God existed before time and He created time

Vipi ww ukiwa mbunifu wa kitu flani ambalo umekichagua kukitengeneza kwa namna flani ambayo mtu flani hakuipenda, je! Itakuondolea sifa ya ww kuwa mbunifu wake na kulpa sifa gar hilo kwamba lilijiunda wenyewe?

Hitaniondolea sifa ya wewe kuwa mbunifu.

Lakini hapa unaonesha huelewi hoja yangu. Sikatai uwepo wa Mungu kwa sababu ulimwengu aliouumba Mungu sijaupenda. Kama Mungu yupo, na kaumba ulimwengu, na ulimwengu huo sijaupenda, mimi kutoupenda ulimwengu huo hakufanyi Mungu huyo asiwepo.

Nakataa uwepo wa Mungu, kwa sababu, ulimwengu tunaouona unapingana na uwezekano wowote wa kuwepo huyo Mungu mnayemsema yupo.

Ni sawa sawa na tuseme kwamba, mtoto A wa miaka 10, hawezi kuwa Baba mzazi wa mwanamme B wa miaka 40 kwa wati huo ambao mtoto A ana miaka 10.

Kwa sababu ili mtoto A (10) huyu aweze kuwa baba mzazi wa mwanamme B (40), inabidi huyu mtoto A awe mkubwa kuliko huyo mwanamme B.

Sasa hapo mtu akija kukuambia kwamba, mtoto A ana mdogo wake C mwenye miaka mitano, na huyu mdogo C mwenye miaka 5 ndiye baba mzazi wa mwanamme B mwenye miaka 40, utakubali?

Mungu hayupo si kwa sababu mimi siupendi ulimwengu alioumba. Hayupo kwa sababu ulimwengu mnaousema kauumba unakanusha uwepo wake kwa contradiction, contradiction sawasawa na kusema mtoto wa miaka mitano ni baba mzazi wa mwanamme mwenye miaka 40. Ukisikia habari yenye contradiction hivyo, moja kwa moja unajua huu hauwezi kuwa ukweli.


Nakingine nataka kujua Kwann ww unaamin tu vitabu vinavyopinga uwepo wa Mungu na si vinavyounga mkono uwepo wake?

Siamini, sitaki kuamini. Nataka kujua. Inaonekana hata ninachoandika huelewi.
Tatu ninyi mnawaitaje watu wanaoamini uwepo wa Mungu Maana Sisi tunawaita wale Wasio amini Ni MAKAFIRI،.

Tunawaita waamini Mungu.

Wewe kuweza kusema neno hilo makafiri ni ushahidi mwingine Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote hayupo, angekuwepo asingeumba ulimwengu ambao watu fulani wanawaita wengine makafiri.
Nne nataka kujua unataka nikuthibtishie vipi kuwa Mungu yupo?

Start by being logically consistent.
Umeoneshwa kazi za ustad wake umekataa,

Kazi gani? Unaweza kuzitaja? Unajuaje hizo kazi ni zake ni si story tu anapakaziwa?

Je! Unataka sikio lake? Je! Unataka kusikia saut yake au unataka umuone kabsa!?

Wapi umelipata hili? Je, hapo ndipo mwisho wa fikra zako?

Na kingne nataka kujua unaitambua vipi historia ya BIBLIA mtu Kama Yesu kwa mtizamo wako unamuonaje!??

Yesu ni mwanafalsafa sawa na kina Socrates, Confucius, etc, kwa nini unauliza hili?
Maana niyeye peke yake alietujuza kwa kina kuhusu Huyu Mungu tunaemzungumzia hapa!!/ mwenye mashabiki wengi .

Yesu kaja miaka 2,000 tu iliyopita, kakuta watu kibao washamtangulia, ukisema ni yeye pekee katujuza kuhusu huyu Mungu tunayemzungumzia hapa unanionesha humjui Yesu wala Mungu yunayemzungumzia hapa.

Naomba unisaidie katka hayo ili tuende sawa

Wewe kuniomba nikusaidie nao ni ushahidi kwamba Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote hayupo.

Angekuwepo, usingeomba nikusaidie.
 
Unaweza kuthibitisha Adamu alikuwepo na na si story tu?

Naweza kuthibitisha.
Pili unaposema Story una maanisha nini ?

Ukijibu swali hilo nitaendelea hapa nilipoishia.
 
Naweza kuthibitisha.
Pili unaposema Story una maanisha nini ?

Ukijibu swali hilo nitaendelea hapa nilipoishia.
Story ni hadithi ya kutungwa tu, isiyo na ukweli.

Kama ile proof yako ya 1=2 ya division by zero.

Unaweza kuthibitisha Adam aliwahi kuishi kweli na si hadithi tu?
 
Story ni hadithi ya kutungwa tu, isiyo na ukweli.

Kama ile proof yako ya 1=2 ya division by zero.

Unaweza kuthibitisha Adam aliwahi kuishi kweli na si hadithi tu?

Naona unapenda kukariri makosa sana bro. Hivi unaweza kukubali hadharani kama umekosea endapo ukiwa umekosea kweli kama mimi nilivyofanya ? Hili naliweka kiporo.

Nimekwambia nina uwezo wa kufanya hilo.

Kabla sijakuthibitishia. Nataka twende taratibu. Je masimulizi yasiyo ya kutunga yanaitwaje kwa Kiingereza na kwa Kiswahili pia ?

Hili sasa ni swali mama,umejuaje kama habari za Adamu ni za kutunga ?

Ukishajibu maswali hayo marahisi nakuja kukupa faida juu ya hadithi,masimulizi na elimu ya kuhakiki habari.

Nipo ...
 
Story ni hadithi ya kutungwa tu, isiyo na ukweli.

Kama ile proof yako ya 1=2 ya division by zero.

Unaweza kuthibitisha Adam aliwahi kuishi kweli na si hadithi tu?

Je kila hadithi ni ya kutunga ?

Na utajuaje hii ni hadithi ya kutunga dhidi ya ile ambayo ni kinyume chake. Hili swali nimeliuliza kwenye post # 205, hapa natilia mkazo tu kwa namna hii.....

Nasubiri jibu,ili nikufundishe elimu ya uhakiki wa habari japo kwa uchache mno...
 
Habari inayojipinga yenyewe haiwezi kuwa katika kweli.

Unakubali?
 
Thibitisha Mungu yupo,
 
Habari inayojipinga yenyewe haiwezi kuwa katika kweli.

Unakubali?

Hapa unatakiwa utoe vigezo vya uhakika wa habari,kwako wewe ili habari iwe thabiti na ya kweli inapaswa iwe na vigezo gani au sifa gani ?

Je kujipinga yenyewe ndio kigezo cha kutokusihi habari ?

Je huwezi kutoa hitimisho moja katika maelezo yenye kutofautiana ukapata jibu moja ?
 
Habari inayojipinga yenyewe haiwezi kuwa katika kweli.

Unakubali?

Bado nakudai majibu ya maswali katika post # 205 na 206 ,leo nataka twende kwa mtindo huu ili nikuonyeshe ujinga wako uko wapi.

Nasubiri majibi ya maswali hayo.....

"Ukipenda kujibiwa maswali yako,basi na wewe upende kujibu maswali ya wenzako"

Nipo .....
 
Hata tukisema tukubali kuwa kuna hiyo contradiction,bado inabaki kuwa majibu ya kuwa hakuna Mungu ni madai yako binafsi tu kwa sababu hiyo contradiction haiondoi uwepo wa Mungu.
 
Hapa unatakiwa utoe vigezo vya uhakika wa habari,kwako wewe ili habari iwe thabiti na ya kweli inapaswa iwe na vigezo gani au sifa gani ?

Kwa muktadha gani? Bila muktadha hakuna uthabiti wowote wa chochote kwa sababu uthabiti wa chochote usiowekwa katika muktadha utakuwa na makadirio yasiyothabitika na hivyo uthabiti wenyewe hautakamilika.Umeelewa

Je kujipinga yenyewe ndio kigezo cha kutokusihi habari ?

Habari inayojipinga yenyewe haiwezi kusihi kuwa kweli. Mathalani, kama tukikubaliana kwamba, in a non relativistic time dilation world, mama wa mtoto kamwe hawezi kuwa mdogo kuliko mwanawe wa kumzaa mwenyewe, nikikwambia kwamba leo kuna msichana wa miaka mitano ambaye ni mama mzazi wa mwanamke mwenye miaka 40, habari hii inajipinga yenyewe.

Tumejua mama ni lazima awe mkubwa kuliko mtoto wake ili aweze kumzaa.

Na mtu akikuambia mtoto wa miaka 5 ni mama mzazi wa mwanamke mwenye miaka 40, utaona habari hii inajipinga ukiiweka na ukweli kwamba mama ni lazima awe mkubwa kuliko mtoto.

Kujipinga huku kunaonesha kwamba habari hii ina mushkeli, si ya kweli.

Haiwezi kusihi kiukweli.

Je huwezi kutoa hitimisho moja katika maelezo yenye kutofautiana ukapata jibu moja ?

Hiki ni kitu tofauti.

Unachosema hapa ni kwamba.

Dodoma ni mkoa. Iringa ni mkoa. Mikoa yote ipo Tanzania.

Hili halina kupingana.

Sijaongelea kabisa hilo.

Ninachoongelea mimi ni hiki.

Dodoma ni mkoa ambao upo Tanzania. Mkoa wa Dodoma haupo ndani ya Tanzania.

Hiki hakiwezekani kuwa kweli chote kama kilivyoandikwa, kuna sehemu ina makosa. Haiwezekani mkoa uwe ndani ya Tanzania, halafu hapo hapo usiwe ndani ya Tanzania. Habari hii inajipinga, kujipinga huku kunaonesha habari ina makosa na ni ya uongo. Haiwezekani kuwa kweli kama ilivyoandikwa, kwa sababu kabla mtu mwingine hajaanza kuipinga, habari imeanza kujipinga yenyewe.

Na Mungu wenu habari za uwepo wake zinajipinga hivyo hivyo, kwa contradiction.
 
Hata tukisema tukubali kuwa kuna hiyo contradiction,bado inabaki kuwa majibu ya kuwa hakuna Mungu ni madai yako binafsi tu kwa sababu hiyo contradiction haiondoi uwepo wa Mungu.
Contradiction haiondoi uwepo wa Mungu.

Kwa sababu Mungu hayupo. Kama Mungu hayupo, contradiction haiwezi kuondoa uwepo wa Mungu. Inabidi Mungu awepo ili chochote kiondoe uwepo wake.

Contradiction inaonesha Mungu hayupo.

Ndiyo maana hata wewe huwezi ku prove Mungu yupo.

Kama unabisha, prove Mungu yupo.
 

Bro uhakiki wa habari hauna muktadha yaani hauthiriwi na hali,hapa nazungumzia habari kwa maana yako wewe unaitaja kama Story za kutunga. Hapa unatakiwa utulize kichwa ujibi hilo swali la vigezo. Nikisema uhakiki wa habari ujue tunautafuta ukweli hapo.

Tukiza akili ujibu swali langu la vigezo.

Naendelea ....
 
Ushawahi kusikia kitu kinaitwa Godel's Incompleteness Theorems?

Ushawahi kusikia kitu kinaitwa Hegelian dialectics?

Ushawahi kusikia kitu kinaitwa Heisenberg's Uncertainty Principle?

Ushawahi kusikia kitu kinaitwa Einstein's Theory of Relativity?

Ushawahi kusikia kitu kinaitwa Wave Particle duality?

Unaelewa kwamba vyote hivi vinaeleza kwamba hakuna uhakiki bila muktadha?
 

Hapa katika kujipinga mwenyewe naona unarudia kukosea kama unavyokoseaga kila siku. Kuna siku niliwahi kukwambia una udhaifu mkubwa sana wa kutoa mifano na kulinganisha mambo bila kutumia mizani.

Hapa kuhusu mama na mwana hakuna habari inayojipinga,kwani hii inakubalika na inajulikana wazi ya kuwa kamwe mtoto hawezi kumzidi mama,na hii haiwezi kuwa habari.

Ukishindwa kuleta mfano hili nitakupa mfano wa habri au simulizi mbili tofauti zenye kuleta hitimisho moja.

Hapa tena narudia tena bro,unatakiwa utulize akili sana.

Ndio maana kuna mwanazuoni mmoja alipata kusema hivi "Qur'an na hadithi hazipingani kwa zenyewe na ukiona zinapingana au kuhisi zinapingana basi ituhumu elimu kwa kutofikia uwezo wa kung'amua au ituhumi akili yako kwa kutoelewa maandiko hayo" au kama alivyosema mwanachuoni huyo.

Bro mama kuwa mkubwa kwa mwana huo ndio ukweli,na mwana kuwa mkubwa kwa mama hii sio habari bali huo ni uongo na kamwe uongo hakai pamoja na ukweli.

Hapa pia bado hujajibi hoja yangu. Leta mifano ya kweli tupu.
 


Kaka usilete dibaji na msamiati lukuki,wewe jibu hoja kwa hizo nadharia zako nikuonyeshe wapi unapo yumba. Halafu mimi siongozwi na nadharia mzee,naongozwa na ukweli halisi.

Nasubiri ujibu hoja zangu sio dibaji na kupoteza muda.

Nipo ...
 
Iweje mie ninayebisha ndio niprove na si wewe? Nilitegemea ungesema naweza kuprove kama ukibisha.

Nasema contradiction haiondoi uwepo wa Mungu kwa sababu wewe badala ya kusema kuna contradiction kwenye suala la Mungu mwenye upendo,ujuzi na uwezo wote kuwa ndiye kuumba huu ulimwengu ila wewe unatumia hiyo contradiction kusema hakuna Mungu,hivyo ni sawa na kumuondoa Mungu kwa hiyo contradiction.
 

Nilijua tu hapa lazima uangukie pua,sababu elimu hii huko kwenu hamna. Ndio maana niliacha kuisoma elimu ya mantiki (logic) kwa kushindwa mambo madogo kama haya na kutumia akili ndogo kama hii.

Ukiwa mfuasi wa logic lazima ukubali kuwa mvivu wa kufikiria.

Huo mfano wa mkoa hauingii katika kauli yangu hiyo,huo mfano ni wako wewe kwa kudandia maelezo usiyo yaelewa.

Nakupa muda tena wa kufikiria hicho nilichokwambia. Na kama ukituliza akili na ukaamua kujifunza lazima utaona ajabu ya elimu ya uhakiki wa habari.

Nipo .....
 
Mungu anaweza kuwa na upendo wote halafu akaruhusu uovu uwepo wakati anaweza kuuzuia?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…