Godbless Lema amuomba Rais Samia kuchunguza kupotea kwa Ben Saanane na kushambuliwa kwa Tundu Lissu

Naona kiki ya Sabaya imekosa mvuto sasa wanaanzisha mpya!
Unaitaje kick wakati kweli Ben saanane hajulikani alipo mpaka saa hizi, unasemaje kick wakati walio mpiga Risasi Tundu hawajulikani mpaka saa hizi. unaonekana unajua kuandika na kusoma lkn huelewi kitu chochote kichwani mwako.
 
Asante sana my dear cocastic kwa kuwakumbusha hawa watu. Sijui huwa wanajiondoa ufahamu au hawana kumbukumbu sahihi?
Madam SSH alikuwa sehemu ya Serikali wakati hayo yote yakitokea, hivi kweli Lema anafikiri Madam SSH atajikaanga kwa mafuta yake mwenyewe??
 
Hivi ktk ukoo wenu kuna mtu mwenye akili timamu kweli?
Huwa mkiandika huku wote ni ujinga tu, naona ni ule ulevi wenu uliopindukia au laana flani hivi ktk ukoo.
Shida yako ni moja tu!..

Kupenda kusikia unachopenda kusikia tu basi!
 
Kwani wewe inakuuma nn mama akichunguza hayo mauaji ya kinyama na kupigwa risasi kwa mh.lisu au wewe unahusika?
 
Kuna watu wanabeza ombi la Lema na kulifanya kisiasa.

Iko hivi, Kuna siku mwanafamilia yako atapotea Kama Ben Saanane, atapigwa Risasi Kama Lissu, atapotezwa Kama Azory na utahangaika pasipo majibu, utalia pasiwe na wa kukufuata machozi.

Utafuatilia kwenye kila taasisi hutapewa ushirikiano uliotegemea. Utatamani kukaa matanga lakini utasema je akiwa bado yu hai itakuaje.

Hivyo kabla ya kubeza kuweka siasa jiulize hili linamanufaa kwa umma?

Pili tutambue mojawapo ya kazi ya serikali ni kulinda raia wake na Mali zao popote walipo hata nje ya mipaka. Sasa anapotokea kapotea mtu au kuuwawa pasipo kujulikana lazima serikali ichunguze na kuwakamata wahusika.

Sasa kupotea kwa Ben na Azory Kuna Mambo mengi yamesemwa, kupigwa kwa Lissu Risasi Kuna mengi yamesemwa. Familia zao zinataka majibu na watanzania tunataka majibu.

Kuna waliokotwa beach na mtoni watanzania wanataka majibu wale ni kina Nani na waliuwawa na kina Nani?

Watanzania wengi wamepotea hasa huko Rufiji na Mkuranga watanzania wanataka kujua walipo.

Lakini pia Kuna watu walitekwa Mohomed Dewj, Roma na wengine watanzania wanataka majibu kina Nani walikua wanafanya utekaji ule? Je wameshadhibitiwa?

Vijana wa CCM na all pro CCM, Kuna wengi mlikua mnamshabikia Sabaya na kusema alikua anamshughulikia Mbowe, kumbe alikua anafanya yaliyo kinyume na kiapo chake Sasa hivi mnamkimbia.
 
Siro wkt anahojiwa na middle kipindi cha dk 45 alichomekewa swali la kupotea kwa saa8 na risasi za lisu akabaki anachekacheka tu.
 
Yaan hata mwenyewe nashangaa wamesahau mara hii, wakati miezi michache iliyopita SSH alitema cheche kuhus jambo hilo tena wazi kabisa, sasa sijui SSH yule na wa sasa ni tofauti, hata sielew mweeeeh.
 
Pia ametoa dondoo za mahali pa kuanzia , ambapo aliyekuwa RPC wa Dodoma Murroto , Mbunge wa CCM Alexander Mnyeti , Paulo Makonda na Askofu Gwajima wametajwa kuweza kusaidia uchunguzi

View attachment 1806775
huyu mbona ameanza kujijambia huko aliko? si arudi atoe ushahidi sasa? mbona mbowe haulizwi kuhusu ben? aukwakuwa kawalogamnamtukuza kama ndiye aliye waumba? lema ukweli anaujuwa ila anapotosha uma kamata mbowe rudisha lissu watoe ushahidi
 
Maza alizinguaga sana
 
Ukivivaa viatu vya wazazi wa Ben Saanane pamoja na ndugu zake hii kitu inauma sana.
Hiv mtu anayemtukana kiongozi wa nchi si anakua tayar ameshajiandaa kwa lolote ama?...hata wazaz huwa wanawakanya watoto wao..wazaz huwa wanajua huyu mtoto wetu anahatarisha maisha yake hata mkewe anakua anafaham hilo.so huwa wanajiandaa kwa lolote..si gafla tu..so nauhakika..wazaz walijiandaa kwa lolote...kwahyo ukivaa viatu vyao ni inakua kama hvyo..walijua mwisho si mzur.....hii ni africa..huwez tukana tu watu wanakuangalia..tatzo mnajisahau sana kufikir mko ulaya au marekani kwenye uhuru huo...hapa ni africa jaman..huwez tus watu ..hata mtaan huwez tukana watu hovyo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…