Gharama za vifurushi zimepanda kwa asilimia 100

Gharama za vifurushi zimepanda kwa asilimia 100

Lycaon pictus

JF-Expert Member
Joined
Jan 31, 2021
Posts
9,189
Reaction score
16,128
Hili suala kwakweli limekuwa baya sana. Kadri siku zinavyosonga, maisha ya watu yanazidi kutegemea mtandao. Na kwa kawaida teknolojia inavyozidi kukua ndivyo bei inapozidi kushuka. Sasa inakuwaje hawa jamaa wanaongeza bei kwa asilimia 100.

Kwa Tsh 1000 nilikuwa napata GB 1 ya tigo. Sasa napata MB 500. Wanaongeza gharama mara mbili? Hili suala ni counterproductive kwa uchumi. Serikali imefika mwisho wa kufikiri na imeona njia pekee ya kupata pesa ni kodi! Haya, hizi zikifika sehemu hazitoshi mtaongeza kwenye nini tena? Maana haichukui muda hizi tozo zinakuwa hazitoshi. Mtapata wapi zingine na mmekwamisha watu biashara, mnajua ukubwa wa biashara zinazofanyika mitandaoni?

Hata wakoloni hawakuwa kama nyinyi, mnakamua bila kulisha.
 
Mkuu usiwe na shaka, hizi kampuni zitapigwa doro mpaka watakua wanapita barabarani na kutangaza gb 100 kwa elfu 2 mwezi mzima, starlink ya Elon Musk tayari imefika Nigeria sisi huku ni next year hapo mambo yanajipa speed wanasema ni 150Mbps ikishuka ni 50Mbps.

Ushenzi wanaoufanya wanafikiri dunia inawasubiri, watu wanakwenda mwezini sisi bado tunapambania bundle.

$99 mwezi mzima unlimited ni very cheap tusisahau pia mchina mkombozi wetu atakuwa hayupo nyuma kuja na suluhisho la upatikanaji rahisi na nafuu wa mtandao.
 
Mkuu usiwe na shaka, hizi kampuni zitapigwa doro mpaka watakua wanapita barabarani na kutangaza gb 100 kwa elfu 2 mwezi mzima, starlink ya Elon Musk tayari imefika Nigeria sisi huku ni next year hapo mambo yanajipa speed wanasema ni 150Mbps ikishuka ni 50Mbps..
Wakati tajiri namba moja Africa Dangote anaingia Mtwara tuliambiwa simenti itauzwa elfu saba nchi nzima... Mkuu zilongwa mbali, zitendwa mbaliii.
 
2845551_IMG-20210716-WA0007.jpg
Huyu ndio mchumi anayemshauri Chief Hangaya
 
wanaweza kupigwa vikwazo kutoa huduma mkuu ili tu tuteseke
na mie nina wasi wasi huo lakini, mitandao yetu ni kama demand ya mtandao imekuwa kubwa mnooo, yaani huduma za unlimited sasa hakuna kabisa, hata wale wazee wa usiku unlimited wamepotea.

Lakini kama satellite zingine zinafanya kazi Africa wakizuia itakuwa sio fair, mpaka sasa kuna kampuni za satellite internet zinaoperate kama kawaida, hii ikija mimi nitanunua , uzuri mnaweza share na watu wakakusaidia kulipia fee/month...
 
Hili suala kwakweli limekuwa baya sana. Kadri siku zinavyosonga, maisha ya watu yanazidi kutegemea mtandao. Na kwa kawaida teknolojia inavyozidi kukua ndivyo bei inapozidi kushuka...
Amia Halotel au TTCl
 
Mkuu usiwe na shaka, hizi kampuni zitapigwa doro mpaka watakua wanapita barabarani na kutangaza gb 100 kwa elfu 2 mwezi mzima, starlink ya Elon Musk tayari imefika Nigeria sisi huku ni next year hapo mambo yanajipa speed wanasema ni 150Mbps ikishuka ni 50Mbps..
Hiyo nayo wanaweza kuiwekea bei kubwa ikawa vilevile. Hawa watu hawataki kuendelea. Wanachoangalia ni kama kodi ya kuwafanya waendelee kutawala ipo.

Watu walipohamia kupiga simu nje kwa whattsap badala ya simu wakaanza kulalamika kodi imepungua. Badala ya kuangalia jinsi whatsap ilivyorahisiha mambo, wao wanawaza kukwamisha ili wapate kodi, pathetic luddists☹️
 
Hili suala kwakweli limekuwa baya sana. Kadri siku zinavyosonga, maisha ya watu yanazidi kutegemea mtandao. Na kwa kawaida teknolojia inavyozidi kukua ndivyo bei inapozidi kushuka. Sasa inakuwaje hawa jamaa wanaongeza bei kwa asilimia 100...
Serikali zote duniani zinajiendesha kwa kulipa kodi. Tulipe kodi kwa maendeleo ya nchi.
 
Hili suala kwakweli limekuwa baya sana. Kadri siku zinavyosonga, maisha ya watu yanazidi kutegemea mtandao. Na kwa kawaida teknolojia inavyozidi kukua ndivyo bei inapozidi kushuka. Sasa inakuwaje hawa jamaa wanaongeza bei kwa asilimia 100...
Tunyweni bia jamani
 
Iko shida kubwa mbele.maana hali ni ngumu kila eneo.ata hatuelewi uelekeo ni upi.
 
Back
Top Bottom