SI KWELI Godbless Lema awashauri vijana, wakimaliza kupiga kura, warudi nyumbani wakalale

SI KWELI Godbless Lema awashauri vijana, wakimaliza kupiga kura, warudi nyumbani wakalale

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Source #1
View Source #1
1761710786801.png
 
Tunachokijua
Godbless Lema awali aliteuliwa kuwa mjumbe wa kamati kuu ya Chama cha Demokrasia na maendeleo CHADEMA kabla ya uteuzi wake kutenguliwa na Msajili wa vyama vya siasa, na kisha baadaye kuteuliwa tena kwa ajili ya kukaimu nafasi hiyo kwa kipindi cha mwaka mmoja.

Lema ni miongoni mwa wanachama wa CHADEMA wenye ushawishi mkubwa kwa watu wengi kutokana na dhamira yake ya kupigania demokrasia, uwajibikaji na haki za binadamu. Kumekuwepo na taarifa inayisambazwa mtandaoni ikidaiwa kuchapishwa na Lema kwenye mtandao wa X akisema,

"Watu wajinga ni Mtaji kwa watu wenye akili timamu naona kuna vijana wanajisahau sana labda niwakumbushe, Wakati unawaza kuamka kesho asubuhi kwenda kuleta vurugu au kuharibu jambo fulani fikiria anayekutuma kwanza amebeba dhamira gani juu yako kama kweli wanaosema kesho mkafanye jambo lolote baya ni wenzenu waambieni na wao wawe miongoni mwenu ili kama virungu mpigwe wote.

Nawashauri Vijana wa leo mimi kaka yenu kesho ukimaliza kupiga kura rudi nyumbani kalale achana na ujinga ambao hautakuwa na manufaa kwako wala familia yako"


Je, ni upi uhalisia wa taarifa hiyo?


Ufuatiliaji uliofanywa na JamiiCheck kwa kutumia utafutaji wa maneno muhimu (Key Word Search) picha ya chapisho hilo si ya kweli kwani ujumbe huo haujachapishwa na Lema kupitia ukurasa wake kwenye mtandao wa X kama inavyoonekana.

Kumbuka wapotoshaji wanaweza kutumia utambulisho wa mtu maarufu au kiongozi wa kisiasakutengeneza na kusambaza taarifa isiyo ya kweli kwa lengo la kupotosha.​
Iwe kweli ama tofauti, Yeye ni nani mpaka kuwapangia watu nini cha kufanya na kufikiri?
 
Chadema wenye akili wawili tu siku hizi, Godbless Lema na Sugu. Mbowe alikuwa watatu wao.
 
Nasikitika sana kuona mpaka saivi sijaona kima yoyote aliyeingia barabarani ngoma bado bila bila 😂
 
Back
Top Bottom