Lema ni mtumishi wa Mungu, ameonesha uadilifu wa hali ya juu sana.
Lema anafaa kuchukua nafasi ya Mrema na katibu mkuu abaki kuwa John Mnyika mpaka 2026.
Baada ya hapo basi anaweza akaingia kuwa KM na Mnyika akachukua nafasi ya Lema tena .
Sio vizuri kuwaondoa wote wakati huu . Kundi la Mbowe ni muhimu sana kubaki kwenye uongozi kama sehemu ya maridhiano ya kweli tofauti na maridhiano feki ya CCM na wapinzani .
Wanasema maridhiano lakini wanakataa maamuzi rahisi kabisa ya wananchi.
Kwa mtu mtenda haki hata kama ni ndugu yako wa kuzaliwa akikosa kura unatakiwa umwambie ukweli kwamba bwana nimejirahidi kukusaidia lakini watu wamekukataa kwenye kura . Vumilia kwa sababu serikali ina teuzi na nafasi nyingi nitkuteua kwenye nafasi nyingine ili amani na upendo vitawale. Kama alivyo onyesha Mbowe .
Lakini CCM walekua na ushetani mkubwa wa kubadili kura jambo ambalo kwa misingi ya asili na hata dini ni kosa na dhambi kubwa na kwa sababu wameihalalisha ndio maana inageuka kuwa laana kwa nchi sasa. Wizi wa kura haufai . Kura ni agizo la kimungu kuondoa na kuamua kwenye mabishano .
Zamani hata kupata watumishi wa Mungu ilikua kwa kura. Sasa kama wizi ungekuwa unafanywa basi kazi ya Mungu ingetiwa doa .Wakristo wanaelewa uchaguzi wa nafasi ya kumrithi Yuda Iskari Yote aliyemsaliti Yesu . Kura zimiamua .
Ni aibu na dhambi kwa wanadamu kuvuruga uchaguzi .