A
Anonymous
Guest
Nikiwa mmoja kati ya Wakazi wa Goba, naomba kuwasilisha kilio chetu kuhusu changamoto kubwa ya usafiri wa umma inayotukabili sisi wakazi wa Goba na maeneo yanayotuzunguka.
Kwa sasa hatuna magari ya umma ya kutosha yanayotoa huduma moja kwa moja kama daladala za uhakika. Mara nyingi tunategemea mabasi yanayopita kwenda Mbezi yakitokea Makumbusho au Kawe, lakini hali hiyo imekuwa ikituletea usumbufu mkubwa kutokana na wingi wa abiria.
Ukweli ni kwamba wakazi wa Goba na vitongoji vyake tupo wengi sana kiasi kwamba eneo hili lilipaswa kuwa na kituo kikubwa cha mabasi na huduma maalumu za usafiri. Kuanzia maeneo ya Mbezi, Goba, Madale, Mivumoni, Makabe, Matosa, Tegeta A na baadhi ya wakazi wa Kinzudi, wengi wetu tunategemea barabara kuu ya Goba Road kuelekea kazini na kwenye shughuli zetu za kila siku.
Changamoto kubwa hujitokeza hasa nyakati za asubuhi na jioni. Watu wanakuwa wengi sana, huku mabasi yanayotoka Mbezi yakifika Goba yakiwa tayari yamejaa kiasi kwamba wakati mwingine hakuna hata nafasi ya kusimama ndani ya basi. Hali hii inasababisha wengi wetu kuchelewa kazini na kuathiri majukumu yetu ya kila siku.
Mbali na hilo, tunalazimika kutumia usafiri mwingine kama bajaji au magari ya kukodi ili kufika majumbani. Gharama hizo zimekuwa mzigo mkubwa kwetu. Wakati mwingine bajaji kutoka Makumbusho hadi maeneo ya Goba kama Njia Nne zinatoza bei wanazopanga wao, mara shilingi 4,000 hadi 5,000 hasa wanapoona abiria ni wengi.
Tunaiomba serikali na mamlaka husika kulifanyia kazi suala hili kwa haraka. Tunaomba kuongezwa kwa daladala za uhakika katika eneo la Goba, kuwekwa kwa mfumo mzuri wa usafiri na ikiwezekana kufikiriwa uwepo wa stendi kuu ili kupunguza adha wanayopitia maelfu ya wakazi wa eneo hili.
Usafiri ni huduma muhimu kwa wananchi, na tunatumaini kilio chetu kitafanyiwa kazi ili tuweze kufika kazini na kurudi nyumbani kwa wakati na kwa gharama nafuu.