Nilipata mfahamu jamaa mmoja alikuwa anauza mishkaki kwa waarabu, baada ya muda akawa na ukwasi wa kutosha.majumba,magari,na vitega uchumi sana tu.
kila mmoja alisema lake kuhusu utajiri wa jamaa, oparesheni ya ujangiri ikaja mkumba jamaa kumbe alikuwa anashirikiana na waarabu kuuza pembe za ndovu.
jamaa akakamatwa na mzigo na kuwataja wahusika,ikiwemo matajiri flani wa mjini hapa. tangu hapo mtu ukiniletea habari za fulani aliuza mchicha, mihogo, sijui kababu nakuoa bwege tu.
kuna michakato nyuma ya pazia kwenye haya mafanikio ya watu.