Godbless Lema: Bashiru alitaka kunilipia deni nihamie CCM

Godbless Lema: Bashiru alitaka kunilipia deni nihamie CCM

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Kanda ya Kaskazini, Godbless Lema ametoboa siri aliyekuwa Katibu CCM, Ally Bashiru kutaka kumlipia deni alilokuwa anadaiwa bungeni kwa lengo la kumtaka ajiunga na chama hicho. Hata hivyo alikataa kulipiwa deni hilo na kudai ni heri auze figo alipe.

Lema ameibua hayo jana Aprili 28, 2023 wakati akizungumza na wananchi wa Manispaa ya Moshi katika soko la Manyema kwenye moja ya mikutano ya hadhara ya chama chake.
Kwani kubadili dini/itikadi ni kosa?Acha kutafuta popularity kaka!

Sent from my Infinix X6511B using JamiiForums mobile app
 
Hizi ndio sababu za ndani kwanini hawa jamaa wanaupigania ubunge usiku na mchana, huwezi kuwa na madeni halafu uporwe ubunge wako ubaki na amani na kumpenda yule aliyekupora.

Habari za haki zao hizo ni sababu za nje tu, naona wengine tuendelee kuwa bendera fuata upepo, sio kesi..
 
Back
Top Bottom