Ghorofa refu Tanzania litakuwa hili la TRA DSM, nembo ya jiji

Ghorofa refu Tanzania litakuwa hili la TRA DSM, nembo ya jiji

Yasije yakabaki tupu bila wateja

Nchi inazidi kufunguka wafanyabiashara toka Zambia, Zimbabwe, DR Congo n.k wameongeza imani kuhusu ufanisi unaozidi kuimarika ktk bandari, TRA, barabara na reli bila kusahau malazi ktk hoteli wakiwepo jijini Dar es Salaam

Mdau kutokana nchini Zambia anaelezea utaratibu mzima wa kupata mzigo kupitia wakala n.k unaotakiwa Tanzania na sababu za,wengi kuikubali Dar es Salaam

View: https://m.youtube.com/watch?v=tvax18sBdQU
 
maghorofa marefu ni satanic, ukiona nchi inajenga majengo marefu ujue ni satanic …
 
Ni vizuri Kupendezesha mji! Ila hakuna faida yeyote ni kama la TPA floor karibia zote hazina wapangaji!
TCRA na wao ni yale yale!
Ni mradi usio na maaana kwa kuwa walipa kodi hauwasaidii kwa chochote!
Ni kama walosema wanaivunja Muhimbili yote ijengwe upya badala ya kuikarabati
 
Muonekano wa jiji letu Dar es Salaam City 2023
Inapokuja kwenye magorofa, 'I am for them' hata nikiwa natambua kule kijijini kuna watu wanakunywa tope.

Dar es Salaam inapendeza sana na hayo ma-minara yaliyopo. Ila yule aliye chora yale ya Benki Kubwa, anastahili kunyongwa hadi kufa.
Eneo lile zuri kabisa kaliwekea uchafu usiofaa kuwa hapo.
 
Huo mradi waachane nao. Ni kuchezea hela. Hayo mabilioni. Sio bora wangenunua hata mtambo wa kuzalisha umeme wa gesi asilia hata Megawatt 100 au Megawatt 200(toka Japan, Korea au Siemens),
Au wangewekeza kwenye usambazaji wa maji.
Au wangewekeza kwenye kununua kupima viwanja na kupanga miji ili watu wapate hati na kumaliza migogoro ya ardhi.
Kwanza maghorofa mengi yapo Tupu. Serikali si imehamia Dodoma?

Uwezo mdogo wa kufikiria ndio chanzo za matatizo.
Wenzako hapo wanawaza kupiga mabilioni ya rushwa wala hawana muda na maslahi ya wananchi
 
Msanifu wa majengo Arch. Yassin Mringo kutoka kampuni ya Y&P Architect aeleza kwa undani kuhusu jengo tarajiwa.

Kampuni ya Y&P Architects (T) Ltd ni ya kitanzania na inaongozwa wa wakurugenzi wawili watanzania.

Muonekano wa jiji la Dar es Salaam unazidi kuwa wa kisasa katika ukanda huu wa Afrika ya Mashariki na barani Afrika kwa ujumla.

Uwezo wake katika wilaya ya Ilala jirani na bandari utasaidia kuwa kituo cha huduma chini ya paa moja One Stop Centre kutoa huduma kwa wateja wa ndani na nje ya nchi kutokana na Dar es Salaam kuwa eneo la kimkakati (geostrategic position) ukanda huu wa Afrika ililoona hata na wafanyabishara wa karne iliyopita chini ya Sultan wa Zanzibar, utawala wa kikoloni wa Ujerumani, utawala wa kikoloni na Waingereza na utawala wa nchi huru ya Tanzania.

Muonekano wa jiji letu Dar es Salaam City 2023

Kulikuwa na haja gani ya kujenga hilo jengo Dar? Wakati makao makuu ni Dom? Na je kulikuwa na ulazima wa kujenga jengo refu na kubwa namna hiyo na kazi gani?
 
Msanifu wa majengo Arch. Yassin Mringo kutoka kampuni ya Y&P Architect aeleza kwa undani kuhusu jengo tarajiwa.

Kampuni ya Y&P Architects (T) Ltd ni ya kitanzania na inaongozwa wa wakurugenzi wawili watanzania.

Muonekano wa jiji la Dar es Salaam unazidi kuwa wa kisasa katika ukanda huu wa Afrika ya Mashariki na barani Afrika kwa ujumla.

Uwezo wake katika wilaya ya Ilala jirani na bandari utasaidia kuwa kituo cha huduma chini ya paa moja One Stop Centre kutoa huduma kwa wateja wa ndani na nje ya nchi kutokana na Dar es Salaam kuwa eneo la kimkakati (geostrategic position) ukanda huu wa Afrika ililoona hata na wafanyabishara wa karne iliyopita chini ya Sultan wa Zanzibar, utawala wa kikoloni wa Ujerumani, utawala wa kikoloni na Waingereza na utawala wa nchi huru ya Tanzania.

Muonekano wa jiji letu Dar es Salaam City 2023

Majengo yote mnajenga posta. Na parking ya kutosha ipo?
 
Dodoma hakuna biashara, jiji la Dar es Salaam ndiyo roho ya nchi ya Tanzania kimapato, bandari na eneo mkakati.

Dodoma kuwa makao ya bunge na mawizara inatosha.

Mambo mengine yote jiji kubwa kabisa la kibiashara ni Dar es Salaam na juhudi zifanyike za makusudi kabisa kuliimarisha kwa ajili sababu za kiuchumi, kibiashara na ni lango la nchi 7 ukanda huu :

JIJI LETU JIPYA LA DAR ES SALAAM ILALA
Labda sasa Kariakoo ndani ya jiji jipya itakuwa kama Dubai biashara masaa 24 , mwanga wa kutosha usiku wote lazima biashara zilizokufa Kariakoo ambazo wafanyabiashara kutoka Zimbabwe, Congo, Malawi , Zambia , Comoro n.k warudi na wasiwaze kwenda China wala Dubai kufuata mzigo.

Na machinga wote watasombwa kubwagwa Kinondoni, Ubungo, Temeke na Kigamboni.

Jiji la Dar es Salaam "mpya" litaambaa na barabara ya Nyerere kuchukua ukanda wa Tazara Stesheni DSM, viwanda vote Ukanda wa "Pugu Road " hadi Airport ya Uwanja wa Kimataifa wa JNIA. Jiji hili jipya litaamba Kurasini mivinjeni mpaka bandari zote kavu na bandari yenyewe. Maeneo ya Mjini Kati Posta, Gerezani, Mnazi Mmoja , Upanga, Magomeni hadi Ukanda wa Morogoro road Ubungo Maji mpaka Stendi Mpya Mbezi Louis.

Bila kusahau maeneo ya Oysterbay , Masaki hadi Mawasiliano 2000 stendi yatakuwa ndani ya Jiji jipya la Dar es Salaam lenye miundo-mbinu ya flyover, madaraja , BRT mwendokasi, superfast internet, bila uchafu wa meza za wamachinga, bidhaa kupangwa barabarani sehemu za wenda-kwa-miguu.

Hii itasaidia Jiji jipya la Dar es Salaam kukusanya kodi kwa kusaidiana na TRA kwa ufanisi huku miundo-mbinu ikibaki wazi na safi kwa wenye shughuli zenye TIN Number TRA na Dar es Salaam jiji jipya kuwa ULAYA ndani ya Africa.

Hawa wamachinga "wametuchelewesha" sana Dar es Salaam yenye miundombinu na magorofa makubwa kuchangia kodi, kwani biashara zimekufa na wameharibu muonekano wa jiji kisa wamechangia Tshs. 20,000 kitambulusho cha mfanyabiashara mdogo wakati wanaharibu mazingira ya biashara kubwa, biashara za kimataifa na hata watu wanakimbiza ofisi zao toka mjini kati kuzipeleka maeneo ya Victoria, Makumbusho ili kuondokana na hawa "wakuja" machinga wasioelewa maana ya jiji.

Watendaji nao wa serikali madiwani, mameya, waDC , Mkuu wa Mkoa bila kusahau viongozi wa CCM ngazi zote Dar es Salaam nao wamekuwa waoga na kukosa ubunifu kulifanya jiji kuwa Dubai au Singapore ya Afrika huku serikali imewekeza matrilioni ya fedha kuinua hadhi ya mji wa Dar es Salaam uwe wa kisasa kufuatana na uwekezaji mkubwa wa Maendeleo ya Vitu uliowekwa jijini Dsm.
 
Msanifu wa majengo Arch. Yassin Mringo kutoka kampuni ya Y&P Architect aeleza kwa undani kuhusu jengo tarajiwa.

Kampuni ya Y&P Architects (T) Ltd ni ya kitanzania na inaongozwa wa wakurugenzi wawili watanzania.

Muonekano wa jiji la Dar es Salaam unazidi kuwa wa kisasa katika ukanda huu wa Afrika ya Mashariki na barani Afrika kwa ujumla.

Uwezo wake katika wilaya ya Ilala jirani na bandari utasaidia kuwa kituo cha huduma chini ya paa moja One Stop Centre kutoa huduma kwa wateja wa ndani na nje ya nchi kutokana na Dar es Salaam kuwa eneo la kimkakati (geostrategic position) ukanda huu wa Afrika ililoona hata na wafanyabishara wa karne iliyopita chini ya Sultan wa Zanzibar, utawala wa kikoloni wa Ujerumani, utawala wa kikoloni na Waingereza na utawala wa nchi huru ya Tanzania.

Muonekano wa jiji letu Dar es Salaam City 2023

Mnakazana kujenga majengo marefu Dar Es Salaam wakati makao makuu ya nchi ni Dodoma na TRA inatakiwa iwe Dodoma sijui kwanini kuna akili mbovu kama hizi.

Kwa hiyo TRA wanajivunia kufanya ubadhirifu wa fedha za walipa kodi kwa kuweka jengo la kifahari kiwango hicho kwa manufaa gani kwa wananchi wa kawaida?

Huu ni uhujumu uchumi na pindi utawala uliopo ukiondxoka watakaohusika watakuja kufunguliwa mashitaka mpaka ndimi zitawatepeta.
 
KITUO CHA HUDUMA YA PAMOJA / ONE STOP CENTRE- JENGO REFU
1700927954613.png

Katika jengo la refu la TRA inaweza kunufaisha yafuatayo

Ni sehemu itakayotengwa na kwa ajili ya mwekezaji, msafirishaji, mgavi n.k kupata vibali, leseni, taarifa n.k kwa kutumia maofisa wa kutoka mamlaka mbalimbali za serikali wanaohusika na utoaji wa vibali, leseni, vibali n.k. Maafisa wa kituo cha pamoja mjengoni TRA ni maafisa kutoka mamlaka za serikali ambao wamewekwa na kutekeleza majukumu yao kutoka mamlaka na ofisi mbalimbali za serikali . Huduma zifuatazo zinawepatikana katika jengo moja :

  • Huduma za uhamiaji
  • Huduma za KaziMamlaka ya Mapato Tanzania (TRA)
  • Huduma za Wizara ya Ardhi na Makazi
  • Shirika la Viwango Tanzania (TBS)
  • Mamlaka ya Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA)
  • Baraza la Taifa la Usimamizi wa Mazingira (NEMC)
  • Mamlaka ya Kikazi, Usalama na Afya (OSHA)
  • Mamlaka ya Chakula na Dawa Tanzania (TFDA)
  • Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA)
Badala ya kukimbizana katika maeneo tofauti ndani ya jiji la Dar es Salaam au kusafiri kati ya Dodoma na Dar es Salaam, kuokoa muda, gharama n.k ambavyo vitaifanya lango la ukanda wa eneo mkakati la Dar es Salaam kushinda washindani wa nchi zingine ktk biashara za kimataifa kupitia bandari
(Imehaririwa kuweza kutoa picha pana)

What are One Stop Facilitation Centre and its benefit to the investors?

Answer:
It is a place designated by TIC for an investor to obtain permits, approvals, license, information, etc. using TIC stationed officers from various government authorities dealing with the issuance of permits, license, approvals etc. Stationed officers are officers from government authorities who are placed at TIC and perform their duties from TIC. The following services are currently available;

  • Immigration services
  • Labour Services
  • Tanzania Revenue Authority (TRA)
  • Ministry of Lands and Human Settlements services
  • Tanzania Bureau of Standards (TBS)
  • Business Registration and Licensing Authority (BRELA)
  • National Environment Management Council (NEMC)
  • Occupational, Safety and Health Authority (OSHA)
  • Tanzania Food and Drugs Authority (TFDA)
  • National Identification Authority (NIDA)
Source : TIC | What are One Stop Facilitation Centre and its benefit to the investors?
 
Back
Top Bottom