Gharama za umeme zimepanda lini? Tsh.10,000 kwa unit 72 badala ya 82 imekuwaje?

Gharama za umeme zimepanda lini? Tsh.10,000 kwa unit 72 badala ya 82 imekuwaje?

Kwa kawaida, kwa wale wa matumizi ya chini, hawaruhusiwi kununua umeme wa 10,000/= kwa mwezi. Yaani toka tarehe 1 mpaka mwisho wa mwezi. Ukifanya hivyo, mwezi unaofuata, hizo unit zilizozidi kwenye zile unit 75,utazilipia kwa ongezeko la bei kubwa. Kwa hiyo, ukinunua umeme tena, watakata kwanza hicho kiasi, na fedha itakayobaki, utapewa umeme.

Nakushauri kama hizo unit 75 zinakutosha, basi usizidishe. Kwani ukiendelea hivyo, watakutoa, na kukuunganisha kwenye zile bei za juu.
 
Huwa nafanya hivi baada ya kuona hiyo hasara huwa nalipa tsh 5000 napata unit 41 halafu nanua tena tsh 5000 napata unit 41 jumla napata unit 82 inakuwa afadhari kuliko unit 77 kwa tsh 10,000 kwa mkupuo.
Lakini mimi nikinunua hivyo ya kwanza napata units 41, nikinunua tena ya 5000 napata units 36!!!!
 
TANESCO kuna shida kabisa kwanza umeme unakatika katika hovyo sawa hiyo moja lakin nyingine naona ghafla gharama za umeme zimepanda kimya kimya maana kwa Tsh.10000/ tulipata unit 82 lakini sasa mwez huu Tsh.10000 unit unapata unit 72.

Hii ni hujuma au kuna nini huko TANESCO? Maana TANESCO ndiko kuna wizi mkubwa sana huko. Hii ni kwa wale wateja wa matumuz chini ya unit 75 tarif 0
Jamaa, ungekaa kimya tu, nyinyi mo nchi gani ?, mimi huku nilipo shs 10000 napata unit 28, sasa angalia usije haribu ulichonacho
 
Iyo elfu 10 kwa tariff 4 ama 0 mbona haiendani na hela iyo,nijuavyo mie ni kuwa Taiff 4 mwisho wa kununua ni elfu 9 na unapata unit 75,sasa izo 82 unapataje mwenzangu.
Nasikia kama umeme umeisha kabla ya mwezi, huwezi nunua umeme mpaka mwezi uishe....ndiyo hivyo?
 
TANESCO kuna shida kabisa kwanza umeme unakatika katika hovyo sawa hiyo moja lakin nyingine naona ghafla gharama za umeme zimepanda kimya kimya maana kwa Tsh.10000/ tulipata unit 82 lakini sasa mwez huu Tsh.10000 unit unapata unit 72.

Hii ni hujuma au kuna nini huko TANESCO? Maana TANESCO ndiko kuna wizi mkubwa sana huko. Hii ni kwa wale wateja wa matumuz chini ya unit 75 tarif 0
Duu ulikuwa unapata 82?
Mbona sisi tunapata units 28kWh kwa 10k
 
Jamaa, ungekaa kimya tu, nyinyi mo nchi gani ?, mimi huku nilipo shs 10000 napata unit 28, sasa angalia usije haribu ulichonacho
Hawezi kuharibu kwani ni utaratibu halali uliopo ndani ya Tanesco kwa mteja anayetimiza vigezo.
 
Back
Top Bottom