Summarry nimepata points zifuatazo
Goba faida yake
1. Ni sehemu iliyo connect na maeneo mengi ya mjini (mbeziBeach, makongo & kimara)
2. Ni makazi mapya ( Watu wanaweka mijengo kwelikweli)
3. sehemu nyingi Usalama upo kutokana na aina ya watu walioJenga
4. Ipo connected na maeneo mengi
[emoji3469]Challenge ya Goba
1. Vilima vingi (sio tambare - ujenzi gharama)
2. Sio block ( maeneo mengi hayako planned kimitaa (sio viwanja vya serikali) so hakujapangiliwa - upana wa barabara zimekatwa kienyeji )
3. Maji challenge kidogo
4. goba kunafaa mtu mwenye mishemishe ( MbeziBeach, kimara, makongo , na maeneo jirani)
5. Hakuna beach za karibu
6. Foleni - hasa wanaofanya kazi kutokea posta & kariakoo
7 . Haijitoshelezi kila kitu ( huduma zingine lazima uzifuate mbeziBeach au mwenge n.k
8. Wakati wa mvua zile tope na maporomoko[emoji35]
[emoji3469] [emoji3469][emoji3469][emoji3469][emoji3469][emoji3469][emoji3469]
Kigamboni"
Faida zake
1. Kuna sehemu ni Block (planned) - viwanja vya serikali, barabara zimepangika na hata viwanja nimepangiliwa -- areas kama kisota, kibada & Geza . hayo maeneo pamejengeka sana na watu wapo Good na security ipo juu
2. Kigamboni - ipo na beach ( so weekEnd au kwenda kupumzika is okay
3. Kigamboni ipo karibu na uwanja wa Taifa so relaxation is[emoji91]
4. Kigamboni hakuna Jam ya foleni maana ipo pembeni
5 . Kigamboni imepakana na posta so ukivuka maji tu upo kariakoo na maeneo ya posta
6. Kigamboni cost zakujenga ndogo( tambarale, material yapo karibu sana - hata buguruni chap ushapata mbao & bati)
7. Kigamboni imepakana na ukanda wa viwanda vingi ( so materials & kazi ndogo ndogo ni chap)
8. population ni kubwa ( so huduma nyingi zipo )
10. Ni ukanda wa bahari ( so vyakula fresh ni vingi)
[emoji3469]
Challenge za kigamboni
1. Tozo, Tozo, Tozo[emoji35] za gari /kulipia
2. Maeneo ya block ( Planned - kisota, kibada & Geza n.k ) ni expensive sana compared to squatter area
3. Kigamboni kumejitenga tofauti na goba (goba ni connected na sehemu nyingi)
4. Iko mbali na stend ya mkoa ( kwa wenye usafiri sio issue ila wenzangu na mm hadi ufike stend kipengele)
Conclusion kwa nilivoona
[emoji91] Maeneo yote is okay , itategemea mishe mishe unafanyia wapi...coz mtu wa kazi lugalo hawezi tamani kukaa kigamboni...na mtu wa mishe mishe bandarini hata tamani kujenga Goba