mitale na midimu
JF-Expert Member
- Aug 26, 2015
- 10,420
- 17,735
Wanadamu hawakuanza Kunena kwa Lugha (Glossolalia) iliyonje ya uelewa wao pale Yerusalem kama ilivyoandikwa kwenye baadhi ya Vitabu Vitakatifu.
Miaka Mingi BC kuna matukio kadhaa ya watu kunena kwa Lugha zilizonje ya Uwezo wao wa kibinadamu.
Hata kabla ya ukristo kufika maeneo mengi kunena kwa Lugha kumekuwepo maeneo ya China, Japan, Korea, Malaysia, Indonesia, Siberia, Arabia, Burma, na maeneo mengi ulimwenguni ikiwemo Afrika.
Kwa Makabila ya Waeskimo, Washamani wa Ethiopia, Voodoo haiti, Kikundi kimoja cha kijadi huko japan kinachoongozwa na GENJI YANAGIDE katika mji wa Moji.
UNENWAJI WA LUGHA SISIZOFAHAMIKA KABLA YA YESU (BC)
Mwaka 1100 BC kulikuwa na kikundi kidogo cha watu waliofahamika kama "Amen worshipers" ambacho mmumuni alipoingiliwa na muungu(god) alipoteza ufahamu na kuanza kunena kwa lugha na maneno yasiyoelewaka kwa wasikilizaji wake.
ZAMA ZA WAGIRIKI
Miaka ya 400 BC mwanafilosofia nguli wa kigiliki PLATO katika maandiko yake amerekodi uwepo wa watu wengi waliokuwa wakinena kwa lugha zisizoeleweka wakiwa katika kuomba miungu yao. Matukio hayo yaliambatana na uponywaji wa watu hao.
ZAMA ZA WARUMI
Karne moja BC ulimwengu wa wakati ho ukiwa chini wa Dola la kirumi, kuhani wa kike SYBILLINE katika kisiwa cha DELOS walipokuwa katikati ya maombi kwa Mungu wao APOLLO walijikuta wakinena kwa lugha zisizoeleweka. Hii ilitokea alipokuwa akitafakari katika pango oja huko kisiwani.
Katika Ibada za mungu Mithra huko Uajemi, Osiris huko Misri, Dionizi huko Macedonia, Kote kunaonekana ibada hizo ziliambatana na matamshi ya Lugha zisizoeleweka.
Kabla ya mwaka 34AD kulitokea tukio la WAGALILAYA waliokuwa katika Yerusalem kunena kwa lugha mpya ambazo zilikuwa nje ya ufahamu wao. Kama inavyoelezwa katika kitabu cha bibilia.
Ufafanuzi wa tukio hilo (Matendo 2), Waliokuwepo siku hiyo, wayahudi waliotoka nchi mbalimbali kuja kwenye Sikukuu ya Siku ya Hamsini ya malimbuko (Pentecoast), na wasio wayahudi walioongoka wa makabila yote WALIWASIKIA WAKINENA KWA LUGHA ZAO na Sio lugha zisizoeleweka, maana lisingekuwa tukio jipya kwani watu kunena lugha zisizoeleweka ilikuwa ni kawaida kwa jamii karibu zote za enzi hizo.
Kuna matukio Mengi ya watu kuendelea kunena kwa Lugha zisizofahamika hata.
Mfano.
Mwaka (120-198 AD) Mwandishi Lucian wa Somosata anaandika Huko Syria katikati ya ibada za mungu wa kike wa kisyria JUNE, watu walinena kwa lugha zisizoeleweka.
MWISHO
Bandiko hili linalengo la kutanua uelewa juu ya mambo yanayoendelea katika jamii. Usishangae kuona watu wakiwa katika ibada zote za kijadi na za kimagharibi wakinena wakati flani lugha zinazofanana japo hazieleweki.
Lakini pia ni kufahamu kuwa Mwanadamu kutamka Lugha nje ya uwezo wake wa asili ni tukio ambalo lilikuwepo hata kabla ya Yesu (BC).
Jambo lingine usije ukashangaa mambo yanayofanyika katika nyumba za Sala yakafanana na Yale yanayofanyika katika madhabahu za nje ya vitabu vitakatifu.
Video hapo juu inaonyesha WATU Wakivuviwa na ROHO WA KIHINDU katikati ya KUNDALINI YOGA ufanano huu usikutishe bali ukuongezee uelewa wa kuwa raia bora wa dunia.
Karibuni kwa maoni mbalimbali wanaintelijensia na watu wa fikra mtambuka.