Gigy Money na Jackline Wolper wahamia kwa Nabii Malisa

Wanawake wengi ni rahisi sana kushawishika, ndivyo walivyoumbwa, hata nyoka alipitia kwa Eva ili kumhadaa Adam..
 
Usisahau kuwa walawi sio wabongo wala waniga, so hizo sheria za kilawi haziwahusu
Ni kweli ila usisahau biblia ni kazi ya fasihi. Kwa sasa watu wote wanaokaa madhabahuni wamechukua nafasi ya walawi japo sheria haijawahi badilika so na wao wanabanwa na kanuni hizo hizo.

Tukikaa kwenye dhana yako ni sawa na tuseme Biblia haimhusu kabisa mtu mwengine yeyote.tofauti na Myahudi. Jambo ambalo kuna.wakati ni kweli pia, tumeforce sana ituhusu.
 
Kama ni yule Malisa wa ubungo kibangu hawa watakuwa hawara zake. maana huyo dogo malisa alimpiga chini mkewe akamchukua demu mwingine hapohapo kanisani na kanisa likapasuka. Baadhi ya watu wakaondoka na ex wife wake.
 
Biblia Takatifu ina ujumbe mmoja tu ujulikanao nao ni UKOMBOZI, soma kuanzia kitabu cha Mwanzo hadi kitabu Ufunuo ujumbe ni ule ule wa UKOMBOZI WA MWANADAMU.

Kwa mambo ya Walawi ni sheria zilizotungwa kwa ajili ya kundi la watumwa wenye mioyo migumu walioleta ubishi kuhusu wao kukombolewa kutoka utumwani Misri. Ukisoma habari zao utaona kwamba walikuwa ni wasumbufu na wabishi wengi wao walifia jangwani. Hao ndio wayahudi na hawamkuli Yesu Kristo.

Sisi tulioamini tusio wayahudi tumetokana na lile agizo la Yesu "enendeni ulimwenguni kote mkawafanye mataifa kuwa wanafunzi...... "

Kwa kuamini tulifanyika kuwa wanafunzi (wafuasi) wa Kristo.

Tumeokolewa kwa kumwamini Kristo.

Hatuokolewi kwa kufuata sheria za walawi. Pamoja na hayo tunasoma(agano la kale) Mambo ya walawi ili kuelewa mwanzo wa mission ya UKOMBOZI ilivyoanza(kwa wayahudi pekee), tunapoingia kwenye (agano jipya) ukamilifu wa mission ya UKOMBOZI unadhirika kwa watu wa mataifa yote.

Jitahidi kuisoma na kufahamu Biblia ndugu.
 
Kama ni yule Malisa wa ubungo kibangu hawa watakuwa hawara zake. maana huyo dogo malisa alimpiga chini mkewe akamchukua demu mwingine hapohapo kanisani na kanisa likapasuka. Baadhi ya watu wakaondoka na ex wife wake.
Bosi naomba ufungue uzi kuhusu hiyo scandal ya Malisa tuijadili vizuri, tutawasaidia wengi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…