Godbless Lema amuomba Rais Samia kuchunguza kupotea kwa Ben Saanane na kushambuliwa kwa Tundu Lissu

Godbless Lema amuomba Rais Samia kuchunguza kupotea kwa Ben Saanane na kushambuliwa kwa Tundu Lissu

Halafu chadema ni wanafiki Sana wanazungumzia kuhusu Ben 8 lakini hawasemi kuhusu Chacha Wangwe

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
Aliyeshitakiwa kwa kifo cha Wangwe ni dereva wake aliyeitwa Deus Mallya , akafungwa jela lakini baada ya muda mfupi sana AKAACHIWA KWA MSAMAHA WA RAIS , hebu jiongeze mwenyewe
 
acha papara uchunguzi umeshaanza ila shahidi muhimu aliyeshuhudia tukio amefichwa hivi hebu tumia tu akili ndogo hata ya kuvukia barabara kwanini wanamficha dreva ambaye aliona tukio zima kwanini asihojiwe ili upelelezi uendelee? kuna sababu dreva anajuwa

Uganda Waziri kapigwa risasi ,museven cha kwanza ni kwenda kuangalia CCTV camera na wameshapna tukio lilivyofanyika kwa cctv footage ,sasa kwanini nyie mling'oa cctv? kwanini msingeanzia hapo? Tukio zima lilikuwa recorded kwenye camera.
 
Tunataka kujua taarifa ya kifo cha Magufuli kina Tundu Lissu na huyu lema walikuwaga wanazipatia wapi kabla hatujatangaziwa? Na huyu lema aliwahi kutabiri kifo cha JPM tulitaka ahojiwe vizuri atakuwa anajua chanzo cha kifo chake.
Madaktari wenu walisema aliugua nini? Hamuwaamini?

Sent from my G80 using JamiiForums mobile app
 
Wakati huyo Ben Saanane anapotezwa katika mazingira ya kutatanisha na huyo Tundu Lissu anapigwa marisasi, huyu Madam SSH yeye alikuwa nani??
Kesi ya Nyani mnataka Ngedere awe hakimu??

..ni kweli alikuwa ccm na bado ni mwanaccm.

..Je, Mama Samia alikuwa anaunga mkono unyama uliokuwa ukifanywa kwa niaba ya chama chake?

..lingine ni kama Mama Samia yuko tayari kuwatendea HAKI wote walioumizwa na utawala uliopita.
 
mbowe mafia ni wewe tu ndiyo humjui wenzio wana mjua vizuri sana

..mnaotaka Mbowe achunguzwe kuhusu kifo cha Chacha Wangwe hamjazuiwa kuomba msaada wa serikali.

..na nyinyi msiwazuie wale wanaoomba serikali ichunguze kupotea kwa Ben Saanane, kutekwa kwa Roma Mkatoliki na wenzake, kushambuliwa kwa Tundu Lissu, na kuuwawa kwa Aquilina.
 
Gazeti la Mwanahalisi lilimtaja wazi kabisa!
Tatizo wabongo sie hamna lolote linaloweza kufanyika zaidi ya kupata umbea tu na kuishia kuupiga mitandaoni kisha basi....tunasubiria iibuke breaking news nyingine.

Kwa Dr ulimboka watekaji waliwekwa hadharani majina hadi namba zao za simu, kina ighondu msangi kwani leo wako wapi??

Hata leo tukiambiwa muuaji ni fulani hakuna kitu chochote atafanywa....makonda yupo mtaani anapeta tu ndio kwanzaa kitambi na makalio vimeongezeka.
Tanzania kweli ni kisiwa cha amani.
 
Wakati huyo Ben Saanane anapotezwa katika mazingira ya kutatanisha na huyo Tundu Lissu anapigwa marisasi, huyu Madam SSH yeye alikuwa nani??
Kesi ya Nyani mnataka Ngedere awe hakimu??
Alikua makamu ila sio yote alishirikishwa, chezea mwendazake, sijui uko aliko kipi kinaendelea katika kuwaongoza malaika,cheo alichokita sana
 
Pia ametoa dondoo za mahali pa kuanzia, ambapo aliyekuwa RPC wa Dodoma Murroto, Mbunge wa CCM Alexander Mnyeti, Paulo Makonda na Askofu Gwajima wametajwa kuweza kusaidia uchunguzi.

Sio hao tu hata kifo cha jiwe kichunguzwe wengi bado hatuelewi hasa undani wa kifo chake. Pamoja na udhalimu wote naye ni binadamu anahaki ya kuchunguzwa aliondokaje?
 
Kwanini Lema amemtaja Gwajima kwenye uchafu huu ?
 
Back
Top Bottom