Black Thought
Senior Member
- Feb 25, 2015
- 161
- 408
Habarini wakuu,
Kuna mjadala uliletwa humu kuhusu ni nyumba zipi zina gharama nafuu kwenye ujenzi kati ya hizi za kisasa za kuficha bati (‘contempoarary) na zile za kawaida. Ambapo kwa uzoefu wangu nilijaribu kuelezea kuwa kwa kawaida tunatarajia nyumba za paa la kuficha zitatumia tofali nyingi huku bati na mbao zikitumika kidogo sana (maranyingi haizidi nusu) wakati hizi za paa la kawaida zinatumia tofali chache huku zikitumia bati na mbao nyingi zaidi.
Lakini kuna mambo ya kuzingatia
1. Ongezeko la tofali kwenye contemporary house si kubwa sana kulinganisha na utofauti wa mahitaji ya mbao na bati za kupaulia baina ya aina hizi mbili za upauaji wa nyumba.
2. Gharama za mbao na bati kwa ujumla wake zinakupa ongezeko kubwa la gharama kwa nyumba za kawaida kulinganisha na contemporary house.
3. Kuna kitu kinachoongezeka kwenye nyumba za contemporary ambacho ni ‘concrete Gutter’ (mitaro ya kukusanya maji). Ambacho kwa mtazamo wangu nili commet kuwa ndio hasa kinaweza kufanya unafuu wa contempoary uliotokana na roofing ukaja kujilipa (kwa kukalibia au hata kuzidi) kulingana na idadi na namna mitaro ya maji ilivyowekwa kwenye nyumba amabyo kwa namna flani inatokana na ‘spatial arrangement’ ya ndani na namna flani za kuboresha mvuto wa jengo (Contemporary house zinaongezeka mvuto with complexity).
Hivyo basi pendekezo langu lilikuwa ni kwamba kama unataka kujenga kwa kuficha bati na huku pia ukitaka kupunguza gharama ni muhimu kuzingatia mpangilo wa nyumba utakao kufanya uepuke kujenga mitaro mingi kwenye nyumba.
Au unaweza kuepuka kabisa ujenzi wa mitaro kwa kuacha wazi upande wa nyuma ambao ndio maji yataelekezwa huko, na hii ni nzuiri zaidi maana pia itakupunguzia idadi ya tofali ambazo zingehitajika upande wa nyuma huku pia ukiepuka materials kwaajili ya ujenzi wa gutter ambalo lingehitaji zege la nondo.
Na kwakuongeza tu namna hii ya kuacha wazi upande wa nyuma iatakusaidia kupunguza risk ya nyumba kuvuja endapo hukutumia fundi mwenye uzoefu/ujuzi wa nyumba hizi, so risk ya kuvuja itabaki kuwa kwenye maungio ya bati na ukuta (kama fundi ni kimeo).
Kwa maelekezo zaidi juu ya masuala yote yahusuyo ujenzi unaweza kutucheki whatsapp 0717682856.
Unaweza kuona mfano wa hako ka ramani hapo chini (kalichorwa kwa lengo la kusave space na gharama). Kana vyumba vitatu (1master), kiStudy room kidogo, kitchen, dining na public toilet.