Basi mlipe laki mbili maana najua unaielewa elfu hamsini kwa mwezi mzima na bado atume kwao na ajinunulie hata brazzier, underwear nk.
Kimsingi ukitaka ajitegemee mpe laki tatu ya serikali kima Cha chini itakuwa sawa Ila unapompa 50,000 jamani dah nyie watu aisee.
Imagine anaumwa malaria, anachukua pikipiki kwenda dispensary na kurudi let's say elfu nne, kupima malaria 3000, dawa anabaki na nini?
Najua huwezi kutimiza mahitaji ya mtu mzima lakini umlipe mtu na umpatie marupurupu ambayo yapo equitable na kazi anayofanya.
Dada anaamka saa 11 wengine 10 alfajiri, aandae watoto, apige pasi nguo zote , ahakikishe wamekunywa chai kabla basi la shule halijapita, awasindikize watoto kwenye school bus, arudi aandae chai yenu, bado hajatumwa vocha dukani, Mara nguo hutaki kuivaa akupasie nyingine, yani mpaka mnaondoka ameshachoka hapo ndio anaanza kufanya usafi, afue apike, Yani dah tuwe wanadamu wewe kumtibia tu? Only that???? Tena sio anaumwa kila siku