Giza nene alipo Tundu Lissu, Magereza wasema wanafuatilia

DogoWaNjombe

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
3,284
Reaction score
7,708
Go4bdx2WsAAA1Iq.jpg
Chama Cha Demokrasia na Maendeleo Chadema bado kimeendelea kusisitiza kuhusu msimamo wake wa Jana Aprili 18, 2025 wa kulitaka Jeshi la Magereza na Vyombo vingine vya Dola kueleza kwa "haraka" alipo Mhe. Tundu Lissu, Mwenyekiti wa Chadema Taifa, wakieleza kuwa mara baada ya saa 24 kupita, wataeleza umma kuhusu hatua zitakazofuata ikiwa bado haitokuwa inajulikana alipo Mhe. Tundu Lissu.

Kauli ya Chadema kupitia kwa Mkurugenzi wake wa uenezi na Mawasiliano Bi. Brenda Rupia inakuja takribani saa 18 tangu kuchapishwa kwa Taarifa yake kwa Vyombo vya habari, ambapo mpaka sasa si Jeshi la Magereza, serikali ama chombo chochote cha Dola kilichoeleza alipo Mwenyekiti wa Chadema Tundu Lissu, zaidi ya kile kilichozungumzwa mapema Jana na Msemaji wa Magereza Bi. Elizabeth Mbezi aliyekiambia chombo kimoja cha habari kuwa ingali Jeshi hilo linafuatilia kujua kilichotokea.

Lissu amekuwa akishikiliwa mahabusu katika Gereza la Keko lililopo jijini Dar Es Salaam toka alipofunguliwa mashtaka ya uhaini juma lililopita na Chadema ililitaka jeshi la Magereza, mamlaka husika na vyombo vya dola kutoa taarifa wazi na haraka kwa umma kuhusu mahali alipopelekwa Bw. Lissu.

Kando ya Jeshi la Magereza, Kulingana na BBC Swahili, Msemaji wa Serikali ya Tanzania Gerson Msigwa alipoulizwa kuhusu madai ya viongozi wa Chadema na familia kuzuiwa kumuona Lissu na taarifa kuwa ametolewa gerezani, Msigwa naye alijibu kusema kuwa maswali hayo waulizwa Jeshi la Magereza.

Leo Aprili 19, 2025, Brenda Rupia akizungumza na JamboTv kuhusu msimamo wa Chadema mara baada ya taarifa yao ya jana na ukimya mkubwa unaoendelea kutanda meieleza JamboTv kuwa " Kumtafuta mtu ni saa 24, tumetoa taarifa na tunasubiri saa 24 zipite tuje na maamuzi mengine na msijali JamboTv pia tutawaita maana tutakuwa na Mkutano na wanahabari kueleza kile kitakachofuata kama msimamo wa Chama", ameeleza.

Jambo TV mapema leo Jumamosi ilipowatafuta idara ya Habari ya Jeshi la magereza moja ya maofisa habari amesisitiza kuwa taarifa ya msemaji wa Jeshi la magereza ni ile aliyoitoa kwa Vyombo vya Habari jana ijumaa kuwa Bado Idara hiyo inafuatilia SAKATA hilo hivyo Wananchi wawe na utulivu wakati wakisubiri taarifa kamili ya alipo Mhe. Tundu Lissu.

Kulingana na Vyanzo mbalimbali vya habari, Gereza la Keko linalopatikana Temeke Jijini Dar Es salaam, alipokuwa akishikiliwa Tundu Lissu awali ni miongoni mwa magereza machache nchini yaliyojengwa kwa hadhi ya pekee, ikitajwa kuwa ndiyo sababu ya kuwa chaguo namba moja katika kuhifadhiwa hapo kwa Watu mashuhuri, viongozi mbalimbali na watu wenye Kesi za pekee ambazo ni nadra kutokea nchini Tanzania.

Kwa upande mwingine Kulingana na Tovuti ya Jeshi la Magereza, Katika kutekeleza majukumu yake Jeshi la Magereza linawajibika kufuata na kuheshimu sheria zote za nchi pamoja na sheria mbalimbali za kimataifa zinazohusu haki za binadamu, likieleza kuwa mawakili wana haki ya kuwatembelea wafungwa au mahabusu wanaowawakilisha siku yoyote na wakati wowote. Suala la usiri wa mawasiliano baina ya wakili/mwanasheria na mfungwa/mahabusu ambaye ni mteja wao litaheshimiwa.

Chanzo: Jambo TV
 
Jana si kulikuwa na Barua ya Msemaji wa Jeshi la magereza kwamba Bado yupo huko Keko. Na hajahamishiwa Uk
 
Hawa magereza ndiyo maana polisi wanawaendesha tu hovyo. Juzi prison wamzeuiwa gari lao wananchi wamewatetea sasa nao wanaanza kuingia kwenye kundi la mapolisi. Watajiharibia taswira waliyonayo. Kuirudisha sio rahisi.
 
Jana si kulikuwa na Barua ya Msemaji wa Jeshi la magereza kwamba Bado yupo huko Keko. N

Au kama yeye Lisu hataki kuonwa sio kazi ya Jeshi la Magereza kumsemea .

Mahabusu ana haki zake pia ikiwemo kukataa kuonwa na yeyote

Magereza wameshamaliza kuongea yuko Keko .Wanataka nini sasa?

Sio maadili ya magereza kutangaza kuwa mtu wenu hataki kuonwa
 
Kama Magereza hawajui, nani mwingine atakayejua?

Hizi mbinu za kizamani zipo mpaka leo karne ya AI.

Kweli anayelala usimwamshe......
 
Inawezekana wamemuua kwa sumu sasa wanahaha jinsi ya kuileza dunia amekufa kufaje mikononi mwao. Ilaaniwe CCM na serikali yake dhalimu.
 
Au kama yeye Lisu hataki kuonwa sio kazi ya Jeshi la Magereza kumsemea .

Mahabusu ana haki zake pia ikiwemo kukataa kuonwa na yeyote

Magereza wameshamaliza kuongea yuko Keko .Wanataka nini sasa?

Sio maadili ya magereza kutangaza kuwa mtu wenu hataki kuonwa
Una akili kama viongozi wako. Hujasikia jeshi la magereza likikanusha habari inayoenea kwamba limesema Lissu yuko salama keko? Habari ya mwisho ni kwmba jeshi la magereza bado linafuatilia kilichotokea.
 
Back
Top Bottom