Gigy Money na Jackline Wolper wahamia kwa Nabii Malisa

Gigy Money na Jackline Wolper wahamia kwa Nabii Malisa

niite nyeto mechanics eng.
hao mech wengine wako Tabata
1691700682411.jpg

Wana Tabata wanaumia.
 
Wanawake wengi ni rahisi sana kushawishika, ndivyo walivyoumbwa, hata nyoka alipitia kwa Eva ili kumhadaa Adam..
 
Usisahau kuwa walawi sio wabongo wala waniga, so hizo sheria za kilawi haziwahusu
Ni kweli ila usisahau biblia ni kazi ya fasihi. Kwa sasa watu wote wanaokaa madhabahuni wamechukua nafasi ya walawi japo sheria haijawahi badilika so na wao wanabanwa na kanuni hizo hizo.

Tukikaa kwenye dhana yako ni sawa na tuseme Biblia haimhusu kabisa mtu mwengine yeyote.tofauti na Myahudi. Jambo ambalo kuna.wakati ni kweli pia, tumeforce sana ituhusu.
 
Kila mmoja kachukua uamuzi wa kuungana na nabii kwa sababu zake.

1. Tuanze na sababu za Gigy money [emoji116][emoji116][emoji116][emoji116]

"Nilipagawa na Nabii ndio maana nimekuja Kanisani"- Gigy Money

"Mimi nimeanguka sana japo siwezi kusema nilianguka wapi, na pia naweza kusema siyo kila Nabii ninaemuona naweza kwenda kwenye kanisa lake, mimi ni Gigy Money nadhani mnajua, lakini pia nina ile hali kwamba watanionaje nikienda kanisani. Nilivyomuona Prophet Malisa kwa mara ya kwanza nilichanganyikiwa nikasema eeeh mbona Nabii Handsome hivi[emoji848] nikasema mtu kama huyu alifaa kuwa video King kwenye nyimbo za wasanii inakuwaje anamtumikia Mungu? lazima ana kitu"

"Nikasema mbona yupo kwa Mungu na uzuri wote huu, nikasema ngoja nimsikilize, ndio maana nimekuja hapa kusikiliza kilichopo ndani ya Nabii huyu"- Gigy Money.

2. Sababu Kutoka Kwa Wolper [emoji116][emoji116][emoji116]

"Prophet Malisa Nimekuwa Nakufatilia Saana You tube Nikapendezwa na Mahubiri yako,Nilipoingia Mahali hapa Nilipokea nguvu ya Mungu ndani yangu, Kwenye nyumba ya Mungu Mtu ukivaa miwani kama hii niliyovaa inakuwa ni kama vile Namzoom Mungu lakini Mimi nimevaa sio Kama nimependa kuvaa Nikama macho yangu yamevimbaa Kwa kulia,.wiki nzima hii Nimekuwa nikilia tuu kwajili ya Mtoto wangu P ,,Naamini kifika kwenye Madhabau hii Mwanangu P anakwenda kupokea Uponyaji,,

Kila la kheri na safari yao ya imani [emoji120][emoji120]

View attachment 2724535View attachment 2724537
Kama ni yule Malisa wa ubungo kibangu hawa watakuwa hawara zake. maana huyo dogo malisa alimpiga chini mkewe akamchukua demu mwingine hapohapo kanisani na kanisa likapasuka. Baadhi ya watu wakaondoka na ex wife wake.
 
Ni kweli ila usisahau biblia ni kazi ya fasihi. Kwa sasa watu wote wanaokaa madhabahuni wamechukua nafasi ya walawi japo sheria haijawahi badilika so na wao wanabanwa na kanuni hizo hizo.

Tukikaa kwenye dhana yako ni sawa na tuseme Biblia haimhusu kabisa mtu mwengine yeyote.tofauti na Myahudi. Jambo ambalo kuna.wakati ni kweli pia, tumeforce sana ituhusu.
Biblia Takatifu ina ujumbe mmoja tu ujulikanao nao ni UKOMBOZI, soma kuanzia kitabu cha Mwanzo hadi kitabu Ufunuo ujumbe ni ule ule wa UKOMBOZI WA MWANADAMU.

Kwa mambo ya Walawi ni sheria zilizotungwa kwa ajili ya kundi la watumwa wenye mioyo migumu walioleta ubishi kuhusu wao kukombolewa kutoka utumwani Misri. Ukisoma habari zao utaona kwamba walikuwa ni wasumbufu na wabishi wengi wao walifia jangwani. Hao ndio wayahudi na hawamkuli Yesu Kristo.

Sisi tulioamini tusio wayahudi tumetokana na lile agizo la Yesu "enendeni ulimwenguni kote mkawafanye mataifa kuwa wanafunzi...... "

Kwa kuamini tulifanyika kuwa wanafunzi (wafuasi) wa Kristo.

Tumeokolewa kwa kumwamini Kristo.

Hatuokolewi kwa kufuata sheria za walawi. Pamoja na hayo tunasoma(agano la kale) Mambo ya walawi ili kuelewa mwanzo wa mission ya UKOMBOZI ilivyoanza(kwa wayahudi pekee), tunapoingia kwenye (agano jipya) ukamilifu wa mission ya UKOMBOZI unadhirika kwa watu wa mataifa yote.

Jitahidi kuisoma na kufahamu Biblia ndugu.
 
Kama ni yule Malisa wa ubungo kibangu hawa watakuwa hawara zake. maana huyo dogo malisa alimpiga chini mkewe akamchukua demu mwingine hapohapo kanisani na kanisa likapasuka. Baadhi ya watu wakaondoka na ex wife wake.
Bosi naomba ufungue uzi kuhusu hiyo scandal ya Malisa tuijadili vizuri, tutawasaidia wengi.
 
Back
Top Bottom