Godbless Lema anatukumbusha kuwa ukipata uongozi, kuwa makini na wale wanaoamini walikusaidia kuupata

Keynez

JF-Expert Member
Joined
Feb 12, 2007
Posts
3,809
Reaction score
6,948
John Magufuli baada tu ya kupata urais, alimtupa mbali rafiki yake Charles Kitwanga aliyekuwa amempa uwaziri baada ya kusemekana kuongea bungeni akiwa bwiii. George W. Bush alivyopata tu Urais, alijitenga na rafiki yake wa karibu (jina nimelisahau) aliyekuwa amempa nafasi ya uongozi. Barack Obama alipata shida sana kutokana na kauli za Reverend Wright, mchungaji na kiongozi wake wa kiroho wa muda mrefu ikabidi ajitenge naye na kauli zake. Ditopile Mzuzuri alimuua mtu kwa bastola dereva wa daladala barabarani mchana kweupe na rafiki yake wa karibu Jakaya Kikwete akiwa Rais akafumba macho, hakuweza hata kumsaidia katika skendo yake.

Mifano ni mingi ya watu ambao walifanya madudu baada tu ya rafiki zao kupata Urais na moja ya sababu ni kudhani kuwa ushikaji wenu wa kitambo unakufanya uweze kummudu au kwamba unaweza kutofautiana naye hadharani, au kufanya madudu mengine na yeye atakukingia kifua.

Kwa jinsi Tundu Lissu alivyoingia madarakani ndani ya CHADEMA, ni wazi Godbless Lema anaamini kuwa bila yeye Lissu na Heche wasingepata huo uongozi. Bado anajiona yeye ndiyo "Kingmaker" na kwamba uongozi wao unategemea huruma na sauti yake. Hii ni hatari sana kwa CHADEMA.

Lema anaona chochote anachofanya nje ya maamuzi rasmi ya chama anakifanya kwa nia njema na kwamba hakuna mpumbavu yoyote anayeweza kumuhoji. Leo amesema bila yeye, Heche asingefika pale na kwamba hakuna mtu mwingine yoyote (akiwemo Lissu) anayeweza kuclaim otherwise. Yaleyale ya Denzel Trainer na Doumbia yanajirudia.

Moja ya kitu cha kwanza Tundu Lissu anatakiwa afanye kuanzia sasa, ni kujiweka mbali na kuvunja ukaribu wote na Godbless Lema.
 
Yaani Lema awe na ushawishi kuliko Iissu? Wakati JK alitamka wazi na hadharani, ni heri uwe na wabunge 100 wa upinzani bungeni, kuliko LISSU m1 pekee yake.

Hata Mbowe anafahamu Mziki wa Lissu.
Sikupingi. Ninachosema ni Lema anaamini kwamba yeye ndiye aliyewaweka pale juu Lissu na Heche.

Mtu wa namna hiyo anaamini anawamudu hao viongozi na amewaaminisha watesi wao kuwa kupitia yeye, anaweza kuwashawishi au kuwacontrol kwa jinsi wanavyotaka hao watesi wao.

Halafu issue ya Lissu kwa kauli ya Kikwete siyo ushawishi, ni kwamba siyo mtu anayeweza kuyumbishwa au kuhongwa kirahisi.
 
Labda hao wengine, kwa Lissu hamuwezi abadani.
 
lema,F.A.M ni wapumbavu flani wanao tanguliza maslai yao
 
CDM mlifanya ujinga sana kuwapa chama wanaharakati mange na sarungi. Huo mtego hamtoki leo wala kesho. Kama mnaakili jitengeni nao sasa kwa huu upepo wa Lema.
 
Yaani Lema awe na ushawishi kuliko Iissu? Wakati JK alitamka wazi na hadharani, ni heri uwe na wabunge 100 wa upinzani bungeni, kuliko LISSU m1 pekee yake.

Hata Mbowe anafahamu Mziki wa Lissu.
Heche na Lissu wanatakiwa kumpuuza tu Lema, maana kwa sasa Lema anatapatapa hasa baada ya usaliti wake kufichuliwa.
 
CDM mlifanya ujinga sana kuwapa chama wanaharakati mange na sarungi. Huo mtego hamtoki leo wala kesho. Kama mnaakili jitengeni nao sasa kwa huu upepo wa Lema.
CDM ndiyo nini?
 
Heche na Lissu wanatakiwa kumpuuza tu Lema, maana kwa sasa Lema anatapatapa hasa baada ya usaliti wake kufichuliwa.
Hakika kabisa. Na hao Iissu na Heche hawana mpango nae huyu Meku mfika bei. Lol
 
Yaani Lema awe na ushawishi kuliko Iissu? Wakati JK alitamka wazi na hadharani, ni heri uwe na wabunge 100 wa upinzani bungeni, kuliko LISSU m1 pekee yake.

Hata Mbowe anafahamu Mziki wa Lissu.
Aliongelea wapi hayo?
 
Ndo ushawishi wenyewe huo
Lisu anakubalika sana kwa ukweli wake
 
Lissu amekijenga chama, Lema amejengwa na chama!!. Sasa huyu lema si sawa na shoga Lokole tu!.
 
CDM mlifanya ujinga sana kuwapa chama wanaharakati mange na sarungi. Huo mtego hamtoki leo wala kesho. Kama mnaakili jitengeni nao sasa kwa huu upepo wa Lema.
Utakiwi kuwashtua. Waache walale usingizi wa pono.
 
Yaani Lema awe na ushawishi kuliko Iissu? Wakati JK alitamka wazi na hadharani, ni heri uwe na wabunge 100 wa upinzani bungeni, kuliko LISSU m1 pekee yake.

Hata Mbowe anafahamu Mziki wa Lissu.
Hili liko wazi. Yahani serekali yote haijiamini inamuona mtu mmoja ana uwezo wa kuipindua, uwezo wake si wa kawaida.
 
Lissu amekijenga chama, Lema amejengwa na chama!!!.
Lema ashajiona mkubwa sana kuliko maslahi mapana ya wapenda haki. Pesa za wananchi yaani kodi anazopewa na Abdul kama hongo zimeshamlewesha kabisaaa huyu jamaa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…