Gharama za usafiri Air Tanzania zinatisha

Wengi mnapenda kulalamika bila utafiti mbona bei ni kuanzia 340k View attachment 3021572
Hizo best offer zinatumika online kama chambo na huwa zinatangazwa kubakia nafasi mbili au tatu tu lakini ni sawa na majibu wanayotoa kuwa ndege imejaa wakati wakikulazimisha uchukue tiketi ya bei kubwa ambayo inacheza kwenye laki saba.
 
Hizo best offer zinatumika online kama chambo na huwa zinatangazwa kubakia nafasi mbili au tatu tu lakini ni sawa na majibu wanayotoa kuwa ndege imejaa wakati wakikulazimisha uchukue tiketi ya bei kubwa ambayo inacheza kwenye laki saba.
Sio chambo
Ukichagua unapata nafuu kweli
Ama ulitaka Business ticket?
 

Kwanza booking yenyewe umekosea, ndiomana kuna maagent. Unaemda dar ila hapo nikisoma ni mpanda dar na ndiomana nauli ipo juu hivo. Lkn pia kwa ushauri chukua dar mbi kata week 2 kabla ya safari nauli ni kitonga. Kama ukiweza nifate inbox nikuhudumie nahusika na hizo kaz mkuu, au weka namba ntakuchek. Ahsante.

Angalizo sina uhakika wa ndege za Tc kutua mpanda, huenda zatua maramoja moja ndiomana bei inakuw kubwa. Nyanda za juu ndege hutua mby tuu nnavojua.
 

Attachments

  • Screenshot_20240620_184754_Chrome.jpg
    311.1 KB · Views: 6
Labda pia ni kuporomoka kwa thamani ya sarafu ya tshs dhidi ya sarafu za kigeni mfano dola.
 
Wiki iliyopita nilikuwa Kigoma, Booking za Air Tanzania kutoka Kigoma Geita na Mwanza zilichezea kwenye kati ya 500K na 700K. Miaka yote nasafiri kwa 340K+ lakini mwaka huu nilipata tiketi ya 418K kutoka Mwanza hadi Dar tena saa saba usiku na kuwasili alfajiri ya leo.
Kwa mara nyingine tena nauona uchakavu wa ndege za Air Tanzania, upo bayana! Nimeona mapungufu mengi kwa watoa huduma ambao hawaonekani kutoa huduma kwa weredi zaidi ya kutimiza wajibu bora liende.

Hatma ya Air Tanzania iko mashakani na kwa hakika wanahitaji kuwa na mshindani kuliko kuhodhi route zote wao tu. Precision Air wapewe route zile zile za Air Tanzania ili kuwe na ushindani kuliko kulazimika kutumia Air Tanzania tu. Ningetamani kuona Fastjet wakirudi kwenye anga zetu tena kwani waliacha historia kwenye usafiri wa anga hapa Tanzania.
Najiuliza tu, wahudumu huwa hawabadilishwi baada ya safari moja kwenda nyingine? Nimeshuhudia uchovu kwenye nyuso zao na mbaya zaidi uniform zao hazikuwa safi na smart.....Au ni kwa kuwa safari ni za saa saba usiku? 😳
 
Sio chambo
Ukichagua unapata nafuu kweli
Ama ulitaka Business ticket?
Inawezekana tickets za economy zinaisha haraka na hivyo kulazimisha kuuza tickets za Business class. Hata hivyo bado kuna dosari kwenye mfumo wa ticketing wa Air Tanzania.
 
Kwanza ukikata ONE WAY ni gharama kuliko two way.

Pia, muda unaokata mfn imebaki siku moja au wiki moja ni gharama zaidi.

Class unayochukua pia...

Kingine flight time inachangia gharama.

Pia hiyo hela unayoona hapo bado sio yenyew ukiona imeleta 700k ujue kuna 50+k mbele..
Kodi
Siti
etc..

Ndege sio za hoehae, kama huna hela dandia SARATOGA ,SAIBABA, KIMBINYIKO etc.
 
Songea pia inatua.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…