Tatizo lenu mnaletaga ushindani na sio kujifunza vitu vipyaMkuu nimesoma comment yako iliyosheeni mambo mengi fikirishi
lakini msimamo wa kila muumini ni uleule MUNGU yupo na mimi naamini hivyo japo najua wewe Ndugu huamini na ni vigumu kuelewana
Mnapotoka sanaHawa wakana mungu walikuwepo zamani,ila hawa tulionao ni wafuasi wa wakana mungu,hii imeshakuwa imani,imani amnayo haikujengeka katika misingi ya kielimu.
Imani iliyojengeka juu ya ujinga,huwezi kupata faida kwayo zaidi ya wafuasi wake kubisha,kupoteza muda na kuzozana.
Wakana mungu,kama ulivyosema hawakuanza leo,na huu ni muendelezo tu,wa watu waliopo gizani ......
Narudi ....
Mnapotoka sana
Hivi unajua kuwa mungu ni idea?Hapa nasema chochote kuhusu hili.
Mola muumba alikuwepo kabla ya chochote kuwepo kabla yake na atakuwep kabla ya chochote kuwepo baada yake.
Suala la muda nilishawahi kujadiliana na mtu mmoja katika jukwaa hili lakini upingaji wake ulikuwa wakitoto na kucekesha sana.
Mola wetu aliumba muda,na Mola wetu ameapa sana kwa muda. Na akatuwekea hali na viumbe wengine ili kuutambua muda,kudhibiti miaka na kudhibiti mahesabu.
Kwa ufupi Mola hajatanguliwa na wakati .....
Nipo ....
Vipi ww ukiwa mbunifu wa kitu flani ambalo umekichagua kukitengeneza kwa namna flani ambayo mtu flani hakuipenda, je! Itakuondolea sifa ya ww kuwa mbunifu wake na kulpa sifa gar hilo kwamba lilijiunda wenyewe?Msimamo mimi sina tatizo nao.
Unaweza kuwa na msimamo kwamba wewe ni Bill Gates, bilionea wa kimarekani.
Nikajua wewe si Bill Gates, nikakuachia tu ukae na ndoto zako, kwa sababu zinakufariji.
Lakini ukienda benki ambayo mimi nina hisa kubwa, ukaanza kuomba mkopo wa mabilioni ya dola, kwa sababu wewe ni Bill Gates, kama fact, hapo tutataka uthibitishe kama kweli wewe ni Bill Gates.
Hii misimamo mbona inatetewa mpaka kikatiba, na hata mimi natetea haki yako ya kuwa na msimamo wako, kama sehemu ya uhuru wa kuabudu.
Sibishani misimamo.
Nabishana fact.
Unaelewa tofauti?
Hata ukienda sehemu ambayo Hakuna BIBLIA wala Qur'an utakuta watu wanafnya ibada na Kuwa na Amri za Mungu NDANI mwao kwahyo kuhusu hilo usitutshe mkuuMungu ni idea iliyotengenezwa na mtu ili ije kuishi kwenye vichwa vyenu. Ndio maana mtu hawezi kujua habari za mungu bila kufundishwa.
Huwezi kunielewa kwakua lile lengo la walioanzisha hiyo idea ya mungu limetimia
Mungu ni idea kama ilivyo idea ya kuweka mipaka, idea ya kuunda herufi, idea ya kuunda namba, idea ya kupeana majina, idea ya kuvaa nguo, idea ya kupika chakula.Nasubiri ulete hoja ....
Wapi huko wankofanya ibada na kuwa na amri za mungu bila biblia wala quran?Hata ukienda sehemu ambayo Hakuna BIBLIA wala Qur'an utakuta watu wanafnya ibada na Kuwa na Amri za Mungu NDANI mwao kwahyo kuhusu hilo usitutshe mkuu
Mimi ni Mkristo, sio mkristo😊wewe ni mkristo au muislam?
umeandika as if unanijua sana kiufupi ni kwamba nazijua hoja zote za pande zote mimi sio kama wale waumini wasiotaka kujifunza hoja pinzaniTatizo lenu mnaletaga ushindani na sio kujifunza vitu vipya
Yaani mnadhani sisi hatujui mnayojua nyie ndio maana labda tupo hivi.
Kwa taarifa yako, mimi nisiyeamini mungu najua mengi kuhusu idea ya mungu kuliko wewe. Maana sijaifungia akili yangu.
Penda kujifunza zaidi ya vile unavyovijua utapata mwanga
Samahani mkuu, mimi naomba tu kueleweshwa kuhusu hili. Je, kama Mbingu na Jehanamu it's just fictional as your claim towards God and Satan, je uganga/ulozi/uchawi/miujiza hizi supernatural forces zinaoriginate from where? Kwa mfano ndugu zangu waislamu wana kitu kinaitwa Albadir ukisomewa hiyo lazima madhara yakufike. Au unafika kwa mganga anakuelezea matatizo yako yote kabla hujatamka lolote. Au vile kwa church wanavo cast out demons/spirits out of people. Nguvu hizi ni za kisayansi au ni za namna gani?kama unaijua biblia na quran vizuri nitakwambia tatizo lao
kuna never resolve consistency/contradictions ambazo zinafanya vile vitabu viwe vichekesho
kwa kubase tu kwenye maandiko yao inatosha kuona kuwa hiyo miungu yao ni uzushi
unajua ingekuwa rahisi kuelezea miungu yao kama wasingeweka kwenye maandishi
maandishi yao ni vituko vitupu (kwa mtu anayevichambua kwa uhuru wa kifikra)
Ungejua hoja za upande wote, usingeweza kuamini habari za uwepo ww Mungu maana ni uongo mtupu. Na hazina uhalisia kabisa zaidi ya kutumia vitisho ambavyo watu huanza kufundishwa tangu wakiwa wadogo ili imani iwakae zaidi.umeandika as if unanijua sana kiufupi ni kwamba nazijua hoja zote za pande zote mimi sio kama wale waumini wasiotaka kujifunza hoja pinzani
siku nyingine uwe unauliza kwanza
kuna waislam wanaijua bible yote na kuna wakristo wanaijua quran yote hii haimfanyi mtu kuacha dini yake kisa ana maarifa ya dini nyingineUngejua hoja za upande wote, usingeweza kuamini habari za uwepo ww Mungu maana ni uongo mtupu. Na hazina uhalisia kabisa zaidi ya kutumia vitisho ambavyo watu huanza kufundishwa tangu wakiwa wadogo ili imani iwakae zaidi.
Hata kwa akili ndogo tu. Hamjiulizi inakuaje kumuona huyo mungu mpaka ufe?
Yaani waliokua na idea hiyo ya mungu, hapo ndo waliweka mtego. Walijua kabisa umuhimu wa maisha yako upo ukiwa hai ndio maana wakaharibu ubongo wako ili wakutawale vizuri. Maana wanajua ukisha kufa, hutaweza kuamka na kuhoji kuhusu kuto kumuona huyo mungu ambaye umekua ukimsikia tangia utotoni.
Shtukeni
Lazima ufundishwe ili uchague kuamini au kutokuamini,maana jambo lenyewe ni la imani.Mungu ni idea iliyotengenezwa na mtu ili ije kuishi kwenye vichwa vyenu. Ndio maana mtu hawezi kujua habari za mungu bila kufundishwa.
Huwezi kunielewa kwakua lile lengo la walioanzisha hiyo idea ya mungu limetimia
Duh!na elimu ELIMU hapo inachukua nafasi gani?Mungu ni idea kama ilivyo idea ya kuweka mipaka, idea ya kuunda herufi, idea ya kuunda namba, idea ya kupeana majina, idea ya kuvaa nguo, idea ya kupika chakula.
Na ili uamini uwepo wa mungu ni lazima ufundishwe. Kitu chochote ambacho ni idea huenda sambamba na mafundisho. Ni tofauti na vitu ambavyo vipo by nature. Kwa mfano mtoto kulia pindi tu azaliwapo. Au mtoto kusema da da da da da
Habarini wa GT.
Kumekuwa na mgongano wa mawazo kuhusu uwepo na ithibati ya Mungu.Naomba niseme ya kuwa mgongano huu haujaanza leo wala jana bali ni karne kwa karne zimeshapita. Nitaanza kwa kusimulia visa kadhaa kabla ya kujenga hoja.
Mwanafalsafa Plutarch(myunani) aliyekufa mwaka 120b.c na mwandishi wa habari za wayunani na warumi katika kitabu chake kinachoitwa "Parallel lives of illustrious Greek and Romans"aliandika ya kuwa Kuna miji isiyo na kuta, wala vitabu isiyo na mfalme, wala nyumba wala hazina wala mahala pa kuchezea michezo; Lakini hakuna mji usiokuwa na hekalu la Mungu(mungu fulani) hakuna mji huo na hutapata kuuona.
Mwana sayansi wa elimu ya viumbe Athanasius Kirchner(1601-1680) alikuwa na rafiki yake ambaye alikuwa anapinga uwepo wa Mungu. Kuna siku huyu rafiki alimtembelea Kirchner, Alikuta Kirchner ameshika tufe lenye sura ya dunia, kutokana na ustadi uliotumika kulifanya tufe hilo Jamaa akamuliza Kirchner"Nani aliyeufanya mfano wa dunia hivi? Kirchner akajibu Hakuna mtu, umejifanya wenyewe.Jamaa akasema acha kunichekesha aliyeufanya mfano huu lazima awe mstadi mkubwa, Jinsi gani Kirchner akahoji? Hutaki kukubali ya kuwa mfano huu dhaifu wa tufe la dunia umejifanya wenyewe lakini unakazana kuwa dunia hii kubwa (universe) umejifanya wenyewe.
Kuna watu wa aina bado wapo.
WHAT'S INVISIBLE THAT CREATES WHAT'S VISIBLE.
Kama kitu hakithibitishiki kwa milango ya fahamu (pua,ulimi, macho, ngozi,masikio) haifanyi kitu hicho kisiwepo.Kuna ya vitu hauwezi kuthibitisha kupitia milango ya fahamu lakini vipo katika mazingira yetu.Ili kuthibitisha uwepo wa mambo/vitu hivyo tuna angalia athari yake (Low of course and effect)Hapa nitaweka baadhi vitu/mambo hayo ili kuelewa vizuri low hii.
These facts are not all of one kind, some are material and some are non material. We shall mention here a few of them.
Electricity, Gravitation, Magnetism, Invisible radiation, Intelligence, Love, Hate, Determination. and so on.......
Hivi ni baadhi ya vitu/mambo hatuwezi kuthibitisha kwa milango yetu ya fahamu lakini vipo, Tunamini vipo kwasababu ya athari zake.
Kwa hiyo; hoja ya kuwa Mungu hayupo kwa kuwa hatuwezi kumthibitisha kwa milango yetu ya fahamu inakufa/haina uhai kwa scenario hii.
Mungu hujibainisha kwa viumbe wake kupitia alama/sign mbalimbali rejea paragraph za juu hapo(matukio hayo mawili).
Karibuni
Mkuu,
Kuna Post nimeitoa hapo juu kuchangia swami la Da Hustla ningependa nichangie katika point pale kuwa sifa mojawapo ya Mungu Muumba ni kuwa lazima ajidhihirishe katika hoja za kiakili, kisayansi na kiroho.
Sasa hebu fuatilia Post yangu hii kisha uone kuwa zao la Mungu muumba sio zao la mawazo yaliyopo kichwani mwa mtu bali uhalisia kutegemeana na Mungu yupi unayemuabudu.
Natanguliza kujenga hoja kwa aya ndani ya Qur'an kisha nitoe maelezo kwa ufupi.
Mungu anasema katika Surat At-Talaaq aya ya 12.
"Mwenyezi Mungu nu yule ambaye amezuimba mbingu Saba, na Ardhi kwa mfano wa hizo. Amir zake zinashuka baina Yao, ili mjue kwamba Mwenyezi Mungu ni mwenye uweza juu ya kila kitu, na kwamba mwenyezi mungu amekizunguka kila kitu kukijua vilivyo kwa elimu yake. (quran 65:12)
Ufafanuzi:
Hapo tumeambiwa Mungu kaumba mbingu saba. Kuna tafsiri mbili hapa na mimi nitatoa moja tu.
Mbingu saba kwa matabaka (Atmosperic layers)
1. Troposphere
2. Stratosphere
3. Ozone Layer
4. Mesosphere
5. Ionosphere
6.Thermosphere
7. Exosphere
Hizo ni major spheres ingawa wanasayansi wamejaribu kuzi-subdivide kama stratopause au tropopause, belts ,nk
Ndani ya hizo layers kuna amri nyingi sana (Commands) kama upepo (kuvuma au kutulia), kupwa na kujaa kwa bahari, kimbunga, photosynthesis, mvua (formation of rains), joto, baridi, Masika, kiangazi, radi, mawingu ya kawaida au ya mvua, mawingu kwenda kasi au kawaida,nk. Na hiyo ni katika Troposphere tu. sijakwambia Ozone layer, repulsion of meteors, x-rays, gamma rays. Nasi humo katika layers tunapata manufaa makubwa sana ya kurusha satellites, kupata mawimbi ya sauti, Simu, radio, TVs, rockets zinapita nk.
Aya inasema; "Na ameumba Ardhi kwa mfano wa hizo (Mbingu Saba)":
Hebu nazo tuzione kama kweli zipo saba.
core.
1. Inner Core (Solid)
2. Outer core (Liquid)
Mantle
3. Methosphere
4. Esthenosphere
5. Lisosphere
Crust
6. Continental crust
7. Oceanic crust
Sijakwambia Amri zinazotoka humo pia kama kupwa na kujaa kwa bahari, aina mbalimbali za udongo, miamba,uoto mbalimbali, madini, maji ya visima, ladha za maji mbalimbali, volcano, landsildes, nk, nk, nk
hizo zote ni amri zinazotoka kwa Allah Muumba. Nasi tunapata faida kubwa sana humo na Maisha yanaenda.
Na katika hali zote hizo hakuna mwanasayansi aliyetengeneza au kuumba na wala hawezi kubadilisha chochote Zaidi ya kukielezea tu. Cause and effect remain to al-Mighty God and leaves scientists to explain.
Sasa vyovyote watakavyoelezea, wakipatia sawa, wakikosea Mungu kishasema na kufanya. Naye ndiye aliekizunguka kila kitu kwa Elimu (Ujuzi) yake.
Conclusion: Mungu kasema kafanya, na akasema Kuna amri. Mengi tunayashuhudia na mengine sayansi imethibitisha, akili pia imekubali. Kilichobaki hapa ni roho kuitikia wito kuwa kweli aliyeyafanya haya si mwingine ila ni Mungu Muumba mwenye uwezo wa kufanya, kutoa amri na kuvilinda.
Kwa hiyo wazo la Mungu Muumba au Mwenyezi Mungu sio zao la akili au mawazo. Labda unaongelea neno Mungu kwa tafsiri ya wingi wa miungu.
Kama hizo hadithi walihadithiana watu wa kale iweje hadi leo bado zinasimuliwa? Je,tatizo ni kuwa hadithi za kale au hadithi yenyewe ndio sababu ya kuendelea kuwepo hadi leo?