Ghorofa refu Tanzania litakuwa hili la TRA DSM, nembo ya jiji

Ghorofa refu Tanzania litakuwa hili la TRA DSM, nembo ya jiji

Ni vizuri Kupendezesha mji! Ila hakuna faida yeyote ni kama la TPA floor karibia zote hazina wapangaji!
TCRA na wao ni yale yale!
Ni mradi usio na maaana kwa kuwa walipa kodi hauwasaidii kwa chochote!
Ni ujinga wa Viongozi wa Tanzania tu.

Majengo mengi Dar es Salaam wameyaacha hayana kazi wakati yapo vizuri alafu wanatumia mapesa mengi kujenga Dodoma bila kutumia akili kabisa.

Kiuhalisia Dodoma ilitakiwa iwe sehemu ya Wizara tu. Taasisi nyingine zingebaki tu Dar es Salaam.
 
Dodoma hakuna biashara, jiji la Dar es Salaam ndiyo roho ya nchi ya Tanzania kimapato, bandari na eneo mkakati.

Dodoma kuwa makao ya bunge na mawizara inatosha.

Mambo mengine yote jiji kubwa kabisa la kibiashara ni Dar es Salaam na juhudi zifanyike za makusudi kabisa kuliimarisha kwa ajili sababu za kiuchumi, kibiashara na ni lango la nchi 7 ukanda huu :

JIJI LETU JIPYA LA DAR ES SALAAM ILALA
Labda sasa Kariakoo ndani ya jiji jipya itakuwa kama Dubai biashara masaa 24 , mwanga wa kutosha usiku wote lazima biashara zilizokufa Kariakoo ambazo wafanyabiashara kutoka Zimbabwe, Congo, Malawi , Zambia , Comoro n.k warudi na wasiwaze kwenda China wala Dubai kufuata mzigo.

Na machinga wote watasombwa kubwagwa Kinondoni, Ubungo, Temeke na Kigamboni.

Jiji la Dar es Salaam "mpya" litaambaa na barabara ya Nyerere kuchukua ukanda wa Tazara Stesheni DSM, viwanda vote Ukanda wa "Pugu Road " hadi Airport ya Uwanja wa Kimataifa wa JNIA. Jiji hili jipya litaamba Kurasini mivinjeni mpaka bandari zote kavu na bandari yenyewe. Maeneo ya Mjini Kati Posta, Gerezani, Mnazi Mmoja , Upanga, Magomeni hadi Ukanda wa Morogoro road Ubungo Maji mpaka Stendi Mpya Mbezi Louis.

Bila kusahau maeneo ya Oysterbay , Masaki hadi Mawasiliano 2000 stendi yatakuwa ndani ya Jiji jipya la Dar es Salaam lenye miundo-mbinu ya flyover, madaraja , BRT mwendokasi, superfast internet, bila uchafu wa meza za wamachinga, bidhaa kupangwa barabarani sehemu za wenda-kwa-miguu.

Hii itasaidia Jiji jipya la Dar es Salaam kukusanya kodi kwa kusaidiana na TRA kwa ufanisi huku miundo-mbinu ikibaki wazi na safi kwa wenye shughuli zenye TIN Number TRA na Dar es Salaam jiji jipya kuwa ULAYA ndani ya Africa.

Hawa wamachinga "wametuchelewesha" sana Dar es Salaam yenye miundombinu na magorofa makubwa kuchangia kodi, kwani biashara zimekufa na wameharibu muonekano wa jiji kisa wamechangia Tshs. 20,000 kitambulusho cha mfanyabiashara mdogo wakati wanaharibu mazingira ya biashara kubwa, biashara za kimataifa na hata watu wanakimbiza ofisi zao toka mjini kati kuzipeleka maeneo ya Victoria, Makumbusho ili kuondokana na hawa "wakuja" machinga wasioelewa maana ya jiji.

Watendaji nao wa serikali madiwani, mameya, waDC , Mkuu wa Mkoa bila kusahau viongozi wa CCM ngazi zote Dar es Salaam nao wamekuwa waoga na kukosa ubunifu kulifanya jiji kuwa Dubai au Singapore ya Afrika huku serikali imewekeza matrilioni ya fedha kuinua hadhi ya mji wa Dar es Salaam uwe wa kisasa kufuatana na uwekezaji mkubwa wa Maendeleo ya Vitu uliowekwa jijini Dsm.

Kwa maana hiyo, tuamishe vizara ya kilimo tuopeleke nyanda za juu kusini?
Kwani hizo taasisi zilizoamishia makao makuu yao Dodoma ndipo kunakopatikana wateja wao wakuu?
 
Mkandarasi mwenyewe mzawa au ni dalali tu wa wachina?
 
Hama nchi ,kenge mkubwa kabisa ,unatia aibu
Uwe na tabia ya kujenga hoja, kuna kiongozi pale TPA aliamishiwa bandari ya Tanga kisa yeye alikuwa anapinga ujenzi wa jengo lile la TPA lakini akawa anashauri fedha hizo zitumike kupanua gati na kuboresha mitambo hapo Bandarini...wakaona anataka kuwabania chakula.
Hakuna haja ya ligorofa likubwa kujengwa hapo Dar kwa ajili ya TRA wakati akija kiongozi mwingine wa kisiasa atawakoromea then wanaamia Dodoma.
 
Uwe na tabia ya kujenga hoja, kuna kiongozi pale TPA aliamishiwa bandari ya Tanga kisa yeye alikuwa anapinga ujenzi wa jengo lile la TPA lakini akawa anashauri fedha hizo zitumike kupanua gati na kuboresha mitambo hapo Bandarini...wakaona anataka kuwabania chakula.
Hakuna haja ya ligorofa likubwa kujengwa hapo Dar kwa ajili ya TRA wakati akija kiongozi mwingine wa kisiasa atawakoromea then wanaamia Dodoma.
Hakuna haja kwa taasisi kuhamia Dodoma? What is the logic behind Taasisi kuhamia Dodoma? Tunaongezewa nini kwa Taasisi kuhamia Dodoma?

Kuna shida gani Mawaziri na Wizara tu ndo wakawa Dodoma?
 
Ni vizuri Kupendezesha mji! Ila hakuna faida yeyote ni kama la TPA floor karibia zote hazina wapangaji!
TCRA na wao ni yale yale!
Ni mradi usio na maaana kwa kuwa walipa kodi hauwasaidii kwa chochote!
Kuna maghorofa wameyaacha yanakua magofu ilhali watanzania wangeweza kupanga na yaingize kodi. Wangeweka rates za kawaida, sasa hayo majengo ya TPA kodi yake haigusiki.

Hebu angalia jengo lililokua la ofisi za wizara ya katiba na sheria Dar, linapauka tu.
Dkt. Gwajima D liangalie hili, wapeni hata NHC walipangishe. Vijana tutaweza kupata ofisi humo tukachangia kodi serikali.
 
Kuna umuhimu gani wa kila Taasisi kuhamia Dodoma? Tunaongezewa nini?

Kweli kabisa. Inatakiwa kuhojiwa mantiki ya kiongozi kuhodhi madaraka kupitia dhana kuwa kila kitu kihamie Dodoma, viongozi wa CCM wadhibitiwe uroho wao kuwa na power kama miungu-watu.

Mfano :
Utasikia Bodi ya Korosho Tanzania nayo ina hamishiwa Dodoma toka Mtwara, makao makuu ya Mamlaka ya Bandari Tanzania THA inahama toka DSM kwenda Dodoma n.k n.k

Mji wa Arusha uwe makao makuu ya mhimili wa Mahakama Kuu ili jaji mkuu na mahakama ya rufani wabaki huko mbali siyo kila siku wanahudhuria hafla za wafanyakazi wa serikali kuu na mikoa wakiapishwa na kwa namna hii ya mgawanyo wa mihimili, Mahakama iwe huru toka minyororo na jinamizi lililoundwa ktk awamu ya tano. Arusha ni makao ya korti ya Afrika Arusha | Search Results | African Court on Human and Peoples' Rights , EACJ www.eacj.org , UN Korti za masuala ya maovu dhidi ya binadamu International Residual Mechanism for Criminal Tribunals May Conclude Most Cases by May 2021, Its President Tells Security Council | Meetings Coverage and Press Releases hivyo Mahakama Kuu ya Tanzania na Jaji Mkuu wa Tanzania Judiciary of Tanzania | Home watakuwa wanabadilisha mawazo na wasomi wenziwe kuhusu namna bora ya Mahakama za Tanzania kujiendesha kwa uhuru na kumaliza mrundikano wa kesi kwa kuwa kila siku wanahudhuria hafla zote za mhimili wa serikali .

The Many Capitals of South Africa
South Africa's three capital cities are strategically placed throughout the country, each hosting a separate segment of the nation's government. When asked about a single capital, most people would point to Pretoria.
  • Pretoria is the administrative capital. It is home to the executive branch of the South African government, including the President of the Cabinet. The city also hosts many departments of government and foreign embassies.
  • Located in the province of Gauteng, Pretoria is in the northeast part of South Africa and near the city of Johannesburg.
  • Cape Town is the legislative capital. It is home to the country's legislative parliament, including the National Assembly and National Council of Provinces.
  • Located in the southwest corner of South Africa in the province of Western Cape, Cape Town is the second-largest city in population.
  • Bloemfontein is considered the judicial capital. It is home to the Supreme Court of Appeal, the second-highest court in South Africa. The Constitutional Court (the highest court) is located in Johannesburg.
  • Located in the province of Free State, Bloemfontein is in the center of South Africa.
 
Msanifu wa majengo Arch. Yassin Mringo kutoka kampuni ya Y&P Architect aeleza kwa undani kuhusu jengo tarajiwa.



Kampuni ya Y&P Architects (T) Ltd ni ya kitanzania na inaongozwa wa wakurugenzi wawili watanzania.

Muonekano wa jiji la Dar es Salaam unazidi kuwa wa kisasa katika ukanda huu wa Afrika ya Mashariki na barani Afrika kwa ujumla.

Uwezo wake katika wilaya ya Ilala jirani na bandari utasaidia kuwa kituo cha huduma chini ya paa moja One Stop Centre kutoa huduma kwa wateja wa ndani na nje ya nchi kutokana na Dar es Salaam kuwa eneo la kimkakati (geostrategic position) ukanda huu wa Afrika ililoona hata na wafanyabishara wa karne iliyopita chini ya Sultan wa Zanzibar, utawala wa kikoloni wa Ujerumani, utawala wa kikoloni na Waingereza na utawala wa nchi huru ya Tanzania.

Muonekano wa jiji letu Dar es Salaam City 2023


Serikali ni sikio la kufa bado wanaednele kuwekeaza dar .badala ya dodoma
 
Hizo fedha.zikatumike kuboresha hospitali za mikoa na wilaya nyingi ni chafu sana hazina madawa wala.vifaa.
 
Inapokuja kwenye magorofa, 'I am for them' hata nikiwa natambua kule kijijini kuna watu wanakunywa tope.

Dar es Salaam inapendeza sana na hayo ma-minara yaliyopo. Ila yule aliye chora yale ya Benki Kubwa, anastahili kunyongwa hadi kufa.
Eneo lile zuri kabisa kaliwekea uchafu usiofaa kuwa hapo.
Mkuu kama sikosei kuna mtu/watu alituhumiwa juu ya ujenzi wa hiyo BOT
Mkandarasi mwenyewe mzawa au ni dalali tu wa wachina?
Vipi Mkuu - hautuamini Watanzania?
 
Huo mradi waachane nao. Ni kuchezea hela. Hayo mabilioni. Sio bora wangenunua hata mtambo wa kuzalisha umeme wa gesi asilia hata Megawatt 100 au Megawatt 200(toka Japan, Korea au Siemens),
Au wangewekeza kwenye usambazaji wa maji.
Au wangewekeza kwenye kununua kupima viwanja na kupanga miji ili watu wapate hati na kumaliza migogoro ya ardhi.
Kwanza maghorofa mengi yapo Tupu. Serikali si imehamia Dodoma?

Uwezo mdogo wa kufikiria ndio chanzo za matatizo.
Mkuu, nadhani wangejenga kiwanda ama viwanda vya nguo, ili tuachane na hii MITUMBA iliyozagaa mitaani na kuchafua mandari za jiji letu na hivyo kutoa ajira zenye ujira wa uhakika.
 
UGUMU WA MAISHA..MBILINGE ZA UKUSANYAJI KODI -MATUMIZI MAZURI YA MAKUSANYO
 
Ni vizuri Kupendezesha mji! Ila hakuna faida yeyote ni kama la TPA floor karibia zote hazina wapangaji!
TCRA na wao ni yale yale!
Ni mradi usio na maaana kwa kuwa walipa kodi hauwasaidii kwa chochote!
Hasara kubwa sana
 
Back
Top Bottom