Gharama za umeme zimepanda lini? Tsh.10,000 kwa unit 72 badala ya 82 imekuwaje?

Gharama za umeme zimepanda lini? Tsh.10,000 kwa unit 72 badala ya 82 imekuwaje?

Hapa utakuwa umezima fridge na hutumiii birika kuchemsha chai?..
Ndio maana ni kwa watumiaji wadogo, sana sana, taa, radio, tv na feni.Mimi Nilichofanya , kwanza nilijibana kama mwezi mmoja, nikatumia units 40 nilisafiri kama mwezi hivi huku naendelea kununua, zikafika kama units 70, kwa sasa nina units kama 230!! Na kila mwezi nanunua units 77!! Kwa sasa natumia tu kwa raha zangu kama kawaida, kwani hawawezi nitoa tena, kwani nina akiba ya kutosha sana.
 
Hizo Unit mnazipate wenzetu mbona sisi elf5 tunapata Unit 14!!

Msaada tafadhali
Hii ni bei ya kundi la watu wenye matumizi madogo sana ya umeme yasiyozidi unit 80 kwa mwezi.

Ni mahsusi kwa ajili ya watu wa vijijini wenye vipato vidogo.
 
Sisi tusiokuwa na tarrif mnatuumiza roho tu jamani. Imagine sh. 10,000 tunapata units 28.2
Ni kweli usemalo. Na natamani TANESCO waje hapa watoe ufafanuzi. Sisi wengine hatufikishi units 75 kwa mwezi lakini tunaambulia units 28.10 kwa Tshs. 10,000 kila tununuapo umeme. Ukiuliza kwa nini unaambiwa uandike barua kwa Meneja kwa Tanesco wa eneo lako kubadilishiwa Tarriff!

Binafsi nimefanya hivyo tangu mwaka jana lakini mpaka sasa sijabadilishiwa hiyo tarriff. Kwa nini wasibadilishe tarriff automatically bila urasimu na mlolongo huo mrefu hivyo maana mita zetu zinarekodi kamili wanaotumia chini ya units 75 na wa juu ya hapo!!?
 
Kwa kawaida, kwa wale wa matumizi ya chini, hawaruhusiwi kununua umeme wa 10,000/= kwa mwezi. Yaani toka tarehe 1 mpaka mwisho wa mwezi. Ukifanya hivyo, mwezi unaofuata, hizo unit zilizozidi kwenye zile unit 75,utazilipia kwa ongezeko la bei kubwa. Kwa hiyo, ukinunua umeme tena, watakata kwanza hicho kiasi, na fedha itakayobaki, utapewa umeme.

Nakushauri kama hizo unit 75 zinakutosha, basi usizidishe. Kwani ukiendelea hivyo, watakutoa, na kukuunganisha kwenye zile bei za juu.
Maanake sasa inabidi uwe na matumizi ya unit 2.5 kwa siku ili ufikie lengo la hyo 75 unit per month! duuh!
 
ku tembelea 2.5 kwa siku ngumu mno, 'friji' pekee linalamba 1 kwa siku, 'taa za nje 4' za kawaida nazo zinalamba karibia 1 usiku kucha , jombaa hapo umebaki na nusu units,
Na wakati matumizi ya kawaida tu ya kiwango cha chini kabisa yanafika unit 5
 
Kuna watu mnaishi bongo lakini mnapata charges za umeme kama mpo Dubai
 
Ni kweli usemalo. Na natamani TANESCO waje hapa watoe ufafanuzi. Sisi wengine hatufikishi units 75 kwa mwezi lakini tunaambulia units 28.10 kwa Tshs. 10,000 kila tununuapo umeme. Ukiuliza kwa nini unaambiwa uandike barua kwa Meneja kwa Tanesco wa eneo lako kubadilishiwa Tarriff!

Binafsi nimefanya hivyo tangu mwaka jana lakini mpaka sasa sijabadilishiwa hiyo tarriff. Kwa nini wasibadilishe tarriff automatically bila urasimu na mlolongo huo mrefu hivyo maana mita zetu zinarekodi kamili wanaotumia chini ya units 75 na wa juu ya hapo!!?
Baada ya kuandika barua unatakiwa kufuatilia mwenyewe ofisi zao tanesco, mie nilisumbuana nao hiyo siku mpaka nikawaambia narudi tena kwa meneja ikishindikana hadi kwa meneja wa mkoa, wakazie sana bila hivyo hawatakubadilishia
 
Mm 10000 ni unite 24 nyny mnatumia mita zipi mnapata unite nyingi kiasi iko
 
Back
Top Bottom