Uchaguzi 2020 Godbless Lema azindua kampeni kwa Kishindo, uwanja watapika, Wananchi wajazana kupita uwezo wa eneo husika

Uchaguzi 2020 Godbless Lema azindua kampeni kwa Kishindo, uwanja watapika, Wananchi wajazana kupita uwezo wa eneo husika

Huwa nashangaa huyu mtu ni sifa gani zimemsababisha akawa mbunge wa Arusha...ila nadhani kwasababu kipindi kile cha2010-2015 watu walikuwa washabiki wamabadiliko kiasi kwamba, hata mbuzi angekuwa mgombea kwa wakati ule angepita tu..ndio kipindi hicho jamaa akatumia fursa kupata hii nafasi.
2010-2015,2015-2020 na bado atapita tena 2020-2025!Sijui hapo utasemaje!!!😁
 
Unajua zamani Arusha walikuwa wanataka tu mabadiriko ndio maana waliwahi chagua mpaka Mzee wa mitulinga Makongoro sasa huyu naye chalii wa chinja chinja pale kilombero akapitia hapo hapo.Arusha sasa inahitaji mtu mtulivu ambaye ataleta maendeleo.ule mji wa utalii kwahyo wavuta bangi, wanywa viroba na mirungi muda wao umeisha
Utateseka sana!!!!Maumivu yakizi kanywe chimpumu!
 
Huu uchaguzi utakua na ushindani mkubwa sana hapo Arusha mjini kuanzia nafasi ya ubunge mpaka kwa madiwani...

Ila Ccm kwa sasa imejiimarisha sana hapo Arusha mjini tofauti na miaka ya nyuma hivyo lolote laweza kutokea.

Kata kama Ngarenaro,Sombetini, Sokon one, Sinoni,Muriet kama zitaenda Ccm hakuna atakayeshangaa.

.... Arusha ni jiji zuri sana tena sanaaaaaa kama litapata mbunge makini,mchapakazi na baraza la madiwani makini na wenye maono.

....yoyote atakayeshinda kila laheri kwake.
 
Arusha watakuwa wapumbavu sana kama wataamua kuchagua Mwanaharakati(Lema) badala ya Kiongozi (Gambo), Lema hawezi tena kuibadili Arusha ila Gambo anaweza leta changes kubwa sana mimi nilijiandisha Arusha na mwezi wa kumi ntatoka huku nilipo ili nije kumpa Kura yangu Rais magufuli na Mbuge Mrisho Gambo, Siwezi kuwa mjinga nichague Genge la wahuni sijui kamanda wa Anga ni ujuha
Kura yako itapunguza ushindi wa Lema kwa 0 .001%!So huna madhara!
 
Hapo vipI!

Lema leo amezindua kampeni zake pale soko kuu Arusha. Na amechagua sehemu ambayo ina highest interaction ya watu kwa kipindi chote.

Hii tafsiri yake nini?
Kwanza, hajiamini ya kwamba bado anakubalika, hivyo ili kuepuka aibu ya mwaka imembidi ajipenyeze sokoni.

Pili, amegundua yakwamba kwa sasa wana waarusha wamemshtukia na wamemchoka na hizo siasa zake za kihuni..hivyo ameamua kufanya hivyo kuificha aibu.

Tatu, akili yake ni sawa na mvuta bangi anayejificha nyuma ya sahani ya ugali, akiamini yakwamba haonekani.

Ukweli nickwamba hii ni ishara inayomuashiria taa nyekundu. Watu wa Arusha wameshamchoka na siasa za kihuni na harakati zake kwenye jiji hili la Arusha. Lema anaelewa siasa zake za mbege zimepelekea jiji la Arusha likadumaa kama vile Kilimanjaro.

Kitendo cha Lema cha kuanza kutafuta ujomba kwa Mrisho Gambo ni ishara ya kujitengenezea mazingira salama baada ya kukabidhi kijiti kwa Gambo.

Na mshauri ajiandae kisaikolojia na ampigie Gambo kampeni kwasababu tumaini la wana wa Arusha Lipo kwa CCM.View attachment 1563991
sema tunmaini lako wewe ni ccm usitujumuishe wote mbona ni kama unatsemea
 
Arusha ni jiji zuri sana tena sanaaaaaa...kama litapata mbunge makini, mchapakazi na baraza la madiwani makini,watendaji na wachapakazi.

... Kila laheri wakazi wa Arusha...Mungu awaongoze mfanye maamuzi sahihi kwa mustakabali mzuri wa Jimbo lenu na taifa kwa ujumla.
 
Anaewaalika wasanii kwenye mikutano yake,
1.Ana sera zisizo endana na maisha halisi ya wananchi,
2.Hapendwi ila analazimisha tu
3.Hana mvuto,kachuja kifupi hana jipya
4.Anaishia kugawa kofia,kanga na tisheti kama hongo ili achaguliwe.
TAKUKURU wamezuia rushwa ya ubwabwa wa kufirika ila kanga,kofia,barabara na madaraja wakati huu wa kampeni hawavioni.
Rushwa hapa Tanzania inategemea mtoaji ni nani.
 
Natumai hukuumia tu bali ulipatwa na uchungu kabisa, vipi leba ulienda na ulijifungua ka kike au kiume??
uzuri wa kampeni za ubunge hazidanganyi,atakapoanza kwenda kata kwa kata hapo ndipo atakapoadhirika kama Mdee alipolazimika kusimama juu ya matofali,nimeumia sana mimi
 
Ccm itawachukua miaka 100 kuelewa strategy ya Lema na Kwa nini Lema huwa anashinda Arusha!!

Lema anapiga kambi kwenye kundi ambalo ndo mtaji wa CCM. Kwa hiyo kamwe hamtomweza
 
Ccm itawachukua miaka 100 kuelewa strategy ya Lema na Kwa nini Lema huwa anashinda Arusha!!

Lema anapiga kambi kwenye kundi ambalo ndo mtaji wa CCM. Kwa hiyo kamwe hamtomweza
Kwa kipindi hichi anatumia mbinu za kitoto sana.
 
Back
Top Bottom