Silaha za kivita Afrika na hapa Tanzania tunatumia ndege jeshi za China mzee..., nenda kachukue boda ni Chinese, ukiwasha simu yako kama sio Tecno,Infinix, Huawei,Xiaomi useme ni iphone bado ni assembled in China mzee..., panda gari kwenda mikoani, barabara ya kila siku unayokwenda kazini ni Chinese hao, Radio unayosikiliza hapo ni Chinese, ukija kwenye nguo hizi brand kama african boy, viatu, mitumba ni Chinese mzee, hiko kikombe cha udongo hebu fanya kukiangalia kwa chini uone made in where ni Chinese huyoo...,
Tuacheni majivuno ambayo hayana tija, mnadanganywa ni utumwa wakati ukweli ndio huo, mchina katufungulia dunia afrika, Kariakoo pale bidhaa 90% ni Chinese mzee baba, huyo ndio anafanya maduka yamesheheni bidhaa...
Uwanja wa Taifa, Malls nyingi hapa nchini, majengo mbali mbali ... ni Chinese yaani kila nikisema kitu malizia "Chinese"
Mnajifaragua wakati hamna lolote, siasa kwenye kila kitu, kuna jamaa mmoja humu alisema Mwafrika ni kima aliyechangamka[emoji1787][emoji1787][emoji1787], najua watu inawatia hasira mpaka wanafikia hatua ya kujitusi sababu ya watu wachache hasa viongozi ambao wanawaza kutumia sijui nini..