Gharama za Ujenzi kwa Nyumba za ‘Contemporary’ Vs ‘Traditional’ Roof

Nadhani ili kuepuka kuvujiwa nikuacha nyuma wazi ili maji yatiririke bila tatizo
 
Kwa uzoefu wangu, hamna gharama inayopongua, una save kwenye kupaua, unaumia kwenye concrete gutters na slabs za vibaraza, shughuli ni pevu
Issue ya gutter na nimeelezea hapo kuwa ili gharama ipingue inategemea sana na namna gutters zilivyo sanifiwa.
Ishu ya Vibaraza sio lazima viwefunikwe kwa slabs, Vinaweza kufunikwa kwa bati likiwa linefichwa pia.
 
Mkuu Heri kwako ila twende mbele turudi nyuma, nyumba zile kweli za contemporary kweli ile contemporary house bongo ni chache sana,,kwa upeo wangu mdogo,mara nyingi nyumba za contemporary hutawaliwa almost 90% kwa concrete na glass,hata huko juu wabongo tunaforce kuweka bati tena kuna wengine wanajinasibu kuweka bati cheap zaidi kwa vile watu hawalioni ili kukwepa gharama,pasipo kuhusisha factors nyingine ikiwepo hali ya hewa,ubora wa matumizi ya material yenyewe kwa shughuli husika,kutu si rafiki baada ya miaka kadhaa,ukiacha swala la kuvuja pembeni,dawa ni kupiga zege tu,mwite fundi akupe makadirio na ushauri,fit kwny design yako, anza nondo mdogo mdogo,mifuko ya cement,gari kokoto,gari mchanga,pvc,mbao,hela ya fundi material ndogo ndogo,kata mzizi wa fitna ishi kweli kwny contemporary house.vinginevyo wabongo tunafake tu.😀
 
Unaweza kuwa sahihi pia mkuu. Lakini muhimu ni ujuzi/taaluna na uzoefu juu ya kitu kinachofanyika. Hata roof slabs zipo zinazovuja pia. Hizi contemporary zina mambo mengi yanayoweza kufanya zikavuja endapo yasipozingatiwa, na ishu kama bati kupata kutu yes inaweza kutokea endapo roof pitch ikiwa ndogo sana ndio maana huwa inatakiwa slope isipungue walau nyuzi kumi. Kuna vitu vingi sana vya kuzungumza hapa ikiwepo hata aina za bati zinazofaa zaidi, namna ya kutengeneza na kulinda makutano ya bati na kuta ili kusitokee uvujaji pembeni n.k
Ndio maana nikasema kupunguza gharama sio tatizo ila kukwepa gharama mara nyingi huleta gharama kubwa zaidi baadae.
 
Tunauza mbao kwa bei ya jumla.Njoo ofisini kwetu TEGETA tukuhudumie kwa gharama nafuu sana:-
2*2 fut12=2500
2*2 fut12(treated) ya dawa=2800
2*2 fut18(treated) ya dawa=5000
2*4 fut12 treated(ya dawa)=5000
2*4 fut12 isiyo ya dawa=4500
1*6 fut12=4500
1*8 fut12=8000
1*8fut12 ya fisher board(treated)=9500
1*10 fut12=13000
1*10fut 18 fisher board( treated)=15500
2*4 fut18(treated)=9500
2*6 fut12=8000
1*4 fut12=2800
2*6 fut 18=19000
Tunapatikana muda wote kwa namba za simu zifuatazo:-
----0759630751
----0687371138
----0654830416

vile vile kuna huduma ya kuchana,kuranda na kusize mbao inapatikana ofisini kwetu
 
You have spoken my mind.... Sio kuwa tunapenda cheap... Uwezo ndio shida...mkono unapoishia
 
Jamaa umeongea kitu cha ukweli haswaaa!! Contemporary kwa wenzetu ni zaidi ya ile style ya kupaua, ni muundo mzima wa jengo kwa maana kama ulivyosema. Na nia ya contemporary kwa wenzetu wala sio kupunguza gharama! Sasa sisi tumeivamia hiyo style ya kupaua kwa vile wengi wanaoitwa mafundi wanaiuza kwamba inapunguza gharama ya upauaji! Kitu ambacho kinaweza kisiwe sahihi sana, ndo tunaishia kuvujiwa na nyumba kisha tunalaumu kuwa hiyo style ni mbaya!
 
Turejee kauli ya Mzee wetu Hayati Julius Kambarage Nyerere-"Ukweli haupendi kupuuzwa puuzwa"
 
Hizo contemporary ni nzuri sana kwa muonekano, ila nnavosikia zinaharibika haraka zinavujisha (nadhani shida itakua kwa wataalamu wetu) hawajazijulia vizuri....
Kuna jamaa kajenga haina hata mwaka tayari ndani kunavuja
Uko sahihi sana lakini:
1. Hutokana na kutumia watu wasio wazoefu
2. Kutokujua aina ya matirio ya finishing

Mfano kwenye mfereji na maungio ya bati ukutani kunahitaji (1) butmen nyeupe hii hupatikana NABAKI AFRIKA
(2) Membrane cloth hivi hutumika kwa pamoja na hutaona kuvuja wala unyevu.

3. Maungio ya mabati yanatakiwa overlap migongo 3 tofauti na ujenzi wa kawaida
 
Basi shida ipo hapo kwenye utaalamu, swala la kuvuja limekua kawaida kwa hizo nyumba....
Ila kwakweli kwa kutizama zinavutia ni nzuri
 
Inaelekeaaa mkuu unaauzoefu mzur na hz nyumbaaa
 
Basi shida ipo hapo kwenye utaalamu, swala la kuvuja limekua kawaida kwa hizo nyumba....
Ila kwakweli kwa kutizama zinavutia ni nzuri
Shida inaanzia mbali.... Boss mwenye mjengo ana opt kupaua hivyo ili ku save cost, fundi-mchundo anaekutana nae pia anamuaminisha kuwa hiyo ita save costs sana. Mimi kuna fundi alinishauri mapema kabisa kuwa kama lengo lako ni kusave costs, achana na upauaji wa aina hiyo kabisa. Ila kama unachagua style hiyo kwa kuwa unaipenda na unapenda vitu vizuri, na suala la gharama sio shida kwako, go for it.
Evelyn Salt
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…