Uchaguzi 2020 Godbless Lema achukua fomu ya kugombea ubunge wa Jimbo la Arusha Mjini kupitia Wakala wake

Hii ni dharau kubwa sana kwa wanaarusha. Inaonyesha ni namna gani mwakilishi huyu ambavyo hayupo serious na kazi anayoomba au hajiamini. Dharau hizi zilianza kwa Lissu nasasa Lema anaziendeleza.
 
Ameshindwa kabla ya muda...Pale Arusha Mjini kwa Sasa Ni Kijani tupu kila Kona...Lema Arudie Kazi yake ya zamani ya kuiba Madini....Loliondo
Atapigwa asubuhi tu
 
Leo Lema kaingia mitini antenna imenusa zomea zomea akaona ohh isiwe nongwa
Kama vile CCM ilivyoona noma kwenda kupandisha zile bendera zake pale Dodoma ikaona iwatumie wale wafungwa la sivyo wangezomewa hatari
 
Aliyekuwa Mbunge wa jimbo la Arusha Mjini (Chadema),Godbless Lema ametangaza nia ya kugombea nafasi ya ubunge ndani ya chama hicho baada ya kuchukua fomu makao makuu ya chama hicho na kuahidi ushindi was kishindo.

Akikabidhi fomu hiyo kwa mke wa Lema,Neema Lema baada ya Lema kuwa safarini, katibu wa chadema wilaya ya Arusha ,Mosses Nanyaro alisema kuwa chama hicho kimejipanga kutoa mgombea aliyebora ili kulirejesha jimbo hilo kwa kishindo kwa kuwa anaamini bado chadema inakubalika Arusha Mjini.

Nanyaro alisema kuwa utaratibu wa chama hicho katika nafasi ya ubunge ni kuwa na wagombea wapatao watano watakaotia nia ila hadi sasa waliojitokeza ni wanne akiwemo Lema aliyeamua kujitangaza huku wengine majina yao yakibaki siri.

Akiongea kwa niaba ya Lema ,Neema alisema kuwa ameamua yeye na watoto wake kumchukulia fomu mume wake kwa kuwa familia inaunga mkono jitihada zake za kisiasa .

"Ninauhakika iwapo chama kitampitisha Lema, chadema itashinda ubunge Arusha mjini asubuhi na mapema ,kwani mambo yaliyofanywa na baraza la madiwani wa chadema katika jiji la Arusha ni kielelezo tosha cha ushindi" Alisema Neema.

 
Arusha jiji la wana mabadiliko kamanda Lema atapita asubuhi mapema. CCM ni maporini kwa wajinga ndio wanapeta.
Hana chake arudi akafanye ile kazi yake
Sioni vizuri huyo aliyeshika fomu ni mwanaume au mwanake simwelewi mwelewi
 
Kaogopa kuzomewa mitaani.Arusha leo ingerindima kwa zomea zomea
we huijui Arusha, kama ni hivyo usemavyo basi Jafo asingefukuza mtu. Kwa Jafo hakukuwa na mtu na Lema akajua lazima watu wangeandamana kwake hivyo kuepusha shali katumia wakala.
 
Wagombea wa CCM Arusha, pamoja na dola wasitarajie mteremko wamuulize RPC wa Wakati ule 2010, Basilio Matei anaujua mziki wa wanaarusha.
 
Bila pilisi na NEC ccm ni sawa na tlp tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…