Gigy Money kafanya nini huko kwenye ziara ya Tumewasha na Tigo?

Mnaonaje tukimtafuta aliemuuzia iyo nguo nae ale bun au vipi...
 
Je unaweza ruhusu mtu kuja kulia kitimoto ndani ya nyumba yako kwakuwa yeye anakila? Najua huwez bas hiki ndicho nakimaanisha inatakiwa TCRA na BASATA kupiga marufuku nyimbo na videos zote za nje na ndani zenye mahudhui ya ngono au zisizona maadir kuchezwa kwenye local media, sio waangalie upande mmoja tu
 
Mnaonaje tukimtafuta aliemuuzia iyo nguo nae ale bun au vipi...
Nafikiri tufanye msako wa nyumba kwa nyumba usiku, tutakayemkuta amevaa kama hiyo naye atulipe faini ya 1mil
 
Mkuu unatia aibu sana, yani miiko ya kitanzania juu ya mavazi hivi kuna kabila linavaa kama alivyovyaa gigy money? Ficha aibu yako usijibu vitu vinavyokuonyesha hujatumia akili
 
Nimeangalia vazi la Gigy kwa mbele na kwa nyuma. Hapina staha ya kufumbiwa macho. Anastahili adhabu Kali Sana kuliko aliyopewa
 
Nimeangalia vazi la Gigy kwa mbele na kwa nyuma. Hapina staha ya kufumbiwa macho. Anastahili adhabu Kali Sana kuliko aliyopewa
Tulia mzeee...!! Mbona vazi poa tuu[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Mkuu unatia aibu sana, yani miiko ya kitanzania juu ya mavazi hivi kuna kabila linavaa kama alivyovyaa gigy money? Ficha aibu yako usijibu vitu vinavyokuonyesha hujatumia akili

Sawa kaka mimi "Akili sina" na ninakuunga mkono kwa asilimia 100%.
Ila sababu ni kuwa ukisema nina akili wakati sina au sina wakati ninazo haitobadili uhalisia wangu hata kwa 0.00000000001%.
 
Sawa kaka mimi "Akili sina" na ninakuunga mkono kwa asilimia 100%.
Ila sababu ni kuwa ukisema nina akili wakati sina au sina wakati ninazo haitobadili uhalisia wangu hata kwa 0.00000000001%.
Sorry usichukulie seriously hilo neno sio kwamba nimuku underrate ndugu, samehe saba mara sabini
 
Kwenye kampeni Diamond mwenyewe aliimba lichupi mbele ya meza kuu akiwamo Rais,

It was very embarrassing.

Maadili hakuna tena.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…