Goba ni uswazi iliyochangamka ni Manzese ama Tandale ya miaka 30 ijayo

Goba ni uswazi iliyochangamka ni Manzese ama Tandale ya miaka 30 ijayo

Goba na milima yake kuanzia Kayuni mpaka huko tegeta A. Kama ingepangiliwa vizuri ikapimwa ingekuwa kama Beverly hills, Capetown RSA, Lavington Nairobi, Cite El nasr Au Menzah VI Tunis au Cairo New city Egypt, Cocody Abidjan Ivorycoast.

Hakuna raha kama mitaa inaelekea milimani halafu nyumba zimepangana. Sijui Nyerere alisahau wapi kuongoza upimaji ardhi na makazi maana yeye peke yake ndio alikuwa na akili za kuona miaka 100 mbele.

Ukitaka kujua nyerere alikuwa na akili angalia ardhi aliyowapimia na kuwapa TPA, Tazara, TRC wangekuwa hawa viongozi wa sasa wasingekuwa na akili ya kuacha ardhi kubwa leo gsm anafaidi eneo la tazara, azam anafaidi eneo la TPA, TRC. Hii kambi ya Lugalo enzi za mwalimu ilikuwa inaanzia mwenge mpaka mto mbezi bondeni kawe yote haikuwepo.
Nyerere ndo sababu ya matatizo yote Tanzania
 
Yaani huwa kuna jambo linanishangaza sana. Unakuta mji baado ila serikali imetulia tu. Baadae umashanhaa hizi nyumba zimetoka wapi? Kwanini hawawahi mapema mpangilio? Ujinga sana. Yaani nyumba ni kali sana ila ndo hivyo. Halafu huko katikati mbona kuna nyumba mbaya nyingi tu? Na ni msururi wa uswazi kbs.
Utasikia nina banda langu goba
 
Hahahah ndioo. Ni gharamaa. Ila pia madalali wamezidi. Wakiambiwa wauze mil 10 wao wanakuuzia mil 50. Very stuppid
Hakuna sehemu Goba utapata kiwanja cha 10m mkuu, labda kama kipo njia ya maji. Kuna sehemu naifaham inaitwa Kulangwa, vidume peke yao ndio wanapamudu..sio poa!
 
Wikiendi iliyopita, Jumamosi na Jumapili nilipata wasaa wa kutembea Goba kwa sehemu kubwa kwa sababu nilikua na ndugu yangu ambae katoka huko mkoani anataka kiwanja na kujenga Dar.

Ndugu yangu kafika hapa tayari alishachagua eneo analolitaka kua ni Goba, basi tukatafta madalali na kuanza kuzungukia viwanja, kuanzia makongo, Goba Senta, Goba Kulagwa, Goba Kilalata kwa awadhi, ostabei na sehemu nyingine nyingi.

Baada ya mizunguko ya siku 2 ndio nikagundua kwamba Goba ni Uswahilini kwenye nyumba za kisasa.

Kwa maana kwamba Goba haijapangiliwa kabisa. Goba kuna nyumba kali na za kisasa sana ila hakujapangwa, nyumba nzuri ila zimejegwa zigzaga, hakuna mitaa iliyonyooka.

Miaka 30 ijayo Goba itakua kama Manzese ya sasa ama Tandale, itakua uswazi.

Ni wakati sasa Serikali inapaswa kuingilia hii biashara ya upimaji na uuzaji ardhi. Hua najiuliza hivi viongozi wetu wakienda huko ulaya hawaoni wenzetu miji yao ilivyopangwa? Mbona huku kwetu wanaacha mambo yanakua hovyo hivi?

Ni hayo tu wakuu.
Mbagala ya Kaskazini Magharibi
 
Hakuna sehemu Goba utapata kiwanja cha 10m mkuu, labda kama kipo njia ya maji. Kuna sehemu naifaham inaitwa Kulangwa, vidume peke yao ndio wanapamudu..sio poa!
Screenshot_20231007_034731_Google Earth.jpg

Hii ndio Goba Kulangwa.

Nyumba nzuri hakuna mpangilio.
 
Unaonesha ww ni dalali

Sent from my Infinix X683 using JamiiForums mobile app
Sijawahi hata kuwaza mkuu, ila Goba naifaham kidogo, hasa maeneo ya kuanzia Mageti, njia nne, njia ya madale....huko hakushikiki chief, kama umefika mitaa wanaita kwa madokta(madr wa muhimbili wana vichuguu huko), hupanunui hata kwa 20m.
 
Hakuna sehemu Goba utapata kiwanja cha 10m mkuu, labda kama kipo njia ya maji. Kuna sehemu naifaham inaitwa Kulangwa, vidume peke yao ndio wanapamudu..sio poa!
Hapo nimetolea mfano mkuu. Madalali wanazinhia sana
 
Sijawahi hata kuwaza mkuu, ila Goba naifaham kidogo, hasa maeneo ya kuanzia Mageti, njia nne, njia ya madale....huko hakushikiki chief, kama umefika mitaa wanaita kwa madokta(madr wa muhimbili wana vichuguu huko), hupanunui hata kwa 20m.
Nina eneo kubwa kidogo hapo flamingo madale ila kwakweli sipendi. Sifurahii jinsi majirani walivyojipangilia
 
Nina eneo kubwa kidogo hapo flamingo madale ila kwakweli sipendi. Sifurahii jinsi majirani walivyojipangilia
Umbali gani toka barabara kuu?
Mbona flamingo, huko mkoroshini ni pazuri tu(japo sipafaham sana)
 
Kwa maana hiyo bhas viwanja vingi vya goba sio surveyed plots, watu wameuziana ile kwenda serikali ya mtaa?

Watu wa mipango mji walikua wapi mda wote huo?

After 20 years mnataka kusema goba itageuka kuwa scansca (tegeta) ?
 
Back
Top Bottom