Godbless Lema amesema Katiba mpya haitsaidia bila mabadiliko ya fikra

Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Godbless Lema, amewataka Watanzania na vijana wanaoikimbilia Katiba Mpya kutambua kuwa mabadiliko ya sheria mama hayatakuwa na tija kama jamii haitabadilika kiutendaji, kiimani na katika kulinda utu wa binadamu.

Akihutubia wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika leo Oktoba 20, 2026 wilayani Karatu mkoani Arusha, Lema amesisitiza kuwa wananchi hawapaswi kutarajia katiba pekee iondoe uoga na kutojali pale haki za wenzao au ndugu zao zinapokiukwa.

Akifafanua kuhusu Katiba Mpya, Lema amesema, “Sasa hii hali mbaya kila mtu anaongea katiba mpya. Nawaambia mimi katiba mpya haitakuwa na maana kama wewe hautabadilisha fikra na uwe na tabia mpya kuhusu maisha yako".

Katika mkutano huo, Lema pia amezungumzia uhusiano kati ya Jeshi la Polisi na raia, akibainisha kuwa mfumo na wanasiasa wametengeneza chuki kati ya raia na askari wa usalama waliokula kiapo cha kulinda amani. Amesisitiza kuwa msimamo wa CHADEMA unabaki kuwa kutolipa ubaya kwa ubaya.

"Sisi hatuwezi kulipa ubaya kwa ubaya... Tukifikiri kama wao tukatenda kama wao maanake ni kwamba wanachokifanya sasa ni sahihi. Tunawaambia wanachokifanya sasa siyo sahihi ndio sababu tumechagua kuwa wapinzani tubadilishe namna watu wanavyofikiri na wafikiri kwa upendo na siyo kwa chuki na mauaji", ameeleza Lema.

Aidha, amekosoa vikali mtazamo wa kuchukulia biashara ya bodaboda na bajaji kama ajira rasmi za kuwakomboa vijana kutoka kwenye umaskini, akitaja hatua hizo kama mbinu za kuwakandamiza zaidi.

Lema amesema kugawa pikipiki chache kwa kundi la vijana sio kuwainua kiuchumi bali ni kuendeleza mzunguko wa umaskini, huku akitolea mfano mgomo na maandamano ya madereva wa bajaji yaliyotokea jijini Mbeya kama ishara ya ugumu wa maisha.

"Nilisema hizi bajaji na hizi boda boda siyo ajira. Mnawakusanya huko vijana wanakutana kwa sababu ya ugumu wa maisha. Serikali lazima iwe na ubunifu wa kutosha kuwatoa vijana kwenye umaskini. Mbunge ananunua pikipiki anaita kundi la vijana anawapa pikipiki tano au 10... Pikipiki 10 kwa vijana 20 siyo kuinua vijana ni kuwafanya vijana kuwa maskini", ameeleza Lema.

Chanzo: Jambo tv

Hajasema katiba mpya sio muhimu sasa point yako ni nini hasa
 
  • Thanks
Reactions: Lax
katiba ni kijitabu ,watu wanaapa kwa vitabu vya dini ila bado wanafanya ujinga sembuse hiko kijitabu.
 
Useful dictatorship ,hata wewe ukiwa Rais (Panapo majaliwa ndoto zako zikitimia) najua utapiga sana shaba wajinga wanaotetea wanyonyaji😂
Huu uhuru mdogo wa kuchangia jamiiforum ukiwa rwanda huwezi upata inshort jamiiforum ingekuwa rwanda ingeshafungiwa kibabe mda sana

Nigeria ndo nchi imetoa madikteta wengi ila angalia jinsi ilivyo

Miaka ya 1970's almost nchi zote za afrika zilikuwa na udikteta ila umaskin haukoondoka
 
Hawakuwa wanajielewa
 
Yupo sahihi. Watanzania tu watu wa ajabu sana. Kwa mfano mtu anatangaziwa kbs ndani ya bus kuwa choo cha ndani ya bus ni kwaajili ya haja ndogo tu, lakini mtu mzima kbs anaingia anakunya na anaacha mavi yake anavaa anatoka zake. Huyu hata umpe katiba mpya haiwezi kumsaidia kwa namna yyt ile.
Fikra mpya ni budi iwe ndani ya mfumo mpya. mindset evolving and protected by new reforms and systems
 
Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Godbless Lema, amewataka Watanzania na vijana wanaoikimbilia Katiba Mpya kutambua kuwa mabadiliko ya sheria mama hayatakuwa na tija kama jamii haitabadilika kiutendaji, kiimani na katika kulinda utu wa binadamu.

Akihutubia wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika leo Oktoba 20, 2026 wilayani Karatu mkoani Arusha, Lema amesisitiza kuwa wananchi hawapaswi kutarajia katiba pekee iondoe uoga na kutojali pale haki za wenzao au ndugu zao zinapokiukwa.

Akifafanua kuhusu Katiba Mpya, Lema amesema, “Sasa hii hali mbaya kila mtu anaongea katiba mpya. Nawaambia mimi katiba mpya haitakuwa na maana kama wewe hautabadilisha fikra na uwe na tabia mpya kuhusu maisha yako".

Katika mkutano huo, Lema pia amezungumzia uhusiano kati ya Jeshi la Polisi na raia, akibainisha kuwa mfumo na wanasiasa wametengeneza chuki kati ya raia na askari wa usalama waliokula kiapo cha kulinda amani. Amesisitiza kuwa msimamo wa CHADEMA unabaki kuwa kutolipa ubaya kwa ubaya.

"Sisi hatuwezi kulipa ubaya kwa ubaya... Tukifikiri kama wao tukatenda kama wao maanake ni kwamba wanachokifanya sasa ni sahihi. Tunawaambia wanachokifanya sasa siyo sahihi ndio sababu tumechagua kuwa wapinzani tubadilishe namna watu wanavyofikiri na wafikiri kwa upendo na siyo kwa chuki na mauaji", ameeleza Lema.

Aidha, amekosoa vikali mtazamo wa kuchukulia biashara ya bodaboda na bajaji kama ajira rasmi za kuwakomboa vijana kutoka kwenye umaskini, akitaja hatua hizo kama mbinu za kuwakandamiza zaidi.

Lema amesema kugawa pikipiki chache kwa kundi la vijana sio kuwainua kiuchumi bali ni kuendeleza mzunguko wa umaskini, huku akitolea mfano mgomo na maandamano ya madereva wa bajaji yaliyotokea jijini Mbeya kama ishara ya ugumu wa maisha.

"Nilisema hizi bajaji na hizi boda boda siyo ajira. Mnawakusanya huko vijana wanakutana kwa sababu ya ugumu wa maisha. Serikali lazima iwe na ubunifu wa kutosha kuwatoa vijana kwenye umaskini. Mbunge ananunua pikipiki anaita kundi la vijana anawapa pikipiki tano au 10... Pikipiki 10 kwa vijana 20 siyo kuinua vijana ni kuwafanya vijana kuwa maskini", ameeleza Lema.

Chanzo: Jambo tv
Eti Katiba mpya haitasaidia kitu mpaka watu wabadilishe fikra zao kwanza 🤣🤣😁 !
Yaani anawataka akina nani wabadilishe fikra zao kwanza ?
Walioshika kwenye makali ?! Au walioshika mpini ?! 🤣🤣 !

Kweli Ukistaajabu ya mussa utayaona ya Firauni !
 
Huu uhuru mdogo wa kuchangia jamiiforum ukiwa rwanda huwezi upata inshort jamiiforum ingekuwa rwanda ingeshafungiwa kibabe mda sana

Nigeria ndo nchi imetoa madikteta wengi ila angalia jinsi ilivyo

Miaka ya 1970's almost nchi zote za afrika zilikuwa na udikteta ila umaskin haukoondoka
Tofauti kati ya Dikteta na Dikteta muadilifu ni huu mfano :-
Baba pale nyumbani ni Dikteta fulani hivi kwa tabia na sheria zake !
Lakini yeye ni Dikteta muadilifu kwa sababu kubwa moja anasimamia nidhamu na hataki shida yeyote iipate familia yake 😳 !
 
LEMA YUPO SAHIHI KABISA.KATIBA km hatujabadili fikra zetu tutaona km kijitabu tu cha riwaya.
Fikra zitalazimishwa kubadilika kwa sheria kali zitakazoletwa na hiyo Katiba !
Sheria kali katika kudhibiti mali za Nchi kama ilivyo China 🇨🇳 ni lazima wakora watabadili fikra !

Lakini ukingoja wabadilike bila kuwepo zile Sheria kali kama za China , Utangoja sana tena sana 😳 !
 
Back
Top Bottom