Gharama za umeme zimepanda lini? Tsh.10,000 kwa unit 72 badala ya 82 imekuwaje?

Gharama za umeme zimepanda lini? Tsh.10,000 kwa unit 72 badala ya 82 imekuwaje?

polokwane

JF-Expert Member
Joined
Dec 16, 2018
Posts
3,361
Reaction score
5,842
TANESCO kuna shida kabisa kwanza umeme unakatika katika hovyo sawa hiyo moja lakin nyingine naona ghafla gharama za umeme zimepanda kimya kimya maana kwa Tsh.10000/ tulipata unit 82 lakini sasa mwez huu Tsh.10000 unit unapata unit 72.

Hii ni hujuma au kuna nini huko TANESCO? Maana TANESCO ndiko kuna wizi mkubwa sana huko. Hii ni kwa wale wateja wa matumuz chini ya unit 75 tarif 0
 
Sometimes ukitaka majibu ya uhakika hatua ya kwanza ni kuwauliza wahusika (direct from the horses mouth) na kama una alternative kuliko kuwasubiri wajibu hapa jaribu kupiga simu / kuwatembelea ofisi zao za karibu.
Wana majibu gani sasa huko kama sio kujibiwa swala lako tunalifanyia kazi halafu unakaa wiki nzima hadi uwatafute, cha msingi wafikiwe kwa namna yeyote ile na wamefikiwa maana hapa JF si wapo? Wajitokeze watoe jibu maana hapa naelekea twitter account ya mama samia kueleza wizi huu maana huko pia wapo na huwa wana respond haraka tu.
 
Iyo elfu 10 kwa tariff 4 ama 0 mbona haiendani na hela iyo,nijuavyo mie ni kuwa Taiff 4 mwisho wa kununua ni elfu 9 na unapata unit 75,sasa izo 82 unapataje mwenzangu.
 
Iyo elfu 10 kwa tariff 4 ama 0 mbona haiendani na hela iyo,nijuavyo mie ni kuwa Taiff 4 mwisho wa kununua ni elfu 9 na unapata unit 75,sasa izo 82 unapataje mwenzangu
Hapana mwisho huwa ni 10, 000 unapata units 77!!kwa hizo 82, ndio na mimi nashangaa
 
Huwa nafanya hivi baada ya kuona hiyo hasara huwa nalipa tsh 5000 napata unit 41 halafu nanua tena tsh 5000 napata unit 41 jumla napata unit 82 inakuwa afadhari kuliko unit 77 kwa tsh 10,000 kwa mkupuo.
Unavyonunua ivyo unanunua ndani ya mwezi huo huo naomba nielewe hilo.
 
Back
Top Bottom