Kiranga
Platinum Member
- Jan 29, 2009
- 78,790
- 128,275
Kwanza thibitisha Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote yupo.Nacheka sana,bro unajua ya kuwa mamno ambayo mimi nafanya kimijadala na kielimu wewe huwezi kufanya ?
Hivi wewe unaweza kukiri kukosea hadharani kwamba kweli umekosea ? Hili si la msingi nimekupa tu kama chachu mzee. Kwangu mimi hilo limeshapita na wala halibadilishi chochote katika mimi na hoja zangu.
Najua nakudai maswali yangu kadhaa,nasubiri majibu mzee. Nyinyi huwa nawaambia laiti kama mngekuwa mnajibu maswali tunayowaukiza humj msingesalia kwa lolote,sababu hoja hamna,misingi ya kumithilisha mambo ndio hamjiwezi kabisa.
Hujajibu maswali yangu ya post # 205 na 206, kadhalika nilikuuliza. Je imani bila elimu ina weza kuwa imani na kusimama ? Swali hili hujajibu mzee.
Sasa kama umeamua kupoteza muda kwa jambo ambalo nilikiri kukosea,hapa unaleta utoto mzee.
Kukiri kukosea ni ushujaa na ni katika adabu za kielimu. Au unataka suala la kukosea kwangu liwe mada nini bro ? Iweke tu iwe mada kisha tuijadili kielimu,naimani utafaidika. Humu bro hatushindani wala hatutafuti ukubwa kwahiyo kukiri kukosea kwa jambo nililokosea ndio kumenifanya mimi Zurri kuwa hapa na kujifunza mengi katika elimu miongoni mwa yale nisiyoyajua.
Nipo ....
Nimekutaka uthibigishe huki awali kabisa. Umeshindwa.
Kwa sababu huwezi kuthibitisha.
Kwa nini umeshindwa kuthibutisha?
Kwa sababu Mungu huyo hayupo.
Kwa nini hayupo?
Kwa sababu dhana ya kuwepo kwake inajupinga yenyewe. Ni sawa na useme kuna Mama A ana mtoto wa kumzaa B. Halafu huyo mtoto B pia ni mama mzazi wa mama A.
Ukiambiwa tu hiyo habari unajua ni uongo.
Haiwezekani kuwa kweli.
Kwa sababu inajipinga yenyewe. Mtoto hawezi kuwa mama wa mama yake mzazi.
Kama unabisha unasema Mungu yupo, thibitisha.