Sio lazima aliechora ndio ajenge, lakini angalau kunakua na uhakika wakufanya kwa ubora unaotakiwa kulingana na design.
Na issue ya kupenda cheap, sio tatizo ndio maana nikasema angalau uwe na uhakika na uwezo wa mtu anayefanya kazi. Sio tu kwakuwa mtu ananusu bei basi unamkabizi kazi, kisha baadae unakuja kulalamika umeharibiwa kazi, uliokoa laki tano na unapata hasara ya million tano au zaidi.
Njia nzuri inaweza kuwa kujilizisha na uwezo wa mtu unayempa kazi kupitia watu aliowafanyia kazi. Au unaweza kumpa fundi kazi kisha ukamtumia mchora ramani (architect/engineer) kuja kukagua kwenye hatua muhimu za ujenzi kisha yeye ukamlipa hela ya site visiting tu.