Ghorofa refu Tanzania litakuwa hili la TRA DSM, nembo ya jiji

Ghorofa refu Tanzania litakuwa hili la TRA DSM, nembo ya jiji

Nashindwa kuuelewa huu uzi, kwan mpaka 2023 hilo jengo lilikuwa bado halijajengwa?
 
Msanifu wa majengo Arch. Yassin Mringo kutoka kampuni ya Y&P Architect aeleza kwa undani kuhusu jengo tarajiwa.



Kampuni ya Y&P Architects (T) Ltd ni ya kitanzania na inaongozwa wa wakurugenzi wawili watanzania.

Muonekano wa jiji la Dar es Salaam unazidi kuwa wa kisasa katika ukanda huu wa Afrika ya Mashariki na barani Afrika kwa ujumla.

Uwezo wake katika wilaya ya Ilala jirani na bandari utasaidia kuwa kituo cha huduma chini ya paa moja One Stop Centre kutoa huduma kwa wateja wa ndani na nje ya nchi kutokana na Dar es Salaam kuwa eneo la kimkakati (geostrategic position) ukanda huu wa Afrika ililoona hata na wafanyabishara wa karne iliyopita chini ya Sultan wa Zanzibar, utawala wa kikoloni wa Ujerumani, utawala wa kikoloni na Waingereza na utawala wa nchi huru ya Tanzania.

Muonekano wa jiji letu Dar es Salaam City 2023


Haya majengo yapo tangu 2014-2016 halafu unaleta uzi mwaka 2023 kana kwamba ndio jengo limejengwa kuna akili kweli au ulitaka kumpamba nani hasa mpaka mwaka huu Juni 2024?
 
Back
Top Bottom