Wafuatao ndo wakulaumiwa either mmoja wao, wawili au wote kwa pamoja.
1. Msanifu jengo husika (Arch/Engineer); kwa kushindwa kuandaa na kuproduce structure analysis za hilo jengo ambazo ndio miongozo ya kipi fundi anatakiwa ajenge na kuzingatia.
2. Mmiliki wa jengo; Kama mmiliki alikuwa bahili, akataka dezo kujenga structure sensitive Kama ghorofa kwa kutumia mafundi tu bila wataalam wa usanifu Majengo, Basi matunda ya ubahili huo ndo hayo. Na hili ni tatizo kwa watanzania wengi, wanapenda Sana cheap na kurash mambo kuliko kufuata procedures zinazotakiwa.
3. Mafundi; hapa Kuna mawili,
Mosi, Yawezekana mafundi hawakuwa na uzoefu au ujuzi wa kujenga high structural building, ikiwemo kushindwa kutafsiri lugha ya kihandisi iliyopo kwenye sheets za raman, hasa structural plans ambazo huitaji akili nyingi kidogo kuzielewa specifications zake.
Pili; Wizi wa materials site, mafundi baadhi siyo waaminifu, unakuta sehemu inayotakiwa atumie ratio ya mortar 1:4 yeye anatumia 1:6 ili tu mifuko ya siment kadhaa apite nayo,
Au unakuta sehemu inayotakiwa kuwekwa zege la Grade 25 yeye anaweka 20 ili tu nondo na siment zitakazo baki ziwe faida yake. Au unakuta anatumia nondo 3 badala ya nne kwenye column au beam kama ilivyoshauriwa na mtaalam.
Ifikie mahali Sasa tuache uswahili kwenye mambo ya mhimu Kama haya ya ujenzi wa maghorofa, mambo ya kupeleka mambo kimazoea matokeo yake ndo hayo yaliyo tokea kwenye huo mpolomoko.