Kiranga
Platinum Member
- Jan 29, 2009
- 78,790
- 128,275
Vipi ww ukiwa mbunifu wa kitu flani ambalo umekichagua kukitengeneza kwa namna flani ambayo mtu flani hakuipenda, je! Itakuondolea sifa ya ww kuwa mbunifu wake na kulpa sifa gar hilo kwamba lilijiunda wenyewe?
Hitaniondolea sifa ya wewe kuwa mbunifu.
Lakini hapa unaonesha huelewi hoja yangu. Sikatai uwepo wa Mungu kwa sababu ulimwengu aliouumba Mungu sijaupenda. Kama Mungu yupo, na kaumba ulimwengu, na ulimwengu huo sijaupenda, mimi kutoupenda ulimwengu huo hakufanyi Mungu huyo asiwepo.
Nakataa uwepo wa Mungu, kwa sababu, ulimwengu tunaouona unapingana na uwezekano wowote wa kuwepo huyo Mungu mnayemsema yupo.
Ni sawa sawa na tuseme kwamba, mtoto A wa miaka 10, hawezi kuwa Baba mzazi wa mwanamme B wa miaka 40 kwa wati huo ambao mtoto A ana miaka 10.
Kwa sababu ili mtoto A (10) huyu aweze kuwa baba mzazi wa mwanamme B (40), inabidi huyu mtoto A awe mkubwa kuliko huyo mwanamme B.
Sasa hapo mtu akija kukuambia kwamba, mtoto A ana mdogo wake C mwenye miaka mitano, na huyu mdogo C mwenye miaka 5 ndiye baba mzazi wa mwanamme B mwenye miaka 40, utakubali?
Mungu hayupo si kwa sababu mimi siupendi ulimwengu alioumba. Hayupo kwa sababu ulimwengu mnaousema kauumba unakanusha uwepo wake kwa contradiction, contradiction sawasawa na kusema mtoto wa miaka mitano ni baba mzazi wa mwanamme mwenye miaka 40. Ukisikia habari yenye contradiction hivyo, moja kwa moja unajua huu hauwezi kuwa ukweli.
Nakingine nataka kujua Kwann ww unaamin tu vitabu vinavyopinga uwepo wa Mungu na si vinavyounga mkono uwepo wake?
Siamini, sitaki kuamini. Nataka kujua. Inaonekana hata ninachoandika huelewi.
Tatu ninyi mnawaitaje watu wanaoamini uwepo wa Mungu Maana Sisi tunawaita wale Wasio amini Ni MAKAFIRI،.
Tunawaita waamini Mungu.
Wewe kuweza kusema neno hilo makafiri ni ushahidi mwingine Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote hayupo, angekuwepo asingeumba ulimwengu ambao watu fulani wanawaita wengine makafiri.
Nne nataka kujua unataka nikuthibtishie vipi kuwa Mungu yupo?
Start by being logically consistent.
Umeoneshwa kazi za ustad wake umekataa,
Kazi gani? Unaweza kuzitaja? Unajuaje hizo kazi ni zake ni si story tu anapakaziwa?
Je! Unataka sikio lake? Je! Unataka kusikia saut yake au unataka umuone kabsa!?
Wapi umelipata hili? Je, hapo ndipo mwisho wa fikra zako?
Na kingne nataka kujua unaitambua vipi historia ya BIBLIA mtu Kama Yesu kwa mtizamo wako unamuonaje!??
Yesu ni mwanafalsafa sawa na kina Socrates, Confucius, etc, kwa nini unauliza hili?
Maana niyeye peke yake alietujuza kwa kina kuhusu Huyu Mungu tunaemzungumzia hapa!!/ mwenye mashabiki wengi .
Yesu kaja miaka 2,000 tu iliyopita, kakuta watu kibao washamtangulia, ukisema ni yeye pekee katujuza kuhusu huyu Mungu tunayemzungumzia hapa unanionesha humjui Yesu wala Mungu yunayemzungumzia hapa.
Naomba unisaidie katka hayo ili tuende sawa
Wewe kuniomba nikusaidie nao ni ushahidi kwamba Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote hayupo.
Angekuwepo, usingeomba nikusaidie.