Gharama za vifurushi vya intaneti zapandishwa tena kimya kimya. Je, ni censorship ya aina yake?

Gharama za vifurushi vya intaneti zapandishwa tena kimya kimya. Je, ni censorship ya aina yake?

Acha watumalize. Siku hizi mitandao ni sehemu ya maisha kwa kila mtu. Na wengine biashara zao zipo huko. Kuongeza gharama za vifurushi ni kutuua kabisa
 
Screenshot_20220119-093258.png
 
Wamegundua hatumalizi gb ndio maana wametupunguzia
Mtu ananunua gb 2 kwa siku tatu
Lakini siku tatu zikiisha ametumia 1.4 gb
So poa tu
 
Hata mimi hii size yako ndio ujanja wangu vinginevyo nisingetoboa [emoji23]
Tigo sasa hivi ndiyo pekee mpo kwenye hali nzuri yaani kw buku jero wkt voda Gb 1 kwa buku mbili ila nadhani watotoa soon ili wote tuimbe wimbo mmoja.
 
Hii wakiitoa line naitupa

Sent using Jamii Forums mobile app
Usitupe siku hizi ujanja ndio kuwa na line nyingine mbadala maana hawachelewi madaliko huku wakiminya unahamia upande wa pili kwenye auheni kwngine unapumzika na mimi hiyo ndiyo mbinu yng ila safari nimebanwa mbavu kote sina pakutokea naonea wivu wa watu wa tigo.
 
Ilikuwa ukipiga *148*05# unapata vifurushi vizuri vyenye unafuu ila kwasasa hali ni mbaya sijui nihamie wapi?

A9A0D14D-2D9C-4695-87DF-041CB8700A3C.jpeg
 

Ni mwendo ule ule, umafia wa kimya kimya, kwa Voda na Tigo wameanza kutesti mitambo kwa kkupunguza GB za vifurushi vya mwezi.

Kuanzia sasa tutegemee lolote, hii ni trailer tu, bado muvi kamili ya machinjo yatayofanyika kimya kimya gizani usiku wa manane, nadhani tunaweza kuamka asubuhi mabadiliko kadha na kadha yakiwa yamedanyika kwenye vifurushi vingine.

Mtandao gani huu mkuu? Bila shaka itakuwa vodacom maan hawa jamaa ni wapumbavu kuliko maelezo. Halaf hii mitandao wanatufanyia u senge wote huu lakini TCRA wamekaa kimya. Inasikitisha sana.
 
Nimevunja li line la zantel na kutupa huko... Yaani ninunue vocha kwa shida maana huku vijijini hakuna(nanunua kupitia tigopesa) alafu walivyo wajinga wanapandisha vifurushi kimya kimya)
 
Back
Top Bottom