Glossolalia: Kunena kwa Lugha mpya Wagiriki,Warumi, Wagalilaya na Waganga.

Glossolalia: Kunena kwa Lugha mpya Wagiriki,Warumi, Wagalilaya na Waganga.

mitale na midimu

JF-Expert Member
Joined
Aug 26, 2015
Posts
10,420
Reaction score
17,735
maxresdefault.jpg

Wanadamu hawakuanza Kunena kwa Lugha (Glossolalia) iliyonje ya uelewa wao pale Yerusalem kama ilivyoandikwa kwenye baadhi ya Vitabu Vitakatifu.

Miaka Mingi BC kuna matukio kadhaa ya watu kunena kwa Lugha zilizonje ya Uwezo wao wa kibinadamu.
Hata kabla ya ukristo kufika maeneo mengi kunena kwa Lugha kumekuwepo maeneo ya China, Japan, Korea, Malaysia, Indonesia, Siberia, Arabia, Burma, na maeneo mengi ulimwenguni ikiwemo Afrika.

speakingintongues.jpg

Kwa Makabila ya Waeskimo, Washamani wa Ethiopia, Voodoo haiti, Kikundi kimoja cha kijadi huko japan kinachoongozwa na GENJI YANAGIDE katika mji wa Moji.

UNENWAJI WA LUGHA SISIZOFAHAMIKA KABLA YA YESU (BC)

Mwaka 1100 BC kulikuwa na kikundi kidogo cha watu waliofahamika kama "Amen worshipers" ambacho mmumuni alipoingiliwa na muungu(god) alipoteza ufahamu na kuanza kunena kwa lugha na maneno yasiyoelewaka kwa wasikilizaji wake.

ZAMA ZA WAGIRIKI
Miaka ya 400 BC mwanafilosofia nguli wa kigiliki PLATO katika maandiko yake amerekodi uwepo wa watu wengi waliokuwa wakinena kwa lugha zisizoeleweka wakiwa katika kuomba miungu yao. Matukio hayo yaliambatana na uponywaji wa watu hao.

ZAMA ZA WARUMI
20b4a473d3e73821cbd7ae9bd2f97aec.jpg

Karne moja BC ulimwengu wa wakati ho ukiwa chini wa Dola la kirumi, kuhani wa kike SYBILLINE katika kisiwa cha DELOS walipokuwa katikati ya maombi kwa Mungu wao APOLLO walijikuta wakinena kwa lugha zisizoeleweka. Hii ilitokea alipokuwa akitafakari katika pango oja huko kisiwani.

Katika Ibada za mungu Mithra huko Uajemi, Osiris huko Misri, Dionizi huko Macedonia, Kote kunaonekana ibada hizo ziliambatana na matamshi ya Lugha zisizoeleweka.

pentecost.jpg

Kabla ya mwaka 34AD kulitokea tukio la WAGALILAYA waliokuwa katika Yerusalem kunena kwa lugha mpya ambazo zilikuwa nje ya ufahamu wao. Kama inavyoelezwa katika kitabu cha bibilia.
Ufafanuzi wa tukio hilo (Matendo 2), Waliokuwepo siku hiyo, wayahudi waliotoka nchi mbalimbali kuja kwenye Sikukuu ya Siku ya Hamsini ya malimbuko (Pentecoast), na wasio wayahudi walioongoka wa makabila yote WALIWASIKIA WAKINENA KWA LUGHA ZAO na Sio lugha zisizoeleweka, maana lisingekuwa tukio jipya kwani watu kunena lugha zisizoeleweka ilikuwa ni kawaida kwa jamii karibu zote za enzi hizo.

Kuna matukio Mengi ya watu kuendelea kunena kwa Lugha zisizofahamika hata.

Mfano.
Mwaka (120-198 AD) Mwandishi Lucian wa Somosata anaandika Huko Syria katikati ya ibada za mungu wa kike wa kisyria JUNE, watu walinena kwa lugha zisizoeleweka.

MWISHO
Bandiko hili linalengo la kutanua uelewa juu ya mambo yanayoendelea katika jamii. Usishangae kuona watu wakiwa katika ibada zote za kijadi na za kimagharibi wakinena wakati flani lugha zinazofanana japo hazieleweki.

Lakini pia ni kufahamu kuwa Mwanadamu kutamka Lugha nje ya uwezo wake wa asili ni tukio ambalo lilikuwepo hata kabla ya Yesu (BC).

Jambo lingine usije ukashangaa mambo yanayofanyika katika nyumba za Sala yakafanana na Yale yanayofanyika katika madhabahu za nje ya vitabu vitakatifu.
Video hapo juu inaonyesha WATU Wakivuviwa na ROHO WA KIHINDU katikati ya KUNDALINI YOGA ufanano huu usikutishe bali ukuongezee uelewa wa kuwa raia bora wa dunia.

Karibuni kwa maoni mbalimbali wanaintelijensia na watu wa fikra mtambuka.
 
hivi hizo lugha huwa zinaashiria nini?
Ngoja wanaozinena watakuja kueleza vizuri.
Waganga, baadhi ya wakristo wanaozipenda, na wajadi wa makabila mbalimbali maana zote hazieleweki lakini kila mmoja anasababu yake.

Ila wale jamaa wagallilaya ilikuwa wazi.
Zilieleweka, na maana ilikuwa wazi Ujumbe wa Mwalimu wao ulipaswa uende kwa kila kabila na jamaa, Hivyo walihitaji supernatural ability ya kunena lugha zaidi ya kiebrania au kigiriki ili na sisi huku tupate hicho walichoagizwa kutueleza.
 
Leo nimegundua kitu,
Kumbe waganga nao hunena kwa lugha..
Kwa hiyo waganga,walokolee ndo hunena kwa lugha.
Nasikia pia MTU akiwa na mapepo

mkuu hawa sio wakristo. Lakini nao wananena kwa lugha zao wanazozijua wao kutoka wanakojua wao.
 
Ninachoamini kwa wakristo waliookoka walipokea vibaya (bila ya kujua) kipengele cha kinena kwa lugha.
 
Kunena kwa lugha hushuka kwa mtu automatically pale anaposali na kuelekeza akili yake yote kwa hisia ya hali ya juu kwa yule anaemuamini au kumuabudu bila Kuwa na mawazo hasi juu ya huyo mtu, kitu, roho au kiumbe.
 
Kuna kitu kimoja kinabidi kieleweke. Hao ni majini(mapepo) yanayowaingia watu. Na majini wanafahamu lugha za namna nyingi za hapa Duniani. Kama tunavyofahamu Duniani Kuna lugha kuu nyingi ambazo zinatumika kama lugha za Taifa, kuna lugha za makabila vilevile na makabila yapo mengi. Kwa hiyo kunena kwa lugha isiyoeleweka si kwamba nguvu za Mungu zinakushukia, hapana. Nguvu za Mungu hazishuki kwa namna hiyo. Isipokuwa hao ni majini(mapepo) wanawaingilia watu na kunena kwa lugha za mataifa/ makabila mbalimbali. Hata hapa kwetu yanajitokeza, mtu anaweza akawa Mnyakyusa akapandisha majini( mapepo) akanena kwa lugha ya kimasai.

Weka dhana katika hilo kama miaka ya nyuma Wanyakyusa hawakuwafahamu Wamasai wangelisemaje? Lugha ya kimasai hawaielewi bila shaka nao wangelisema "Mizimu imenena nasi".
 
Ndo kusema roho mtakstifu sasa ni jini au pepo,tofauti ni kuwa kuna pepo wabaya ambao ndo mashetani na pepo wema ambao ni kama malaika?
Maana wote hawaonekani.
Tafsiri ya jini kama sikosei ni...isiyoonekana kwa maana ya invisible.
He hii INA explain kwanini waganga wananena kwa lugha kwa kutumia pepo wabaya na watu wa dini wananena kwa lugha kwa kutumia pepo wema au roho mtakatifu?
Kwa maana kuna nguvu chanya kama kiwakilishi cha Mungu na ile hasi ya shetani na wrote wana wasaidizi wao ama majini?
 
nilichoelewa hapa.

Mtu akiwa na akili timamu na uanadamu wake hawezi kunena kwa Lugha ambayo hajawahi kuifahamu au isiyoeleweka.
Shetani anaweza kuigiza kile ambacho Mungu amekisema.
Mtu anaweza kupagawa na Pepo akanena kwa Lugha mpya (inayoeleweka au isiyoeleweka), na fact ya hapa mapepo au majini sio wanadamu na wanagrobal operation hivyo wanajua Lugha zote.
Pamoja na Hayo Mungu anaweza kumuwezesha mtu wake kuongea Lugha asiyoielewa ili afikishe ujumbe aliokusudia licha ya ukweli kwamba hata shetani anaweza hilo (matendo 2).
Hujazungumzia lugha zisizoeleweka ambazo hazipo kabisa katika ulimwengu huu. Historia na uhalisia inaonyesha hizo nazo hunenwa na waganga, watu waliopagawa na mapepo na pia kuna watu wanazinena kwenye makanisa wakidai zao ni za mbinguni au za Malaika.
Kama malaika wanaLugha basi hata mapepo wanazijua maana nao walikuwa malaika. Na kama huo ni ukweli swali linaibuka Utatofautishaje lugha za mapepo na za mbinguni?

Changamoto hii inapaswa kuwafikirisha wapenzi na waumini wa Lugha zisizoeleweka.
 
nadhani changamoto hii inatosha kuwafanya wakristo wa zama hizi ambazo mapepo wamechachamaa na roho wa kweli naye yuko kazini wajiepushe na mtego wa kuhitimisha kuwa mtu Kufanya Miujiza au Kunena kwa Lugha tata zisizoeleweka ni kigezo cha kuwa Mtu wa Mungu.
Mtego huu Utapoteza Wengi sana.

Kigezo kikubwa kiwe ni usambamba wa maneno yake na Bibilia. Ili ukidhi viwango vya kutambua hayo muumini anapaswa kujenga urafiki wa kudumu na bibilia ili aweze kuchambua chuya na mchele.

maoni.
 
nilichoelewa hapa.

Mtu akiwa na akili timamu na uanadamu wake hawezi kunena kwa Lugha ambayo hajawahi kuifahamu au isiyoeleweka.
Shetani anaweza kuigiza kile ambacho Mungu amekisema.
Mtu anaweza kupagawa na Pepo akanena kwa Lugha mpya (inayoeleweka au isiyoeleweka), na fact ya hapa mapepo au majini sio wanadamu na wanagrobal operation hivyo wanajua Lugha zote.
Pamoja na Hayo Mungu anaweza kumuwezesha mtu wake kuongea Lugha asiyoielewa ili afikishe ujumbe aliokusudia licha ya ukweli kwamba hata shetani anaweza hilo (matendo 2).
Hujazungumzia lugha zisizoeleweka ambazo hazipo kabisa katika ulimwengu huu. Historia na uhalisia inaonyesha hizo nazo hunenwa na waganga, watu waliopagawa na mapepo na pia kuna watu wanazinena kwenye makanisa wakidai zao ni za mbinguni au za Malaika.
Kama malaika wanaLugha basi hata mapepo wanazijua maana nao walikuwa malaika. Na kama huo ni ukweli swali linaibuka Utatofautishaje lugha za mapepo na za mbinguni?

Changamoto hii inapaswa kuwafikirisha wapenzi na waumini wa Lugha zisizoeleweka.
Ulichokiandika ni ghali na kizito. Maandishi yako yananyofoa mpaka mizizi katika baadhi ya imani za wahusika. Uhofii kuibua mjadala na hao wahusika?
 
Ulichokiandika ni ghali na kizito. Maandishi yako yananyofoa mpaka mizizi katika baadhi ya imani za wahusika. Uhofii kuibua mjadala na hao wahusika?
nitatoa maoni yangu wakiwepo watakaodhani kuna haja...
kutofautiana kimaoni na mitazamo pia hukamilisha ubinadamu wetu. hivyo kuwa na mitazamo tofauti sio dhambi .
 
nitatoa maoni yangu wakiwepo watakaodhani kuna haja...
kutofautiana kimaoni na mitazamo pia hukamilisha ubinadamu wetu. hivyo kuwa na mitazamo tofauti sio dhambi .
Bila shaka wewe ni mwerevu sana, sikudhani kama ungelitoa jibu zuri la namna hiyo na wala fikra ya namna hiyo sikuwahi kuwa nayo. Shukrani kwa kunipatia hayo maarifa.
 
kunena kwa lugha kwa kwetu hapa naona kama kuna fanana na kuna karirika

tembelea mikutano ya injili ya makanisa yanayojiita ya kiroho utagundua mchungaji huyu na yule hujikuta wakitamka kama vitu vinavyo fan

koooooraaaa mashaka abhabababab ndorobobobobobo na kuyarudia rudia tu

halafu hata dakika haiishi sasa unjiuliza huwa wanapewa semina elekezi kabla ya kuwa wachungaji? kwanini yafanane?
 
Hoja uliyoileta ni hoja nzuri, tunawaomba wahusika kama wanafuatilia huu Uzi waje watusaidie.
 
Mbona hata Dr Manyaunyau huwa ananena lugha ya kipepo?
duniani kote watu wa utamaduni hupractice glossolalia.
watu wa imani pia.
hivyo kazi inabaki kwa wanaimani kuchambua kipi ni sahihi.
japo sio kweli pia Ukinena kwa lugha isiyoeleweka huku umeshika bibilia ni kigezo kuwa lugha hiyo ni ya Mungu inaweza kuwa kinyume pia. Maana hata Shetani hashiki tu bibilia bali amekariri Yote ingawa hamuamini na kumuabudu Yesu anayefunuliwa humo.

uzi huu ni changamoto na fikkirishi kwa waumini, waanze kuwa na uelewa wa kila wanachokifanya. kitu hakiwi halali kisa kimefanyikia kanisani. Huko nyuma kwenye historia ya bibilia Watu wa Mungu waliwahi kuabudu miungu ya kipepo hekaluni.

Ezekiel 8:
14 Ndipo akanileta mpaka mlango wa kuingilia katika nyumba ya Bwana, ulioelekea upande wa kaskazini, na tazama, wanawake wameketi wakimlilia Tamuzi.

15 Akaniambia, Mwanadamu umeyaona haya? Utaona tena machukizo makubwa kuliko hayo
.
Tammuz alikiwa mungu wa kipepo kama hao wa manyaunyau.

watu wanapaswa kuwa makini na kila tendo la ibada wasirudie makosa yaliyowahi kutokea huko nyuma.
hii ni changamoto tu.
 
nilichoelewa hapa.

Mtu akiwa na akili timamu na uanadamu wake hawezi kunena kwa Lugha ambayo hajawahi kuifahamu au isiyoeleweka.
Shetani anaweza kuigiza kile ambacho Mungu amekisema.
Mtu anaweza kupagawa na Pepo akanena kwa Lugha mpya (inayoeleweka au isiyoeleweka), na fact ya hapa mapepo au majini sio wanadamu na wanagrobal operation hivyo wanajua Lugha zote.
Pamoja na Hayo Mungu anaweza kumuwezesha mtu wake kuongea Lugha asiyoielewa ili afikishe ujumbe aliokusudia licha ya ukweli kwamba hata shetani anaweza hilo (matendo 2).
Hujazungumzia lugha zisizoeleweka ambazo hazipo kabisa katika ulimwengu huu. Historia na uhalisia inaonyesha hizo nazo hunenwa na waganga, watu waliopagawa na mapepo na pia kuna watu wanazinena kwenye makanisa wakidai zao ni za mbinguni au za Malaika.
Kama malaika wanaLugha basi hata mapepo wanazijua maana nao walikuwa malaika. Na kama huo ni ukweli swali linaibuka Utatofautishaje lugha za mapepo na za mbinguni?

Changamoto hii inapaswa kuwafikirisha wapenzi na waumini wa Lugha zisizoeleweka.
Uko vizuri na sahihi mkuu
 
Back
Top Bottom