Rula ya Mafisadi
JF-Expert Member
- Dec 28, 2024
- 404
- 852
====
Swali moja la msingi kwa WAJUMBE wa CHADEMA ni hili ,
Ikiwa utapewa pesa , usafiri , pombe na chakula wakati huu lakini hukuletewa pesa wakati wa uchaguzi wa serikali za Mitaa , Kijiji na Vitongoji ,
Je hizo pesa sasa zinatoka wapi ? Na wanaotoa pesa wananunua kura kwa sababu gani kwa kazi isiyo hata na mshahara ?
CHADEMA sio duka wala Bar ni taasisi ya walioumizwa Wajumbe sikilizeni , hiki CHAMA kina damu za rafiki zenu , maumivu makubwa na mateso kwa watu wengi,
Msilaani maisha yenu kwa starehe na rushwa za muda mfupi.
Sasa basi wakileta pesa kula , kunywa halafu waadhibu katika boksi la kura.
Nyie sio Blue Band wakubebwa kama Maboksi.
Sikilizeni, Upinzani ni tabia njema na sio rangi za nguo.
Msiue matumaini ya Taifa kwa kushindwa kutofautisha tabia zetu na CCM.
Godbless Lemma,