ndani ya mwezi anaibiwa na mtu sokoni wanamhadaa watamlipa mshahara mkubwa anakutoroka hapo ndio maana wengine wanawaambia Ile nauli wanawakata kwenye mshahara kuwatreat vibaya.

Mie imenikuta sana, binti unamtoa singida anafika analeta upuuzi sema hizo ni ishu za wife huwa nakuta amefura ameshatimua naona wanavyokera kwakweli unamtreat kibinadamu Ila nao wanakuwaga washenzi sana .

Ila ukibahatika msichana mzuri anayejielewa kwakweli utaenjoy mie huwa likizo ya watoto wakienda kwa bibi yao kama wanapanda ndege na dada anakula mwewe Kuna mmoja alikaa miaka mitano mpaka akaolewa.
 
Mshahara unaomlipa mtumishi kwa mwezi hutegemea sana allowance unazompatia.
Kuna wengine dada akiumwa malaria na UTI anamrusha kwao akipona arudi kazini. Asichoekewa ni kuwa malaria ni dalili kuwa watoto wanakuwa exposed kwenye mbu na UTI inaweza kuwa ni uchafu wa choo. Maana yake ni kuwa hata watoto wake wako hatarini kuugua.
 
Wa kwangu alikuja mjamzito hakuniambia na hatukumstukia. Baada ya miezi miwili kabanwa na tumbo ghafla usiku nikamkimbiza rabinisia nikijua ni tumbo tu la kawaida food poisoning. Kumbe ni uchungu wa kujifungua, kajifungua hapo maana kulikuwa hakuna muda wa kumuhamisha hospitali. Mbaya zaidi alilazwa pale siku kadhaa bili ilipoletwa nilichanganyikiwa akili iliniruka sitakaa nisahau kamwe. Niliapa sitokuja kuwa na msichana wa kazi daima
 
In short, mambo ya kiafya ni vema ukachukua jukumu la kumpima kwa gharama zako sababu huyu ni mtu unayemkabidhi sekta muhimu sana ya usafi wa nyumba, nguo, vyombo chakula nk.

Pia unamkabidhi watoto maana ndio atakuwa anashinda nao muda mwingi sana, huwezi kurisk kumtibu vizuri kisa ubahili itacost familia yako.

Ukiangalia mshahara wake hawezi hata kufanya check up ya maana kuangalia UTI, HIV, TB, nk

Lazima tuwe wakweli kwamba Hawa ni watu wanaotoka kwenye maisha ya chini sana, they can't afford better healthcare, wanaishi mazingira magumu ambayo ni rahisi sana kupata maambukizi ya magonjwa.

Kama kweli unataka aishi kwako ni vema ukatumia gharama kumfanyia check up ya maana Kulingana na uwezo wako pia. Lakini lazima tufahamu hela unayompatia kwa mwezi ukisema hiyohiyo utamkata nadhani ataishia kukaa bure kwako bila mshahara maana imagine 50,000 utaenda hospital gani kwa check up hapo haujakuta ana maambukizi yanahitaji dawa? Let's be humans and be realistic.

Huyu mtumishi akiwa na TB ujue wa kwanza kuumwa ni mwanao maana ndio wanashinda wote Tena unakuta wengine ndio wanalala nao pia.

Ukimpeleka kwao atapataje huduma ya afya? Niliwahi kupata binti ana kifafa hatukufahamu, siku tukashangaa ameanguka jikoni anatoka povu, tukakimbiza hospital anasema kwao walikuwa wanampa dawa ya kienyeji walimwambia amerogwa khaa daktari akamcheki akagundua ana kifafa akampa Kuna vidonge anatumia kila siku komoja akakaa fresh tu na kila wiki dawa ilikuwa just 5000 lakini tulimtibia.

Kuna vitu unafanya Kama mzazi tu for the sake of your kids. Yule tulipima mpaka ukimwi na mimba Ila hakujua nilimtonya dokta.

Sisi akija dada mpya tunapeleka check up Ila dokta anapewa maelekezo apime ngwengwe na mimba ili tusije kuhangaika na mtu kumbe tunalea mama mjamzito pale .

So mambo mengine ni kupima tu kipi Bora.
 
In short, mambo ya kiafya ni vema ukachukua jukumu la kumpima kwa gharama zako sababu huyu ni mtu unayemkabidhi sekta muhimu sana ya usafi wa nyumba, nguo, vyombo chakula nk.
Uko sahihi kabisa. Hili la kutopima mimba lilikuja kunigharimu pesa nyingi sana nilijuta
 
Noma unashangaa kwako ndimu hazikai [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] kumbe mimba inataka ndimu
Ni shida. Ila muajiri kubeba jukumu la gharama za huduma ya afya kwa msichana wa kazi napo naona sio sahihi. Huo ni mzigo mkubwa kumbebesha muajiri
 
Ni shida. Ila muajiri kubeba jukumu la gharama za huduma ya afya kwa msichana wa kazi napo naona sio sahihi. Huo ni mzigo mkubwa kumbebesha muajiri
Basi mlipe laki mbili maana najua unaielewa elfu hamsini kwa mwezi mzima na bado atume kwao na ajinunulie hata brazzier, underwear nk.

Kimsingi ukitaka ajitegemee mpe laki tatu ya serikali kima Cha chini itakuwa sawa Ila unapompa 50,000 jamani dah nyie watu aisee.

Imagine anaumwa malaria, anachukua pikipiki kwenda dispensary na kurudi let's say elfu nne, kupima malaria 3000, dawa anabaki na nini?

Najua huwezi kutimiza mahitaji ya mtu mzima lakini umlipe mtu na umpatie marupurupu ambayo yapo equitable na kazi anayofanya.

Dada anaamka saa 11 wengine 10 alfajiri, aandae watoto, apige pasi nguo zote , ahakikishe wamekunywa chai kabla basi la shule halijapita, awasindikize watoto kwenye school bus, arudi aandae chai yenu, bado hajatumwa vocha dukani, Mara nguo hutaki kuivaa akupasie nyingine, yani mpaka mnaondoka ameshachoka hapo ndio anaanza kufanya usafi, afue apike, Yani dah tuwe wanadamu wewe kumtibia tu? Only that???? Tena sio anaumwa kila siku
 
Matatizo yanaanza pale unapolipwa laki tatu na wewe unatafuta dada wa kazi.

Dada mmoja anamuwa mtoto wake na mama mwenye nyumba alimwambia mradi I’m uache na chakula chake.
 
Basi mlipe laki mbili maana najua unaielewa elfu hamsini kwa mwezi mzima na bado atume kwao na ajinunulie hata brazzier, underwear nk.

Kimsingi ukitaka ajitegemee mpe laki tatu ya serikali kima Cha chini itakuwa sawa Ila unapompa 50,000 jamani dah nyie watu aisee.

Imagine anaumwa malaria, anachukua pikipiki kwenda dispensary na kurudi let's say elfu nne, kupima malaria 3000, dawa anabaki na nini?

Najua huwezi kutimiza mahitaji ya mtu mzima lakini umlipe mtu na umpatie marupurupu ambayo yapo equitable na kazi anayofanya.

Dada anaamka saa 11 wengine 10 alfajiri, aandae watoto, apige pasi nguo zote , ahakikishe wamekunywa chai kabla basi la shule halijapita, awasindikize watoto kwenye school bus, arudi aandae chai yenu, bado hajatumwa vocha dukani, Mara nguo hutaki kuivaa akupasie nyingine, yani mpaka mnaondoka ameshachoka hapo ndio anaanza kufanya usafi, afue apike, Yani dah tuwe wanadamu wewe kumtibia tu? Only that???? Tena sio anaumwa kila siku
Na kuna wanao ulizia mpaka kiporo cha wali na kuku cha jana. Hafikirii anavyomtumikisha dada kwa 40,000
 
Huduma za afya zina gharama na hii ndiyo sababu watu wengi wanaishi kwa kudra za Mwenyezi Mungu. Wengine wanakwenda kupiga ramli kwa kuanguka na kuzimia bila kujua kuwa hii ni dalili ya hatari na inahitaji uchunguzi wa kitaalamu. Wengi huponea hutoa sadaka kanisani ili waombewe. Kuna wanaokwenda kwa Mwamposa kisa wanaharisha. Hili si kusudio la mada.
Wa kwangu gharama za matibabu nagharamia.
 
Wa kwangu alikuja mjamzito hakuniambia na hatukumstukia. Baada ya miezi miwili kabanwa na tumbo ghafla usiku nikamkimbiza rabinisia nikijua ni tumbo tu la kawaida food poisoning. Kumbe ni uchungu wa kujifungua, kajifungua hapo maana kulikuwa hakuna muda wa kumuhamisha hospitali. Mbaya zaidi alilazwa pale siku kadhaa bili ilipoletwa nilichanganyikiwa akili iliniruka sitakaa nisahau kamwe. Niliapa sitokuja kuwa na msichana wa kazi daima
Na kichanga na mama yake walikaa muda gani kwako baada ya kutoka hospitali.
 
Kwa mfumo wa afya ulivyo sasa ni bora bima ya afya ikawa ni moja ya mandatory package kwa hawa wafyakazi wa ndani hata kama ni basic tu .
Hii ya unamlipa mtu 50000 kwa mwaka halafu unataka akiumwa ajitibie ni unyama uliopitiliza .
 
Huduma za afya zina gharama na hii ndiyo sababu watu wengi wanaishi kwa kudra za Mwenyezi Mungu. Wengine wanakwenda kupiga ramli kwa kuanguka na kuzimia bila kujua kuwa hii ni dalili ya hatari na inahitaji uchunguzi wa kitaalamu. Wengi huponea hutoa sadaka kanisani ili waombewe. Kuna wanaokwenda kwa Mwamposa kisa wanaharisha. Hili si kusudio la mada.
Ni vizuri wazazi wa msichana wakaweka wazi taarifa za ugonjwa wa binti kabla hawajamtoa, ni kweli huwa tunawasaidia matibabu lakini kuna magonjwa mengine matibabu yakw ni gharama kiasi kwamba hata boss hawezi kuzimudu

Kuna ndugu yangu alipewa msichana kumbr yule binti ana kifafa na familia yake inajua ila hawakusema, jiweke kwenye viatu vya huyo boss

Magonjwa ya kawaida kama malaria, UTI ambayo sio gharama kubwa ni jukumu la mwajiri lakini magonjwa makubwa kama moyo, kifafa, pumu ni changamoto na pia haishauriwi kuwa na binti wa kazi mwenye magonjwa hayo maana ni risk kubwa
 
Wa kwangu alikuja mjamzito hakuniambia na hatukumstukia. Baada ya miezi miwili kabanwa na tumbo ghafla usiku nikamkimbiza rabinisia nikijua ni tumbo tu la kawaida food poisoning. Kumbe ni uchungu wa kujifungua, kajifungua hapo maana kulikuwa hakuna muda wa kumuhamisha hospitali. Mbaya zaidi alilazwa pale siku kadhaa bili ilipoletwa nilichanganyikiwa akili iliniruka sitakaa nisahau kamwe. Niliapa sitokuja kuwa na msichana wa kazi daima
Pole sana, wengine huwa wanatoa mimba halafu anakuja kuugua ghafla unakuta gharama ya kumtibia ni kubwa mpaka unachanganyikiwa ukizingatia wewe mwenyewe unatibiwa na bima sio mambo ya cash
 
Kwa mfumo wa afya ulivyo sasa ni bora bima ya afya ikawa ni moja ya mandatory package kwa hawa wafyakazi wa ndani hata kama ni basic tu .
Hii ya unamlipa mtu 50000 kwa mwaka halafu unataka akiumwa ajitibie ni unyama uliopitiliza .
Siku hizi hakuna wasichana wa kazi wa 50,000 kwa mwezi, hao walikua zamani sana, siku hizi ukiletewa mdada anaanzia laki na themanini mna bagain mpaka mnafika laki na nusu
 
Back
Top Bottom