Githeri Man awaunganisha Wakenya wakati wa taharuki kwenye mtandao

Githeri sio makande as such, kwa wadau wa kanda ya kaskazini mnajua makukuru, wachaga wanaita ngararum.. Ni mahindi ambayo hayajakobolewa yanachangwanywa na maharage kisha yanatiwa magadi kiaina.. Tofauti na makande ambayo mahindi yamekobolewa na hayawekwi magadi
 
Githeriman tibim! Kweli, kila mtu na siku yake! Britania wanamtaka, KWS wanataka kufanya kazi naye, KCB bank na Safaricom pia. Maina Kageni amesema yeyote atakayemfikisha kwa studio za CapitalFm anapewa 20,000 mara that that! KissFm wanamngoja pia. Yote hayo kwasababu jamaa alihisi njaa wakati akingoja kupiga kura! Wanaosema Mungu hayupo ni mambumbumbu tu.
 
Licha ya kuwepo miongoni mwa wananchi kuhusu matokeo ya kura ya urais, Wakenya kwenye mitandao ya kijamii Jumatano na Alhamisi waliunganishwa na picha ya mwanamume mmoja aliyekuwa akifurahia mlo wa Githeri kwenye foleni ya kupiga kura hapo Jumanne.

Mwanamume huyo ambaye amebandikwa jina 'Githeri Man' alinaswa na kamera ya mmoja wa wapiga kura akila mchanganyiko wake wa mahindi na maharage alioutia ndani ya karatasi ya plastiki katika kijibaridi cha asubuhi ya Jumanne.

Hadi wakati wa kuchapishwa kwa habari hii, jina lake halikuwa limetambulika wala anapoishi, kituo ambapo alipiga kura yake na aliyeipiga.

Kwenye Twitter Githeriman picha ya mwanamume huyo ilihaririwa na kuwekwa katika hali ambazo ziliibua msisimko mkubwa na utani usio na kifani.

Mojawapo ya picha hizo ilionyesha mwanamume huyo akiwa katikati ya Rais Kenyatta, Naibu Rais William Ruto na vinara wa NASA Raila Odinga na Kalonzo Musyoka.

Katika picha nyingine, alionyeshwa akifika Canaan. Msisimko wa safari ya Canaan ulianzishwa na Bw. Raila Odinga aliyasema atakuwa 'Yoshua' na kuwaongoza wakenya kutoka 'Misri'.

Alionekana pia akiwa kondakta, huku pia akitokea katika studio za Runinga za NTV na Citizen. Kwenye Spoti haikuachwa nyuma kwenye uchangamfu huo, mwanamume huyo alionekana kwenye picha mbalimbali.

Daniel Ndambuki wa Churchill Show anamsaka amhoji katika kipindi chake. Mimi niko tayari kumchangia pesa. Kubeba kwake githeri kunaonyesha alikuwa amejitolea kupiga kura. Amewaunganisha wakenya wote katika wakati wa taharuki. Tusherehekee maisha yake.

Ni kuhaririwa kwa picha hiyo ambako kulichangia wakenya mtandaoni kupunguza jumbe za chuki baada ya mwaniaji urais wa NASA, Raila Odinga kudai kwamba mfumo wa KIEMS wa IEBC ulidukuliwa usiku wa kuamkia Jumatano na kuweka matokeo ya uwongo.
 
huyo jamaa yaan kawa man of ze match ghafla
Kweli, ya mungu ni mengi aisee! Britania kampuni ya biskuti na kadhalika wametumia katuni ikila githeri kwa tangazo lao. Sasa hivi wanamtafuta ili wamlipe kwa kutumia katuni inayofanana naye! Dah! KWS, Safaricom na KCB bank wote wanamtaka! Jamaa anafanyia Nairobi County kazi ya kufagia!
 
He looks like Nigerian film star "Usihofu"
Hahahahahahaha
 
ndiyo maisha yalivyo.........supu imemuangukia mdomoni

ila katisha kawa man of ze match zaidi ya uhuru aiseee inaelekea jamaa anaucomedy kwa mbali[emoji15] [emoji23] [emoji23]
 
Zinachekesha sana daaaaah [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]

Sent from my Android phone
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…